Jumatano, 29 Aprili 2015

KIGOMA YETU

Majambazi Matatu (3) Yauawa na Jeshi la Polisi Mkoani Kigoma


JESHI  la Polisi Mkoani Kigoma limefanikiwa kuuwa majambazi watatu baada ya kurushiana risasi na kukamata silaha mbalimbali za kivita.

Akizungumzia tukio hilo ofisini kwake Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kigoma,Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Frednand Mtui alisema kuwa majira ya saa nane usiku katika eneo la  mto kahabwe mpakani mwa Wilaya ya Kakonko na Kibondo, askari Polisi wakiwa doria walirushiana risasi na majambazi ambao idadi yao haijajuikana na kufanikiwa kuwauwa majambazi watatu.

Alisema wamefanikiwa kukamata silaha moja aina ya AK.47 yenye namba 10363 ikiwa na risasi 11 ndani ya magazine na risasi 22 za SMG ndani ya mfuko wa rambo pamoja na mabomu 2 ya kutupa kwa mkono .

Kamanda Mtui alisema kuwa aina ya mabomu waliyokutwa nayo majambazi hao ni offensive handgrenade namba Y.3PM-2 na jingine ni aina  ya deffensive handgrenade ambalo namba zake hazisomeki.

''Leo ilikuwa ni siku ya mnada hivyo inaonekana majambazi hao walijipanga kwenda kupora mali na pesa katika mnada wa leo,tunawashukuru raia wema kwa kutoa taarifa mapema na kufanikiwa kuwanasa majambazi hao na kuwauwa''alisema Kamanda Mtui

Alisema maiti za majambazi wote watatu ambao majina yao hayajafahamika ila wote wana umri kati ya miaka 25-35 zimehifadhiwa katika Wilaya ya Kibondo na upelelezi wa tukio hilo unaendelea.

POSTED BY; RASHID HAMZA

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni