Nape Amtaka Zitto Ajenge Upinzani wa Kweli.....Asema Akitaka Heshima Aachane na Siasa za CHADEMA Zenye Mlengo wa Kuruga Amani
Siku
chache baada ya aliyekuwa Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe,
kutangaza kujiunga na chama cha ACT-Tanzania, Katibu wa Itikadi na
Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Nape Nnauye, amemtaka kujenga
upinzani wa kweli kwa ajili ya kujenga nchi na si kubomoa.
Akizungumza
katika mkutano wa hadhara wa kuhitimisha ziara ya Katibu Mkuu wa CCM,
Abdulrahman Kinana, katika mikoa ya Dodoma, Arusha na Kilimanjaro, Nape
alisema anamkaribisha mwanasiasa huyo upya katika ulingo wa siasa.
Alisema
kinachotakiwa ni upinzani wenye lengo la kujenga na Zitto akitaka
heshima aachane na siasa za Chadema zenye lengo la kuvuruga.
Hata
hivyo, alisema hawawezi kuwa na mfumo wa vyama vingi vyenye lengo la
kubomoa, hivyo ajenge upinzani wa kweli wa kuijenga nchi.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni