Alisema
serikali imeamua kuwapunguzia mzigo wa masomo wanafunzi ili waweze
kumudu masomo yao. Pia kwenye sera mpya ya elimu mtoto wa darasa la pili
hawezi kwenda la tatu kama hajui kusoma, kuandika na kuhesabu na
atalazimika kurudia darasa mpaka afahamu.
Awali,
mbali ya masomo hayo matatu, walikuwa wanasoma pia Kiingereza, Sayansi,
Haiba na Michezo na Stadi za Kazi. "Sera mpya ya elimu ni bora lakini
unashangaa leo mtu anasimama na kuikosoa.
Mtu wa
aina hiyo ni wa kusamehewa tu. "Tumeamua kuwapunguzia mzigo wa masomo
wanafunzi wa darasa la kwanza na la pili ambapo sasa watasoma masomo
matatu ili kuimarisha uelewa wao na kuzingatia masomo na kama kuna kitu
kitakachoongezwa bali ni elimu ya afya tu," alisema.
Alifafanua
kwamba programu ya stadi za kusoma, kuandika na kuhesabu inalenga
katika kuboresha elimu kwa watoto wote wenye umri kati ya miaka mitano
hadi 13 nchini katika ngazi za elimu ya awali na msingi, elimu nje ya
mfumo rasmi kwa watoto walio katika mazingira hatarishi na elimu ya
malezi (Chekechea) kupitia vyuo vya maendeleo ya wananchi.
Naibu
Waziri alisema programu hiyo imelenga katika maeneo matano ikiwemo
kuwawezesha watoto wa shule za awali na msingi kusoma, kuandika na
kuhesabu.
Pia
kuwawezesha watoto ambao hawapo katika mfumo rasmi wa elimu katika
masomo ya awali na msingi kuweza kusoma, kuandika na kuhesabu, kuongeza
uelewa wa watoto wadogo ili kuwawezesha kuingia madarasa ya awali
mapema.
Alisema
malengo mengine ni kuimarisha mfumo wa elimu na watendaji wake katika
maeneo ya mipango, uratibu na uongozi kwa lengo la kuwezesha utoaji wa
elimu bora pamoja na kuongeza ushiriki wa jamii katika kuwezesha
ujifunzaji wa watoto na ufundishaji wa stadi za kusoma, kuandika na
kuhesabu.
Walimu
wazamia semina Wakati huohuo, takribani walimu 1,000 wanaodaiwa kuzamia
semina ya mtaala mpya inayoendelea mjini hapa, wametakiwa kuondoka kwa
kuwa hawana mialiko maalumu. Naibu Waziri Majaliwa akizungumza na walimu
hao juzi wakati wa kufungua mafunzo hayo, alisema kama kuna mwalimu
anajijua amefika kwenye semina hiyo bila kufuata utaratibu ni bora
ajiondoe mwenyewe, si kusubiri mpaka aondolewe.
Alisema
idadi ya walimu walioalikwa kwenye semina hiyo, imezidi na hiyo inafanya
washindwe kupatiwa mahitaji muhimu kama malazi na chakula.
"Nasikia
kuna walimu wamekuja kuwakilisha walimu wengine, waliona tabu kupeleka
barua kwenye shule husika na kuamua kuteua watu wao kuja hapa," alisema
na kuongeza, "Hapa tulihitaji walimu ambao wanafundisha darasa la kwanza
na la pili tu, lakini kama umekuja ukiwa hufundishi masomo hayo ukitoka
kwenye mafunzo haya lazima ukafundishe masomo hayo," alisema.
Pia,
alisema inawezekana kuna walimu wakuu wamekuja kwenye mafunzo hayo na
kuacha wahusika ambao ni walengwa wakubwa wa mpango huo. Kaimu Katibu
Mkuu Tamisemi, Mohamed Pawaga alisema mafunzo hayo yalilenga washiriki
4,430, lakini washiriki waliofika zaidi ya 5,000.
Alisema
hali hiyo imeleta mkanganyiko mkubwa katika kuwahudumia, lakini
kinachofanyika ni kuhakiki taarifa zao ili wale wanaostahili wabaki na
wale wasiostahili kushiriki mafunzo hayo, warudi kwenye vituo vyao vya
kazi.