Jumatano, 1 Aprili 2015

KUMEKUCHA KIGOMA

HAMA CHA WAANDISHI WA HABARI KIGOMA WAZINDUA GAZETI LAO LA KIGOMA YETU


 Na Editha Karlo wa 

Globu ya Jamii, Kigoma 

KWA niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Kanali mstaafu Issa Machibya ,Mkuu wa Wilaya ya Kigoma mjini Exavery Maketa jana alizindua gazeti la Kigoma yetu linaalomilikiwa na CHAMA cha waandishi wa habari wa Mkoa wa Kigoma (KGPC). 

Uzinduzi huo ulifanyika katika ukumbi wa Kibo Peak uliopo mjini hapa na kuhudhuriwa na mamia ya wadau mbalimbali wa sekta ya habari pamoja na wakazi wa Mkoa wote wa Kigoma 

Akiongea katika uzinduzi huo katika hotuba yake Mkuu a Wilaya aliwataka waandishi kupitia gazeti hilo kuepukana na vitendo vya rushwa na badala yake gazeti hilo litumike katika kuchochea kuleta maendeleo katika Mkoa wa Kigoma. 

 Mkuu huyo wa Wilaya aliongeza kwa kusema pia wanahabari lazima waandike habari za ukweli na uwazi na ambazo hazifungamani upande wowote kwani wao ni chombo kinachoweza kuchochea maendeleo ya wananchi endapo wataandika habari zilizofanyiwa uchunguzi wa kutosha. 

 Aidha aliwaomba waandishi kuandika habari zinazo chochea maendeleo kwa wananchi ili wananchi waweze kuhamasika kujishugurisha kuchochea maendeleo katika maendeleo ya mkoa wa kigoma. 

 “Ndugu zangu Waandishi wa habari wa Kigoma kupitia gazeti lenu la Kigoma YETU mhakikishe mnaandika habari zenye kuleta tija katika mkoa wetu zitakazo chochea maendeleo iliwananchi wa Mkoa wa kigoma waweze kufurahia uwepo la gazeti lenu yetu”, alisema Maketa. 

Mwenyekiti wa chama cha waandishi Wa Habari Mkoani Kigoma(KGPC) ,Deogratuas Nsokoro alisema wao kama chama wamejipanga kuhakikisha kuinua uchumi wa Mkoa wa kigoma na kuleta maendeleo kwa kuandika habari zitakazo chochea maendeleo kwa haraka. 

 Alisema waandishi wote wanauelewa wa kuandika habari zilizofanyiwa utafiti wa kina hivyo anaamini wataandika habari zenye kuleta maendeleo katika wa mkoa wa kigoma. 

 Alisema gazeti hilo lilipata ruzuku ya ufadhili wa Tanzania Media Fund(TMF)shilingi milioni 50 kwa kipindi cha miezi sita tokea october mwaka jana hadi march mwaka huu ambapo ufadhili huo unameisha. 

 ”Pamoja kuwa muda wa ufadhili umeisha lakini sisi leo tumezindua rasmi gazeti letu hili la toleo la april na nina wahakikishia wadau wetu gazeti hili halitapotea mtaani litaendelea kuwepo,kwasasa linatoka mara moja kwa mwezi lakini hivi karibuni litaanza kutoka mara mbili kwa mwezi”Alisema Nsokolo

 Mkuu wa Wilaya ya Kigoma Mjini Exavery Maketa akisoma hotuba yake kwa wageni waalikwa (Hawapo pichani)kwa niaba ya mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Kanali Mstaafu Issa Machibya 

 Mwenyekiti wa chama cha waandishi wa habari wa Mkoa wa Kigoma(KGPC) Deogratius Nsokolo akitoa neno la shukrani kwa wageni waalikwa walihudhuria uzinduzi wa gazeti la Kigoma YETU.

 Baadhi ya viongozi wa serekali na dini waliohudhulia katika uzinduzi wa gazeti la Kigoma YETU

  Waandishi wa gazeti la Kigoma YETU wakifuatilia matukio mbalimbali ya uzinduzi wa gazeti hilo

 Waandishi wa chama cha habari mkoa wa Kigoma wakiwa katika picha ya pamoja na mgeni Rasmi Mkuu wa Wilaya ya Kigoma mjini Exavery Maketa baada ya uzinduzi wa gazeti la Kigoma YETU

Wandishi wa Gazeti la kigoma yetu wakifurahia baada ya uzinduzi kutoka kushoto ni Mwajabu Kigaza wakatikati ni Rhoda Ezekiel pamoja na Editha Karlo

 

POSTED BY;HASSAIN MTUNDA

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni