Waziri wa Nishati na Madini Mh.George Simbachawene Awasimamisha Kazi Wahandisi Watatu TANESCO.
Waziri wa nishati na madini Mh.George Simbachawene ameagiza kusimamishwa kazi mara moja kwa wahandisi watatu wa shirika la umeme nchini TANESCO kutoka maeneo matatu jijini Dar es salaam baada ya wahandisi hao kushindwa kuwajibika ipasavyo ikiwa ni pamoja na kutochukua hatua wanapopewa taarifa za kero za wananchi kwenye maeneo wanayosimamia
Wahandisi
hao ni wa Temeke, Tazara na Tabata Magengeni, jijini Dar es Salaam,
wanaodaiwa kusababishia Shirika hilo malalamiko kutoka kwa wananchi kila
wakati.
Akizungumza
na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Simbachewene alisema
baadhi ya malalamiko yanayotolewa na wateja ni taarifa wanazotoa kuhusu
nyaya za umeme na nguzo kuanguka bila kuchukuliwa hatua zozote.
Simbachewene alisema wajibu wa watendaji hao ni kushughulikia kero kama hizo sio wananchi waende kulalamika.
"Kila
kukicha wanalalamikiwa Tanesco jana nilipiga simu Tazara na Tabata
kuwajulisha kuna tatizo lakini hawajaenda, unakuta nyaya ya umeme
imeanguka ina maana inasubiria fedha ya kigeni ndio itolewe hivi kazi
yenu nini? Nguzo imeanguka mnajulishwa mwezi unapita hilo gari la
emergency linafanya kazi gani," alihoji.
"Huyo
mhandisi wa Tabata inawezekana hata hajui kitu, matatizo ni mengi na
sidhani kama anafika na kuyafuatilia, hivyo naagiza chukueni hatua za
kinidhamu ili iwe fundisho na kwa wengine," alisema.
Akizungumzia
kero za kukatika umeme mara kwa mara alisema, umeme unakatika pasipo na
sababu maalum. Waya umeanguka Temeke hadi watu wanakufa hakuna hatua
zilizochukuliwa.
“Wananchi wamepiga simu hakuna hatua zilizochukuliwa mpaka watu wanakufa hatuwezi kuyanyamazia haya," alisema na kuongeza:
“Sisi ni watumishi wa watanzania kwa leo naaza na hawa watatu wanatosha, wengine nitaendelea nao.”
“Sisi ni watumishi wa watanzania kwa leo naaza na hawa watatu wanatosha, wengine nitaendelea nao.”
Aidha,
amepiga marufuku uegeshwaji wa magari ya Tanesco katika maeneo ya
starehe kama baa, jambo ambalo alisema linalalamikiwa na wananchi.
Aliagiza
vibarua wote walikokuwa wakitumiwa kwenye gari la dharura la Tanesco,
kuajiriwa ili wasiwe wanachukua rushwa kwa wateja.
Alisema vibarua hao wamefanyakazi kwa muda mrefu bila kupewaajira na kila wakati ajira za Tanesco zinatangazwa.
Kuhusu
tatizo la Luku, alisema hali imerudi kama kawaida na kuwataka kuendelea
kununua huduma hiyo kupitia mitandao yote ya simu nchini.
Alisema
chazo cha tatizo ni moja ya kampuni ya uwakala wa kuuza Luku
kusimamishwa kutokana na kutokidhi viwango matakwa na taratibu za
Mamlaka za Mapato (TRA),
Alifafanua
kuwa kusimamishwa kwa kampuni hiyo kulilazimu mauzo yote yaliyokuwa
yanapitia kampuni hiyo yapitie kwenye kampuni nyingine.
Alisema
ili kukabiliana na hali hiyo, kampuni za simu zinazotoa huduma hiyo
zililazimika kujiunga na mitandao mingine inayotoa huduma hiyo.
Alisema kwa sasa tatizo hilo limeshughulikiwa na huduma hiyo imeanza kutolewa kama kawaida.
Aidha, alisema mpango wa kujiunga na kampuni nyingi zaidi zinazotoa huduma hiyo unafanyika ili kuondoa ukiritimba.
Akizungumzia
azma ya kampuni ya Selcom ya kuishitaki Tanesco kwa kuvunja mkataba,
alisema suala hilo haliwahusu kwani lipo upande wa TRA pamoja na Selcom.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni