Thursday, April 2, 2015
Hali ni Mbaya Kenya...Al Shabaab Wanadaiwa Kuanza Kuwachinja Mateka Inayowashikila Katika Jengo La Chuo Kikuu Cha Garissa
Baadhi ya wanafunzi waliouawa au kujeruhiwa darasani |
Katika style kama ile ya shambulizi la Westgate Mall, wanamgambo wa al-Shabaab wamevamia na kushambulia chuo kikuu cha Garissa kilichopo katika mji wa Garissa. Zaidi ya watu 15 wameuawa, na wengine zaidi ya 90 wamejeruhiwa.
Mkuu wa jeshi la polisi Kenya, Inspector General Joseph Boinnet amesema
kuwa magaidi hao walivamia geti kuu la chuo hicho na kuwarushia risasi
walinzi alfajiri saa 5.30, wakati wanafunzi wa Kiislam wakienda kwenye
swala ya asubuhi.
Polisi waliokuwepo chuoni hapo walikimbilia katika
eneo la tukio na kuanza kurushiana risasi na magaidi hao, ambao
walifanikiwa kuingia kwenye mabweni ya wanafunzi.
Polisi wa ziada na wanajeshi waliitwa kuja kusaidia na mirindimo ya
risasi ilisikika kati ya wavamizi hao, polisi na wanajeshi.
Wanafunzi
waliokuwa wakipiga simu kutoka ndani ya mabweni wamesema kuwa kuna
majeruhi wengi sana.
Wanafunzi waliofanikiwa kutoroka wamesema kuwa
idadi ya wavamizi hao ni angalau watano na bado kuna wanafunzi na
maprofesa wengi wanashikiliwa mateka.
Taarifa za hivi punde zinaarifu kuwa magaidi hao wameanza kuwachinja baadhi ya mateka
waliowashikilia.
Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya ametuma salamu za rambi rambi kwa familia za wale waliouawa katika shambulizi hilo.
Kenyatta amewataka wakenya kuwa watulivu wakati huu ambapo maafisa wa usalama wanakabiliana na wapiganaji hao.
Wanajeshi wa jeshi la Kenya katika geti la chuo hicho |
Baadhi ya miili ya marehemu waliouawa katika shambulio la al-Shabaab katika chuo kikuu cha Garissa |
Helicopter ya jeshi ikitua na maiti na baadhi ya majeruhi katika kambi ya jeshi la Langata |
Wanafunzi wa shule ya sekondari ya Excel, iliopo karibu na chuo kikuu cha Garissa wakiondolewa kutoka shuleni kuhakikisha usalama wao |
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni