Alhamisi, 2 Aprili 2015

Thursday, April 2, 2015

Athari 12 Za Sheria Mpya Ya Masuala ya Mitandao ( Tanzania Cybercrimes Act, 2015 ) Iliyopitishwa Jana Bungeni......Athari Hizi Zimechambuliwa Na Mbunge David Kafulila

Sheria hii ni muhimu duniani kote na ndio maana hata Tanzania ilikuwa inangojea kupata sheria ya kuongoza masuala ya mitandao yaani Cyber Law kutokana na uhalifu wa aina mbalimbali wa masuala ya mitandao.


Sifa kuu ya sheria ya kuongoza masuala ya mitandao ni kuweka bayana makosa ya mitandaoni na pia kuyatolea adhabu. Sheria hii inayopitishwa kwa dharura madhara yake ni:

Moja, Kifungu 7 (2b): Mpokeaji wa ujumbe (receiver) anaweza kushtakiwa kwa kosa la kupokea ujumbe ambao sheria imeufanya kuwa wa jinai. (Mfano: Mtu akikuforwadia ujumbe, ukiupokea na wewe umefanya kosa la jinai).

Pili, Kifungu 21(1): Mtumia mtandao wa Intaneti yeyote hayuko salama kwani mtoa huduma wake analazimika kutoa habari zake kwa serikali pale zitakapohitajika (kwa lazima).

Tatu, Kifungu 8: Itakuwa ni kosa la jinai kama mtu ataweka wazi nyaraka za siri za serikali hata kama ni nyaraka ya kusaidia nchi kwa ujumla (Mfano: Matumizi mabaya ya mali ya umma).

Nne, Kifungu 14: Picha yoyote yenye mwelekeo unaoweza kuonekana kama ‘mchafu kingono’ inaweza kupelekea mtu kufungwa hadi miaka 10 au kulipa milioni 30; Sasa kama mtu kaweka picha yake Instagram ambayo sio ya ponografia lakini ‘ikatafsiriwa’ hivyo. Sheria haijatafsiri ponografia!

Tano, Kifungu 23: Je, ulijua kuwa ‘kusababisha maudhi ya hisia’ kwa mtu mwingine ni unyanyasaji na unaweza kufungwa kifungo kisichopungua mwaka mmoja?

Sita, Rejea adhabu ya ibara mbalimbali: Sheria hii kila kosa linaweza fanya mtu afungwe kifungo hadi cha maisha na kulipa pesa hadi zisizohesabika kwani hakijawekwa kikomo cha juu cha adhabu bali kikomo cha chini tu kwa Kiingereza “not less than”

Saba, Sheria haijaeleza vizuri suala la kutumia jina lisilo lako kwenye mtandao na hivyo mtu anaweza kushitakiwa kama kuna mtu mwingine mwenye jina kama hilo katika maisha halisi.

Nane, Serikali kupitia waziri husika ndio ina mamlaka ya kusema jambo lililowekwa kwenye mtandao ni la kweli, uongo au la kupotosha. Kumbuka hata ESCROW, EPA walisema ni uwongo; ni wangapi katika mtandao wangeshtakiwa kiuonevu kwa hili?

Tisa, Kifungu 22: Ukiweka ujumbe katika mtandao na ukaufuta au kuuboresha, kama ukishtakiwa kwa kuweka ujumbe huo unaweza kuhukumiwa pia kwa adhabu ya kuuboresha au kuufuta. Ni mara ngapi unafuta ‘status’ zako za WhatsApp? Unaweza shtakiwa kwa kuchelewesha ushahidi kisa tu ulifuta na hamna mtu anayeweza kujua ulifuta kwa kusudi au la.

Kumi, Mkuu wa kituo cha Polisi chochote kile nchini anaweza kuagiza wewe umpatie simu/laptop yako au taarifa zako zote (kwenye email, chats) au hata vifaa vyako au ofisi yako kwa ajili ya upelelezi bila oda ya Mahakama.

Kumi na moja, Kifungu 31 (3a): “As soon as practicable” the law states. Askari Polisi wakichukua vitu vyako wanaweza kukupatia listi ya vitu walivyovipokea muda watakaoona kwao inawezekana kufanya hivyo. Jiulize, inaweza chukua muda gani?

Kumi na mbili, Kifungu 31-35 & 39-45: Kama wewe ni Blogger au mtoa huduma ya mtandao, pale unapobaini kosa ukalitoa na uko katika mikakati ya kuitaarifu mamlaka husika (Kama sheria inavyosema), askari naye anaweza kwa wakati huohuo akaja kukagua na kuchukua vitu vya kazi zako, hivyo sheria inakinzana yenyewe kwa yenyewe. Blogger yuko sawa kisheria na askari yuko sawa kisheria.

Je, sheria hii ikisainiwa na Rais Jakaya Kikwete tutapona?

DAVID Kafulila
Mbunge wa Kigoma Kusini (NCCR-Mageuzi) 
 
POSTED HASSAIN MTUNDA

Thursday, April 2, 2015

Breaking News:Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Yaahirisha Kura ya Maoni Ya Katiba Mpya.....Zoezi La Uandikishaji Kuendelea Hadi Mwezi Wa 7


Tume ya Taifa ya uchaguzi (NEC) imesema kuwa kura ya maoni ya katiba inayopendekezwa, haitaweza kufanyika tena tarehe 30 April hadi hapo itakapotangazwa tarehe nyingine tena.
 
Akizungumza na waandishi wa habari  leo  mchana, mwenyekiti wa tume ya uchaguzi , Jaji Mstaafu Damian Lubavu amesema sababu ya kuhairisha kura hiyo April 30 ni kutokana na kutokamilika kwa zoezi la uboreshaji daftari la kudumu la wapiga kura  kutokana na changamoto za mashine za BVR.

Jaji  Lubavu  amesema zoezi la uandikishaji mkoa wa Njombe litakamilika April 18 na baada ya hapo itafuatia mikoa ya Ruvuma, Iringa, Mtwara na Lindi ‪. Vifaa vya kuandikishia (BVR kits) nyingine 248 zitawasili ndani ya wiki ijayo na vingine 1600 vitafuata baada ya muda mfupi. 
 
Pia,  amesema kama vifaa vya kuandikishia vitafika vyote zoezi la uandikishaji litakamilka ifikapo mwezi julai mwaka huu.
 
Jaji  Lubavu  ameainisha  kuwa Gharama za vifaa vyote vilivyoagizwa kwaajili ya vifaa vya kuandikishia (BVR kits) ni dola za Kimarekani milioni 72 ambazo ni sawa na Tsh bilioni 13,338,520,536
 
POSTED BY ; RASHID HAMZA

KINANA : MIAKA 20 YA USHABIKI WA KISIASA MOSHI MJINI INATOSHA

Tuesday, March 31, 2015

  • Wafanyabiashara wafunga barabara

  • Walalamikia kufungiwa soko la kati kwa mwaka mzima

  • Kwa miaka 20 upinzani hamna walilofanya Moshi mjini

  • Nape awaambia stukeni wananchi,chagueni viongozi watakaowaletea maendeleo

 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia vijana wa boda boda ,Stendi Kuu kata ya Mawenzi ambapo aliwaambia kuwa boda boda ni sehemu ya kupata kipato hivyo inabidi wafanye shughuli yao hiyo kwa umakini mkubwa ,ikiwa kudumisha umoja, kufuata sheria, kujisajiri na kutambulika na mamlaka husika ,kuaminika ili waweze kukopesheka.

 Katibu wa Umoja wa Boda Boda Moshi mjini akisoma risala kwa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana kwenye mkutano uliofanyika ,Stendi Kuu kata ya Mawenzi Moshi mjini.

 Wafanyabiashara wa soko la kati,Moshi mjini wakiwa wamefunga njia kuzuia msafara wa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana usipite mpaka wawasilishe kero yao ya kufungiwa soko kwa mwaka mzima na uongozi wa halmashauri ya mji kwa maelezo ya kupisha ukarabati ambao haujafanyika.
 Katibu wa Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akisoma ujumbe ulioandikwa kwenye mabango na wafanyabiashara wa soko la kati,Moshi mjini.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisoma risala ya wafanyabiashara wa soko la kati,Moshi mjini.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na wafanya biashara ambao soko lao limefungwa kwa zaidi ya mwaka mmoja sasa.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiongozana na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye kuingia kwenye soko la kati, Moshi mjini mkoani Kilimanjaro ambalo lilifungwa kupisha ukarabati ambao mpaka sasa ni mwaka 1 hakuna kilichofanyika na wafanyabiashara wanaishi maisha magumu.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na wafanyabiashara wa soko la kati ambalo limefungwa kwa mwaka mzima sasa.
 Ukuta wa soko la kati Moshi mjini ukiwa na matangazo yanayozuia kufanya biashara
 Katibu wa Vikoba kata ya Kongoroni Mariam Chawapoma akisoma risala ya kikundi chao kwa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana .
 Wanachama wa Vikoba wakishangilia jambo wakati wa mkutano na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wanachama wa Vikoba kata ya Makongoroni ambapo alishiriki kuzindua vikoba 11 vyenye wanachama 330,Kata ya Makongoroni,Moshi mjini.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki kufyatua matofali baada ya kutembelea kikundi Vijana cha Kata ya Miembeni
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipokelewa na umati wa akina mama Lishe wa Njoro,Moshi mjini.


 Wajasiriamali na mama lishe wakishangilia ujio wa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana katika kata yao ya Njoro.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wajasiriamali pamoja na mama lishe.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye pamoja na Mwenyekiti wa CCM mkoa Ndugu Idd Juma
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akikatiza kwenye maji wakati akielekea kwenye eneo la mkutano wa hadhara Bomambuzi viwanja vya shule ya msingi Mandela.
 Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa kutoka wilaya ya Moshi mjini Ndugu Aggrey Marealle akihutubia wananchi wa Moshi mjini ambapo aliwaambia kuwa wakati umefika wa kufanya mabadiliko ya kweli kwa kuchagua CCM kuongoza mji wa Moshi.


 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia wakazi wa Moshi mjini mkutano wa hadhara Bomambuzi viwanja vya shule ya msingi Mandela na kuwaambie wastuke sasa wasiendelee kukandamizwa na viongozi wasiojali maendeleo yao.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wananchi wa Moshi mjini kwenye mkutano wa hadhara Bomambuzi viwanja vya shule ya msingi Mandela na kuwaambia kuwa wamekuwa na ushabiki kwa miaka 20 imefika wakati sasa kuamua kuchagua maendeleo kwa manufaa ya maisha yao
  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiangalia picha ya gari alilotumia Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kabala halijafanyiwa ukarabati na Chuo cha Ufundi Veta, Moshi mjini.
  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akijaribu kuendesha gari alilotumia Mwalimu Julius Kambarage Nyerere wakati wa harakati za kutafuta uhuru,kulia ni Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye.
  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiteremka kwenye gari alilotumia Baba wa Taifa wakati wa harakati za kutafuta uhuru.


Wananchi wakiuaga msfara wa  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana mara baada ya mkutano kumalizika kwenye viwanja vya shule ya msingi Mandela,Bomambuzi, Moshi Mjini.

POSTED BY RASHID HAMZA

KUMEKUCHA KENYA

Thursday, April 2, 2015

Hali ni Mbaya Kenya...Al Shabaab Wanadaiwa Kuanza Kuwachinja Mateka Inayowashikila Katika Jengo La Chuo Kikuu Cha Garissa


Baadhi ya wanafunzi waliouawa au kujeruhiwa darasani
**********  
Katika style kama ile ya shambulizi la Westgate Mall, wanamgambo wa al-Shabaab wamevamia na kushambulia  chuo  kikuu  cha  Garissa kilichopo katika mji wa Garissa. Zaidi  ya watu 15 wameuawa, na wengine zaidi ya 90 wamejeruhiwa.

Mkuu wa jeshi la polisi Kenya, Inspector General Joseph Boinnet amesema kuwa magaidi hao walivamia geti kuu la chuo hicho na kuwarushia risasi walinzi alfajiri saa 5.30, wakati wanafunzi wa Kiislam wakienda kwenye swala ya asubuhi.
 
Polisi waliokuwepo chuoni hapo walikimbilia katika eneo la tukio na kuanza kurushiana risasi na magaidi hao, ambao walifanikiwa kuingia kwenye mabweni ya wanafunzi.

Polisi wa ziada na wanajeshi waliitwa kuja kusaidia na mirindimo ya risasi ilisikika kati ya wavamizi hao, polisi na wanajeshi.
 
Wanafunzi waliokuwa wakipiga simu kutoka ndani ya mabweni wamesema kuwa kuna majeruhi wengi sana. 
 
Wanafunzi waliofanikiwa kutoroka wamesema kuwa idadi ya wavamizi hao ni angalau watano  na bado kuna wanafunzi na maprofesa wengi wanashikiliwa mateka.

Taarifa za hivi punde zinaarifu kuwa magaidi hao wameanza kuwachinja baadhi ya mateka waliowashikilia.
 
Mateka mmoja (mwanafunzi) mwenye asili ya Somalia aliyeachiwa huru na magaidi hao ameviambia vyombo vya habari vya Kenya kuwa zaidi ya wanafunzi kadhaa wamekwishauawa na miili yao imetapakaa ndani ya vyumba na madarasa huku zoezi la Uchinjaji wa mateka wengine walio hai likianza.

Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya ametuma salamu za rambi rambi kwa familia za wale waliouawa katika shambulizi hilo.

Kenyatta amewataka wakenya kuwa watulivu wakati huu ambapo maafisa wa usalama wanakabiliana na wapiganaji hao. 

Wanajeshi wa jeshi la Kenya katika geti la chuo hicho


Baadhi ya miili ya marehemu waliouawa katika shambulio la al-Shabaab katika chuo kikuu cha Garissa


Helicopter ya jeshi ikitua na maiti na baadhi ya majeruhi katika kambi ya jeshi la Langata


Wanafunzi wa shule ya sekondari ya Excel, iliopo karibu na chuo kikuu cha Garissa wakiondolewa kutoka shuleni kuhakikisha usalama wao

POSTED BY:RASHID ZAGA