Jumatano, 1 Aprili 2015

IGP Mangu Afanya Mabadiliko Kwa Baadhi ya Makamanda wa Polisi wa Mikoa.


Inspekta Jenerali wa Polisi IGP Ernest Mangu amefanya mabadiliko kwa baadhi ya makamanda wa polisi wa mikoa.

Miongoni mwa makamanda wa mikoa waliofanyiwa mabadiliko ni pamoja na aliyekuwa kamanda wa Mkoa wa Simiyu, Naibu Kamishna wa Polisi (DCP) Charles Mkumbo anakwenda kuwa kamanda wa Polisi mkoa wa Mwanza na nafasi yake kuchukuliwa na aliyekuwa afisa mnadhimu mkoa wa Manyara Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Gemini Mushi.
 
Aliyekuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza Naibu Kamishna wa Polisi (DCP) Valentino Mlowola anakwenda kuwa Kaimu Kamishna wa Intelijensia makao makuu. 
 
Aliyekuwa kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala Naibu Kamishna wa Polisi (DCP) Maria Nzuki amehamishwa makao makuu kuwa mkuu wa polisi jamii na nafasi yake kuchukuliwa na aliyekuwa kamanda wa kikosi cha ufundi Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Lucas Mkondya.

Wengine ni aliyekuwa Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Godfrey Kamwela amehamishiwa Polisi Makao Makuu na nafasi yake kuchukuliwa na aliyekuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Njombe Kamishna Msaidi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Fulgence Ngonjani.
 
Aliyekuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Ulrich Matei amehamishiwa Kanda Maalum ya Dar es Salaam kuwa mkuu wa utawala na nafasi yake kuchukuliwa na aliyekuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kigoma Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Jafary Mohamed.
 
Aidha, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Ferdinand Mtui aliyekuwa mkuu wa operesheni maalum polisi makao makuu ameenda kuwa Kamanda wa Polisi mkoa wa Kigoma.

Zaidi ya hao wengine waliyohamishwa ni pamoja na aliyekuwa Kamanda wa Polisi mkoa wa Tanga Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Frasser Kashai amehamishiwa Polisi makao makuu na nafasi yake kuchukuliwa na aliyekuwa mkuu wa upelelezi mkoa wa Iringa Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Zuberi Mwombeji.
 
Aliyekuwa Kamanda wa Polisi mkoa wa Temeke Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Kihenya Kihenya amehamishiwa polisi makao makuu na nafasi yake kuchukuliwa na aliyekuwa mkuu wa polisi wa wilaya ya kati Ilala, Dar es Salaam Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Andrew Satta.

Kwa mujibu wa kanuni, taratibu na miongozo ya Jeshi la Polisi, mabadiliko hayo ni ya kawaida katika kuhakikisha kwamba usalama wa raia na mali zao unaendelea kuimarika.

Imetolewa na:
Advera Bulimba-SSP
Msemaji wa Jeshi la Polisi.
 POSTED BY ; R D PRODUCTION

THANKS MPEKUZI BLOG

MAGAZETI YETU LEO

POSTED BY; R D PRODUCTION

Wednesday, April 1, 2015

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumatano ya Tarehe 1 March 2015

Mpekuzi blog






















THANKS MPEKUZI BLOGY

WAPINZANI WAANZA

Breaking News: Vurugu Zaibuka Bungeni.......Wapinzani Wamtuhumu Spika Kuilinda Serikali, Bunge Laahirishwa hadi Mchana. Video Ya Tukio Hilo Iko Hapa.


Kikao cha  Bunge kimevunjika muda mfupi uliopita baada ya kutokea vurugu za maneno kufuatia wapinzani kutaka Waziri Mkuu atoe taarifa juu ya mwenendo wa kura ya maoni ya katiba mpya april 30,2015.

Kutokana na vurugu hizo za dakika kama 10 hivi Spika Anna Makinda amesitisha gafla shughuli za bunge hadi mchana.

Hali likuwa hivi:

Mnyika: Nimesimama kupata idhini kwa mujibu wa kanuni ili shughuli za bunge zisitishwe badala yake tujadili zoezi la uandikishaji nchi nzima.

Mpaka sasa zoezi halijakamilika hata kwa mkoa mmoja tu wa Njombe, jambo hili ni la dharura na lilishatolewa na ukaagiza kamati ishughulikie.Tunaomba majibu tupate kikao hiki na leo tunafunga mkutano.

Spika Makinda: Hoja hii inafanana na ile ya kwanza(  Hoja  ya  mbunge wa Kisarawe Seleman Jafo ambaye  alipendekeza kura ya maoni ya katiba  inayopendekezwa isogezwe mbele  na  badala  yake  kuwe  na  katiba  ya  mpito  kuelekea  uchaguzi  mkuu)

Baada  ya  kauli  hiyo, Mnyika  na  wabunge  wa  upinzani  walianza  kupiga  kelele  bungeni  wakidai  kuonewa  huku  wakimtuhumu  Spika  makinda  kuibeba  serikali.

Hata hivyo, Spika  hakuonesha  kutishwa  na  kelele  hizo  na  badala  yake  alimtaka  katibu  wa  Bunge  atoe  mwongozo  wa  kile  kinachofuata.

Katibu  alisimama  na  kuanza  kusoma  miswada  ya  habari ambapo  wapinzani  nao  walisimama  na  kuzidisha  kelele  huku  wakisema: "Tunataka majibu..Tunataka majibu. Tumechoka kuburuzwa..Makinda kwanini unailinda Serikali.??!!!

Hali  hiyo  ikamlazima  Spika  Makinda  Kuliahirisha  Bunge  hadi  mchana.

Tazama  Video  hapo  chini.



POSTEDY BY; RASHID  HAMZA

CHAMA MAKINI NA WATETEZI WETU

NAPE AZUNGUMZI CHANGAMOTO BAADA YA KUMALIZA ZIARA

KATIBU WA UENEZIKatibu wa Nec Itikadi na Uenezi Npe Nnauye,wa Chama Cha Mapinduzi(CCM)

 

Ziara ya Chama Cha Mapinduzi katika mikoa ya Dodoma,Arusha na Kilimanjaro imemalizika jana mkoani kilimanjaro,ziara hiyo yenye lengo la kukangua miradi ya maendeleo na utekelezaji wa ilani ya Chama.


Nape anazungumzia changamoto walizo ziona katika mikoa hiyo alipozungumza na katika mahojiano maalum na Uhuru FM katika kipindi cha Helllo Tanzania.

 
 

POSTED  BY; RASHID  HAMZA

BLOGGER WETU MAKINI NA MPIGANAJI

KIGOMA YETU

Leo tumeona kukuletea na kuwaomba mafansi wa blog yetu ya SHIRIKISHO LA ELIMU YA JUU MKOA WA KIGOMA

HUYU NI KIJANA ANAYEFANYA KLAZI KATIKA BLOG YETU YA SHIRIKISHO NA NIMKELEKETWA NA MPIGANIA HAKI ZA WATANZANIA ANAITWA RASHID HAMZA HUYU NDIYE MWANDISHI WETU MKUU WA BLOG YETU,TUMEAMUA KUFANYA HIVI KUTOKANA NA BLOG YETU KUWA CHANGA HIVYO TUNAOMBA KWA YEYOTE ATAKAYE TAKA KUTANGAZA MATANGAZO YAKE YOYOTE YALE AMTAFUTE KIJANA HUYO HAPO JUU AMBAYE PIA NI MWANAFUNZI WA CHUO KWA NAMBA ZIFUATAZO;- 0672965856 AU 0757337969  NA KWA HABARI YOYOTE ILE

OMBI LETU NI KUWA 

TUNAOMBA WATANZANIA WOTE KWA UMOJA NA USHIRIKIANO TUPATE HABARI MBALIMBALI ZA KIGOMA NA SEHEMU MBALIMBALI ZA NCHI YETU






POSTED BY; HASSAN MTUNDA (SUB BLOGGER) $ ANNASTAZIA RH



ILOVE KIGOMA                        ILOVE             TANZANIA







Jumanne, 31 Machi 2015

CHAMA CHA MAPINDUZI CCM KINAKUBALIKA

KINANA AWASHIKA PABAYA WAPINZANI

Sasa imefikia wakati wa kusema CCM Hakuna chama kinachoweza kukukabiliana nacho baada ya pulugushani za vyama mbalimbali vya upinzani sasa zimeanza kutoa majibu hatimaye kiongozi wa chama kikubwa cha upinzani chadema amejivua rasmi uanachama kwenye mkutano wa hadhara ambao Uliitishwa na katibu mkuu wea chama cha mapinduzi muheshimiwa ABDULLAHMAN KINANA,Pia kiongozi huyo alikuwa katibu wa mbunge muheshimiwa msigwa,Pia muheshimiwa kinana ameendelea na kukagua na kufanya kazii za kukijenga chama cha mapinduzi na kukitangaza ili iliifikapo katika uchaguzi wa mwaka huu 2015 kila mtu akipigie chama cha mapinduzi kwa jinsi chama hicho kilivyo fanya kazi nzuri na za kupigiwa mifano.

huyo alikuwa kiongozi wa chama cha chadema ,alizungumza na wananchi wakati akitangaza rasmi kujivua uanachama wa chama hicho.Mpaka sasa muheshgimiwa KINANA ameweza kuwachukuwa wanachama wa vyama mbalimbali kutoka vyama vya upinzani.

HAPO MUHESHIMIWA KATIBU MKUU WA CHAMA AKIHUTUBIA WANACHAMA NA WAPENZI WA CHAMA HICHO



ENDELEA KUFUATILIA HABARI KUTOKA SHIRIKISHO LA ELIMU YA JUU MKOA WA KIGOMA


PAMOJA TUNASHINDA 



POSTED BY; RASHID HAMZA (R-D)

Jumatatu, 30 Machi 2015

URAISI TANZANIA NI KICHEKO

CCM YAANG'ARA

KIONGOZI WA CHAMA CHA MAPINDUZI  BWANA MWIGULU NCHEMBA LEO IMEBAINIKA KUWA NDIYE KIONGOZI ANAYEKUBALIKA KIASI KIKUBWA KUSHINDA WAGOMBEA WOTE VIJANA WA VYAMA VYOTE NCHINI HIYO IMETOKANA NA UCHUNGUZI  ULIOFANYWA NA MOJA WA MITNDAO NCHINI KUWA KIJANA HUYO ANAKUBALIKA KUSHINDA WAGOMBEA WOTE WALIOTAJWA KUGOMBEA VYAMA MBALIMBALI AMBAO NI PAMOJA NA ZITTO ZUBERI KABWE,NGEREJA,JANUARI MAKAMBA,FREEMAN MBOWE,HAMISI KIGWANGALA NA WENGINE WENGI KUWA KINARA WA VIJANA ANAKUBALIKA NI HUYU

 

POSTED BY;RASHID HAMZA