WATANZANIA TUUNGANE KUENDELEZA NA KUPATA HABARI KUTOKA KWA WANANCHI WETU WA KIGOMA PAMOJA TUTASHINDA BLOGER BY; RASHID HAMZA 0672965856 MAARUFU KAMA RASHID ZAGA AU DOGO 'R'
Jumamosi, 11 Aprili 2015
FILIKUNJOMBE AKABIDHI MSAADA WENYE THAMANI YA ZAIDI YA TSHMILIONI 32 HOSPITALI YA WILAYA YA LUDEWA
Mbunge wa Ludewa akizungumza na watumishi wa Hospitali ya wilaya ya Ludewa |
Watumishi wa Hospitali ya wilaya ya Ludewa wakimshangilia mbunge wao Deo Filikunjombe kwa msaada Hospitalini hapo |
Mbunge wa jimbo la Ludewa Deo Filikunjombe akionyesha mataulo ya kisasa |
Watumishi wa Ludewa Hospitali wakimsikiliza mbunge wao |
mbunge wa Ludewa Deo Filikunjombe kushoto akishiriki kushusha shehena na vifaa mbali mbali alivyovitoa katika Hospitali ya wilaya ya Ludewa |
Filikunjombe mwenye T-Shet ya CCM akisaidiana na watumishi wa Hospitali ya wilaya ya Ludewa kushusha vifaa mbali mbali |
Mbunge wa Ludewa Deo Filikunjombe mwenye T-Shet ya CCM kulia akisaidiana na watumishi wa Hospitali ya wilaya ya Ludewa kushusha vifaa mbali mbali |
Katibu mwenezi wa CCM mkoa wa Njombe Honoratus Mgaya wa tatu kushoto akisaidia kushusha mizigo |
Vitu vilivyotolewa na Filikunjombe |
Mbunge Filikunjombe akifurahi jambo wakati akizungumza na watumishi wa Hospitali ya Ludewa mara baada ya kukabidhi misaada mbali mbali |
Na FG Blog, Ludewa
KATIKA kukabiliana na tatizo la uhaba wa vifaa mbali mbali katika Hospitali ya wilaya ya Ludewa mkoani Njombe mbunge wa Jimbo la Ludewa (CCM) Deo Filikunjombeamekabidhi msaada wa Mashuka ya wagonjwa 200, Blanketi ya kisasa 100,taulo za kuogea wagonjwa 200 pamoja na mito 100 ya kulalia wagonjwa vyote vikiwa na thamani ya zaidi ya milioni 32 .
Mbunge huyo amefikia hatua hiyo kutokana na tatizo kubwa la Hospitali hiyo kukabiliwa na changamoto mbali mbali ikiwemo na vifaa hivyo kwa wagonjwa .
Akikabidhi msaada huo hospitalini hapo jana mara baada ya kuzungumza na watumishi wa sekta ya afya Mbunge huyo ,aliwataka watumishi hao kuwa waaminifu kwa kuviangalia vifaa hivyo visipotee na badala yake wavitunze na vitumike kwa ajili ya wagonjwa na si vinginevyo .
Alisema,anathamini na kutambua mchango mkubwa unaotolewa na watumishi hao katika kuwahudumia wagonjwa wanaolazwa katika hospitali hiyo lakini amewataka kuthamini wapiga kura wake hao kwa kuwapatia huduma inayostahiri na kuokoa maisha yao.
“Nawaomba sana ndugu zangu watumishi mjitahidi kutunza hivi vifaa nilivyoleta ilimnitie moyo niendelee kusaidia zaidi ,kwani hii ni fedha yangu binafsi niliyokaata kwenye posho yangu ya vikao vya bunge pia naomba muithamini sana kazi yenu ,kwani ajira ni ngumu na kuna watu wanahangaika huko mitaani kutafuta ajira pamoja na usomi wao hakuna ajira, tuwatumikie wagonjwa kwa upendo na furaha ikiwa ni pamoja na kuhokoa maisha yao kwani wanachohitaji toka kwenu ni upendo na huduma nzuri tu,alisema Filikunjombe.
Awali akisoma Risala fupi ya hospitali hiyo kwa Mbunge huyo Kaimu Mganga mkuu Hospitali ya Wilaya ya Ludewa Apolnary Nombo alisema,
Watumishi hao wanaheshimu jitihada kubwa ambazo amezifanyahususani kwenye sekta hiyo katika kipindi cha miaka mitano ainaonekana na zinapimika ndani na nje ya Bunge ikiwa ni pamoja na kuwatembelea mara kwa mara na kutoa misaada hospitalini hapo.
Hata hivyo alisema bado hospitali hiyo inakabiliwa na changamoto mbali mbali ambazo zinakwamisha maelengo yao ikiwemo ya kukosekana vifaa muhimu katika jengo la upasuaji ikiwemo mashine ya kuchemshia vifaa vya upasuaji na mashine za kutolea dawa za usingizi .
Pia changamoto nyingine ni uchakavu wa jengo la wazazi ambao unapingana na MDG 4 na 6 upunguzaji wa vifo vya wazazi pamoja na ukosefu wa chumba cha watoto wachanga ambao wakizaliwa njiti wanahitaji huduma hiyo pamoja na changamoto nyingine ambazo waliomba msaada wa mbunge huyo .
