28 Machi 2015 Imebadilishwa mwisho saa 10:27 GMT
Mtandao
wa facebook umethibitisha kwamba unafungua huduma yake ya messenger kwa
wajenzi .Habari hizo zilitangazwa na Mark Zuckerberg katika kongamano
la nane la wajenzi lililofanyika mjini San Fransisco.Zaidi ya programmu
40 mpya zikiwemo habari za hali ya anga tayari zimeandaliwa kwa huduma
hiyo.Mtandao huo wa kijamii pia ulionyesha programu yake ya video
inayomruhusu mtumiaji kusukuma kamera huku kanda hiyo ikicheza.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni