Jumatano, 29 Aprili 2015

CLOUDS

CLOUDS FM YASHINDA TENA TUZO YA UBORA YA SUPERBRAND KWA MARA YA TATU AFRIKA MASHARIKI.

 Picha ya pamoja ya baadhi ya makapuni binafsi waliopewa tuzo bora za
viwango,kutoka shoto ni Bi.Dorothy Mashamsham kutoka kampuni ya Mafuta
ya PetrolFuel,Mkurugenzi Mtendaji wa ITV/Radio One Bi Joyce
Mhaville,Mkurugenzi wa Uzalishaji na Vipindi Clouds Media Group Bwa.Ruge
Mutahaba,Meneja Masoko Bwa. Elisa Ernest kutoka kampuni ya bima ya
Alliance Insurance.
 Mkuu wa Kitengo cha Idara ya Uchambuzi wa viwango Afrika Mashariki,Bwana
Jawad Jaffer akiwa na baadhi ya viongozi wa juu wa kampuni ya Clouds
Media Group,kutoka kulia ni Mkuu vipindi wa Clouds FM Sebastian
Maganga,wa tatu ni Mkurugenzi wa vipindi na Uzalishaji Ruge Mutahaba na
Mkuu wa kitengo cha huduma,Promosheni na Tamasha Clouds Media Group.Bi
Fauzia Kullane.
 Mkuu wa Kitengo cha Idara ya Uchambuzi wa viwango Afrika Mashariki,Bwana
Jawad Jaffer akimkabidhi tuzo bora ya viwango Mkurugenzi wa Uzalishaji
na vipindi wa Clouds Media Group,Bwa. Ruge Mutahaba,kwenye hafla fupi ya
utoaji tuzo bora za viwango hizo iliyofanyika ndani ya hotel ya Hyatt Regency jijini Dar.
 Mkurugenzi wa Uzalishaji na Vipindi Clouds Media Group,Ruge Mutahaba akizungumza jambo  na Mkuu
wa Kitengo cha Idara ya Uchambuzi wa viwango Afrika Mashariki,Bwana Jawad Jaffer.
 Mkurugenzi wa Uzalishaji na vipindi wa Clouds Media Group,Bwa. Ruge Mutahaba akiishukuru taasisi
ya SUPERBRAND East Africa mbele ya wageni waalikwa na waaandishi wa
habari kwa kutambua ubora wa kituo cha redio hiyo na kuipa tuzo bora za
viwango katika Afrika Mashariki kwenye hafla fupi ya utoaji tuzo hizo
iliyofanyika ndani ya hotel ya Hyatt Regency jijini Dar.
 Baadhi ya Wageni waalikwa na wanahabari wakifuatilia jambo kabla ya utoaji
tuzo bora za viwanga a.k.a SUPERBRAND kwa makampuni binafis nchini
Tanzania.
Mkurugenzi wa Uzalishaji na Vipindi kutoka Clouds Media Group,Ruge Mutahaba akiwa amepozi na Mtangazaji wa ITV Bwa.Godwin Gondwe
 
…………………………………………………………………………….
KAMPUNI ya Clouds Media Group imeendelea kuwa kinara kwa ubora wa SuperBrand kwa mara ya tatu katika nchi za Afrika Mashariki.
 
 Mkuu wa Kitengo cha Idara ya Uchambuzi wa Viwango Afrika Mashariki,Jawad
Jaffer amesema kuwa matokeo ya utafiti huo ulizingatia maoni ya watalaam
wazoefu wa masoko na walengwa wa huduma za bidhaa ambao wanahaki ya
kuamua aina ya haki ya viwango bora vya superbrands na kupongeza
makampuni ambayo yamefanikiwa kuingia 20 bora.
 
Utafiti
huo umefanywa na idara ya uchambuzi wa viwango  makao makuu nchini
Uingereza kutokana na kuzingatia ushauri wa wataalam wa masoko  na maoni
ya watumiaji bidhaa zaidi ya 600 wa huduma hizo.
Amesema kampuni nyingi zilizoingia katika ubora wa superbrands ni 1000
zikapambanishwa na kufanya kampuni 20 ziingie katika ubora superbrands
na kufanya kampuni Clouds Media Group kuendelea kushikiria nafasi ya
jsu  kwa mwaka wa 2015 -2016.
 

POSTED BY; RASHID  HAMZA

RAISI KIKWETE

Rais Kikwete Azindua Meli Mbili Za KIVITA Kwa Kishindo Jijini Dar


RAIS Jakaya Kikwete, jana amezindua na kuzitunukia Kamisheni meli mbili za kivita za Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania Kamandi ya Wanamaji ambazo zitatumika kufanya doria na kulinda mipaka ya majini katika Bahari ya Hindi.


Meli hizo zimepewa majina ya P77 Mwitongo na P78 Msoga zenye urefu wa mita 60 na zina uwezo wa kufanya doria katika kina kirefu cha maji.


Rais Kikwete alisema, kupatikana kwa meli hizo kumeifanya Tanzania kuandika ukurasa mpya wa uhusiano kati yake na China ambao uliasisiwa na waasisi wa mataifa hayo hayati Mwalimu Nyerere na Mao Tse Tung.


Alisema meli hizo zimekuja nchini kwa msaada wa Serikali ya Watu wa China zikiwa na uwezo wa kubeba silaha nzito kila moja ikiwa na mizinga miwili mikubwa na midogo sita.


"Jeshi letu la Wanamaji wakati linaanzishwa 1971, lilisaidiwa na Serikali ya China meli 13, rada na wataalamu wetu kupatiwa nafasi mbalimbali za mafunzo...meli hizi zitatuongezea ulinzi katika mipaka yetu majini.


"Kilio kikubwa cha jeshi letu kilikuwa uwezo mdogo wa meli zetu, tumekuwa na kazi ya kutafuta meli hizo na sasa tuna mpango wa kuchukua meli nyingine kubwa zaidi zenye uwezo, kilichobaki ni taratibu za kifedha tu," alisema Rais Kikwete.


Aliongeza kuwa, lazima Tanzania ijenge uwezo wa kulinda mali zetu, mipaka, samaki na mitambo ya gesi ambayo imesimikwa baharini hivi karibuni.


Kwa upande wake, Waziri wa Ulinzi, Dkt. Hussen Mwinyi, alisema Serikali ya China imekuwa msaada mkubwa kwa Tanzania.


Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Davis Mwamunyange, alisema jeshi hilo limepiga hatua katika ununuzi wa dhana za kivita na kuendeleza mafunzo ya kijeshi.

Amiri Jeshi Mkuu Rais Jakaya Mrisho Kikwete akikagua mara baada ya kuzindua rasmi meli vita mbili za doria bahari kuu TNS Msoga na TNS Mwitongo kwenye sherehe zilizofanyika Kamandi ya Jeshi la Maji Kigamboni jijini Dar es salaam jana April 28, 2015

Amiri Jeshi Mkuu Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipata picha ya kumbukumbu na makamanda wa meli vita mbili za doria bahari kuu TNS Msoga na TNS Mwitongo kwenye sherehe zilizofanyika Kamandi ya Jeshi la Maji Kigamboni jijini Dar es salaam jana April 28, 2015

Amiri Jeshi Mkuu Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Chifu Edward Wanzagi wa kabila la Wazanaki (kati) pamoja na Mbunge wa Afrika Mashariki Mhe Makongoro Nyerere baada ya kuzindua rasmi meli vita mbili za doria bahari kuu TNS Msoga na TNS Mwitongo kwenye sherehe zilizofanyika Kamandi ya Jeshi la Maji Kigamboni jijini Dar es salaam jana April 28, 2015.

 

(PICHA NA IKULU)

 

POSTED BY;RASHID HAMZA

KIGOMA YETU

Majambazi Matatu (3) Yauawa na Jeshi la Polisi Mkoani Kigoma


JESHI  la Polisi Mkoani Kigoma limefanikiwa kuuwa majambazi watatu baada ya kurushiana risasi na kukamata silaha mbalimbali za kivita.

Akizungumzia tukio hilo ofisini kwake Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kigoma,Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Frednand Mtui alisema kuwa majira ya saa nane usiku katika eneo la  mto kahabwe mpakani mwa Wilaya ya Kakonko na Kibondo, askari Polisi wakiwa doria walirushiana risasi na majambazi ambao idadi yao haijajuikana na kufanikiwa kuwauwa majambazi watatu.

Alisema wamefanikiwa kukamata silaha moja aina ya AK.47 yenye namba 10363 ikiwa na risasi 11 ndani ya magazine na risasi 22 za SMG ndani ya mfuko wa rambo pamoja na mabomu 2 ya kutupa kwa mkono .

Kamanda Mtui alisema kuwa aina ya mabomu waliyokutwa nayo majambazi hao ni offensive handgrenade namba Y.3PM-2 na jingine ni aina  ya deffensive handgrenade ambalo namba zake hazisomeki.

''Leo ilikuwa ni siku ya mnada hivyo inaonekana majambazi hao walijipanga kwenda kupora mali na pesa katika mnada wa leo,tunawashukuru raia wema kwa kutoa taarifa mapema na kufanikiwa kuwanasa majambazi hao na kuwauwa''alisema Kamanda Mtui

Alisema maiti za majambazi wote watatu ambao majina yao hayajafahamika ila wote wana umri kati ya miaka 25-35 zimehifadhiwa katika Wilaya ya Kibondo na upelelezi wa tukio hilo unaendelea.

POSTED BY; RASHID HAMZA