Mganga huyo alipongeza jitihahada mbali mbali ambazo zimekuwa wakifanywa na mbunge Filikunjombe katika Hospitali hiyo na Zahanati za vijiji mbali mbali katika wilaya ya Ludewa na kuwa pasipo kuboresha huduma za afya kwenye zahanati hizo yawezekana idadi ya wagonjwa kukimbilia katika Hospitali hiyo ya wilaya ingekuwa kubwa zaidi.
posted RASHID HAMZA
Jumatano, 8 Aprili 2015
DUWA YA KUMUOMBEA RAISI MZEE KARUME
HITMA YA MAREHEMU MZEE KARUME
Tuesday, April 7, 2015
IDADI YA WATU WALIOSOMA HABARI HII:
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein(katikati) akiwaongoza Viongozi mbali mbali pamoja na Wananchi katika Kisomo cha hitma ya aliyekuwa Rais wa Kwanza wa Zanzibar Marehemu Mzee Abeid Amani Karume katika ukumbi wa Ofisi Kuu ya CCM Kisiwandui Mjini Unguja Iliyofanyika leo asubuhi.[Picha na Ikulu.]
Baadhi ya Viongozo wakisoma hitma akiwemo aliyekuwa Rais wa Kwanza wa Zanzibar Marehemu Mzee Abeid Amani Karume(kushoto) Balozi Ali Karume katika ukumbi
wa Ofisi Kuu ya CCM Kisiwandui Mjini Unguja Iliyofanyika leo asubuhi.[Picha na Ikulu.]
Waislamu na wananchi mbali mbali wakiwa katika kisomo cha hitma ya aliyekuwa Rais wa Kwanza wa Zanzibar Marehemu Mzee Abeid Amani Karume katika ukumbi wa Ofisi Kuu ya CCM Kisiwandui Mjini Unguja Iliyofanyika leo asubuhi.[Picha na Ikulu.]
Mke wa Rais Zanzibar Mama Mwanamwema Shein(katikati) akiwa na Mama Shadya Karume Mke wa Rais Mstaafu wa Zanzibar(wa tatu kulia) Mama Fatma Karume (wa pili kulia) Mke wa Makamo wa Rais wa Jamhuri ya Muungano Mama Zakia Bilali (kushoto) Bi Khadija Aboud (wa pili kushoto)Mjumbe wa Kamati Kuu wa CCM,katika hitma ya kumuombea dua Rais wa kwanza wa Zanzibar Marehemu Mzee Abeid Amani Karume,iliyosomwa leo katika ukumbi wa Ofisi ya CCM Kisiwandui Mjini Unguja,[Picha na Ikulu.]
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein akiweka shada la mauwa katika kaburi la Marehemu Rais wa kwanza wa Zanzibar Mzee Abeid Amani Karume,baada ya kisomo cha hitma na dua iliyoombwa na wananchi wa Zanzibar katika Ofisi ya CCM Kisiwandui Mjini Zanzibar leo asubuhi,[Picha na Ikulu.]
Makamo wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilali
akiweka shada la mauwa katika kaburi la Marehemu Rais wa kwanza wa Zanzibar Mzee Abeid Amani Karume,baada ya kisomo cha hitma na dua iliyoombwa na wananchi wa Zanzibar katika Ofisi ya CCM Kisiwandui Mjini Zanzibar leo asubuhi,[Picha na Ikulu.]
Muasisi wa Mapinduzi ya Zanzibar Mzee Hamid Ameir akiweka shada la mauwa katika kaburi la Marehemu Rais wa kwanza wa Zanzibar Mzee Abeid Amani Karume,baada ya kisomo cha hitma na dua iliyoombwa na wananchi wa Zanzibar katika Ofisi ya CCM Kisiwandui Mjini Zanzibar leo asubuhi,[Picha na Ikulu.]
Balozi Ali Karume (Mtototo) kwa niaba ya familia akiweka shada la mauwa katika kaburi la Marehemu Rais wa kwanza wa Zanzibar Mzee Abeid Amani Karume,baada ya kisomo cha hitma na dua iliyoombwa na wananchi wa Zanzibar katika Ofisi ya CCM Kisiwandui Mjini Zanzibar leo asubuhi,[Picha na Ikulu.]
Wake wa Viongozi wakiitikia dua iliyoombwa katika kaburi la Marehemu MzeeAbeid Amani Karume baada ya hitma iliyosomwa leo katika ukumbi wa Ofisi ya CCM Kisiwandui Mjini Unguja na kuhudhuriwa na waislamu mbali mbali Mjni na Vijijini,[Picha na Ikulu.]
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein pamoja na Viongizi wengine wakiitikia Dua iliyoombwa na Mufti Mkuu wa zanzibar Sheikh Saleh Omar Kabi (kulia) baada ya kisomo cha hitma iliyosomwa leo katika ukumbi wa Ofisi ya CCM Kisiwandui Mjini Unguja.[Picha na Ikulu.]
Baba Askofu wa Anglikan wa Kanisa la Mkunazini Michael Hafidh akiomba dua wakati Viongozi mbali mbali waliofika katika kaburi la aliyekua Rais wa Kwanza wa Zanzibar Marehemu Mzee Abeid Amani Karume,baada ya kisomo cha hitma iliyosomwa leo katika ukumbi wa Ofisi ya CCM Kisiwandui Mjini Unguja.[Picha na Ikulu.]
POSTED RASHID HAMZA
Jisajili kwenye:
Machapisho (Atom)