Breaking News: Vurugu Zaibuka Bungeni.......Wapinzani Wamtuhumu Spika Kuilinda Serikali, Bunge Laahirishwa hadi Mchana. Video Ya Tukio Hilo Iko Hapa.
Kikao cha Bunge kimevunjika muda mfupi uliopita baada ya kutokea vurugu za maneno kufuatia wapinzani kutaka Waziri Mkuu atoe taarifa juu ya mwenendo wa kura ya maoni ya katiba mpya april 30,2015.
Kutokana na vurugu hizo za dakika kama 10 hivi Spika Anna Makinda amesitisha gafla shughuli za bunge hadi mchana.
Hali likuwa hivi:
Mnyika:
Nimesimama kupata idhini kwa mujibu wa kanuni ili shughuli za bunge
zisitishwe badala yake tujadili zoezi la uandikishaji nchi nzima.
Mpaka
sasa zoezi halijakamilika hata kwa mkoa mmoja tu wa Njombe, jambo hili
ni la dharura na lilishatolewa na ukaagiza kamati ishughulikie.Tunaomba
majibu tupate kikao hiki na leo tunafunga mkutano.
Spika Makinda:
Hoja hii inafanana na ile ya kwanza( Hoja ya mbunge wa Kisarawe
Seleman Jafo ambaye alipendekeza kura ya maoni ya katiba
inayopendekezwa isogezwe mbele na badala yake kuwe na katiba ya
mpito kuelekea uchaguzi mkuu)
Baada
ya kauli hiyo, Mnyika na wabunge wa upinzani walianza kupiga
kelele bungeni wakidai kuonewa huku wakimtuhumu Spika makinda
kuibeba serikali.
Hata
hivyo, Spika hakuonesha kutishwa na kelele hizo na badala yake
alimtaka katibu wa Bunge atoe mwongozo wa kile kinachofuata.
Katibu
alisimama na kuanza kusoma miswada ya habari ambapo wapinzani
nao walisimama na kuzidisha kelele huku wakisema: "Tunataka majibu..Tunataka majibu. Tumechoka kuburuzwa..Makinda kwanini unailinda Serikali.??!!!
Tazama Video hapo chini.
POSTEDY BY; RASHID HAMZA
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni