Mabadiliko mengine kuhusu uchaguzi mkuu Burundi!!
Hali bado si shwari Burundi..hii inatokana na machafuko ya kisiasa yanayoendelea baada ya Rais aliyeko madarakani Pierre Nkurunziza kutaka kuwania kwa muhula wa tatu mfululizo.
Baada
ya kutofikia makubaliano ikiwemo jaribio la kutaka kumpindua
lililofanywa wiki moja iliyopita kushindikana huku watu wakiendelea
kaandamana kushinikiza aondoke.
Rais huyo amehairisha uchaguzi wa ubunge kwa siku kumi .
Msemaji wake Willy Nyamitwe amesema Rais huyo ameahirisha uchaguzi wa Ubunge kwa muda wa siku 10 kufuatia jaribio la mapinduzi.
Awali uchaguzi huo ulipangwa kufanyika
Mei 26 na sasa utafanyika June 2 na umeahirishwa ili kupata muda wa
kuwasikiliza washirika wa kimataifa pamoja na tume ya uchaguzi.
Hadi sasa tarehe rasmi ya uchaguzi wa Urais uliopangwa kufanywa Juni 26 haijabadilika.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni