Ijumaa, 17 Aprili 2015

KIGOMA KUMEKUCHA

VIONGOZI WA SHIRIKISHO MKOA KIGOMA WAKIWA KWENYE VIKAO MBALIMBALI

 KATIBU WA SHIRIKISHO MKOA WA KIGOMA BWA HASSAN BUSORO AKIZUNGUMZA JAMBO
 MUHESHIMIWA KATIBU AKIENDELEA KUSOMA TAARIFA
 KATIBU AKIENDELEA KUSOMA TAARIFA HIYO


 MEZA KUU WAKIMSIKILIZA KATIBU KWA MAKINI SANA


 HAWA NI BAADHI YA WANACHUO WALIOHUDHURIA MKUTANO HUO

 WAJUMBE AKIENDELEA KUMSIKILIZA

 WANACHUO WAKISIKILIZA KWA MAKINI


 WANACHUO WAKIWA MAKINI MNO KUMSIKILIZA KATIBU SHIRIKISHO MKOA WA KIGOMA

 WAKISIKILIZA KWA MAKINI

 HAPA BAADHI YA WANACHUO WAKIANDIKA DONDOO



 HAPA BAADHI YA WANACHUO WAKIMSIKILIZA



 HAPA BAADHI YA WANACHUO WAKIMSIKILIZA
 HAPA BAADHI YA WANACHUO WAKIMSIKILIZA


  HAPA BAADHI YA WANACHUO WAKIMSIKILIZA
  HAPA BAADHI YA WANACHUO WAKIMSIKILIZA
  HAPA BAADHI YA WAGENI RASMI WAKIMSIKILIZA


 MUHESHIMIWA KATIBU WA MKOA AKIENDELEA KUHUTUBIA

 HAPA AKIKABIDHI TAARIFA KWA MGENI RASMI KATIBU WA MKOA WA CCM  KIGOMA
 HAPO AKISALIMIANA VIONGOZI WA MEZA KUU


 KATIBU WA CCM KIGOMA MJINI AKIHUTUBIA


 KATIBU WA UWT MKOA NA KATIBU WA VIJANA KIGOMA MJINI WAKISIKILIZA
 MGENI RASMI NA MNEC MHESHIMIWA MAYONGA KAHENA WAKISIKILIZA
 KATIBU WA SHIRIKISHO  UCHUMI NA FEDHA MKOA  BI; HADIJA  RUGETE AKISIKILIZA KWA MAKINI
VIONGOZI WA MATAWI (CHUO)

 M/KITI WA TAWI CHUO CHA KIHINGA F.DC  BWANA HUSSEIN H.  BUSORO

 HAPA VIONGOZI NA WANACHUO WAKIWA WANAIMBA MWIMBO KWA FURAHA NA RAHA TELE
 MGENI RASMI KATIBU WA CCM MKOA WA KIGOMA AZUNGUMZA JAMBO (AKIHUTUBIA)
 MUHESHIMIWA KATIBU WA CCM MKOA AKIENDELEA KUTOA UJUMBE KWA WANACHUO
 KATIBU WA UHAMASISHAJI SHIRIKISHO BWANA RUWAZA SHABANI AKIIMBA WIMBO KWA FURAHA






  KATIBU WA UVCCM KIGOMA MJINI NA VIJIJINI PAMOJA NA KATIBU WA MKOA UWT



 WANACHUO WAKIENDELEA KUSIKILIZA



 


POSTED TODAY BY;RASHID HAMZA

Waziri Sitta Awatimua Vigogo wa Kampuni ya Reli nchini (TRL)..... Madeni Kipande Wa TPA Kafukuzwa Kazi Rasmi


SERIKALI imewasimamisha kazi karibu viongozi wote wakuu wa Kampuni ya Reli nchini (TRL), kwa kile kilichoelezwa kuwa hujuma ya mabilioni ya shilingi yaliyotumika kununua mabehewa chakavu.


Waliosimamishwa ni pamoja na Mkurugenzi Mtendaji, Kipallo Kisamfu, Mhandisi Mkuu wa Mitambo, Ngosomwile Ngosomiles, Mhasibu Mkuu, Mbaraka Mchopa, Mkaguzi Mkuu wa Ndani, Jasper Kisiraga na Meneja Mkuu wa Manunuzi wa kampuni hiyo, Ferdinand Soka.

 

Wakati hayo yakiwakuta hao, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari (TPA), Madeni Kipande aliyekuwa amesimamishwa kazi kutokana na tuhuma mbalimbali, sasa amefukuzwa rasmi.

 

Hayo yaliwekwa hadharani jana na Waziri wa Uchukuzi, Samuel Sitta alipokutana na waandishi wa habari na kutoa taarifa ya uchunguzi kuhusu ununuzi wa mabehewa machavu katika Kampuni ya Reli nchini.

 

Sitta, mmoja wa wanasiasa wakongwe aliyeshika nyadhifa mbalimbali serikalini ikiwa ni pamoja na uwaziri tangu enzi za utawala wa Awamu ya Kwanza chini ya Mwalimu Julius K. Nyerere, alisema mbali ya madudu yaliyoonekana katika kamati iliyoundwa na mtangulizi wake katika wizara hiyo, Dk Harrison Mwakyembe, waligundua mambo mengi Jumatatu wiki hii.

 

Yaliyogunduliwa ni pamoja na ukiukwaji mkubwa wa masharti ya mkataba wa ununuzi wa mabehewa hayo, kwani mzabuni alilipwa fedha zote, tofauti na taarifa za awali iliyoonesha malipo yangefanyika kwa awamu.

 

“Hivyo wizara ina maoni kwamba mazingira ya utekelezaji wa mkataba huu yana dalili za hujuma kwa TRL na kwa nchi yetu na siyo uzembe,” alisema Sitta. 

 

Akifafanua hilo alisema TRL iliagiza mabehewa ya mizigo 274 ambapo zabuni ilikwenda kwa Kampuni ya Hindustan & Industrial Engineering Limited ya India, ambapo katika uagizwaji wa mabehewa hayo kulikuwa na uzembe katika ufuatiliaji kiwandani, pamoja na uzembe katika kuyapokea yakiwa mabovu.

 

Alisema mabehewa hayo yalipofikia 150 aliyazuiwa, hivyo 124 yakawa bado hayajafika nchini. Sitta alisema kwa mujibu wa taarifa alizonazo ilibidi mpaka sasa asilimia 50 ya gharama ya mabehewa hayo iwe imeshalipwa, lakini kinyume chake nyaraka zinaonyesha mpaka sasa pamoja na kuzuiwa kwa mabehewa 124 mzabuni huyo ameshalipwa asilimia 100.

 

“Huu ni uzembe, ni hujuma kama kiongozi sitamstahi yeyote atakayekuwa sehemu ya hujuma,” alisema Sitta.

 

Alisema kutokana na hali hiyo ameagiza kwamba uchunguzi wa kubaini uwezekano wa hujuma ufanyike, hivyo amemwelekeza Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Dk Shaaban Mwinjaka asimamie kuundwa kwa kamati ya uchunguzi.

 

Alisema kamati hiyo itaongozwa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kwa kushirikiana na Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (TAKUKURU), Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi katika Sekta ya Umma (PPRA), na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

 

Sitta ametoa wiki tatu kuanzia Jumatatu ijayo Aprili 20, mwaka huu kuchunguza na kukamilisha kazi. Katika kipindi hicho, viongozi wakuu wa kampuni hiyo ya reli wanaowajibika na mkondo wa kashfa hiyo ya uagizaji na malipo ya ununuzi wa mabehewa hayo wote wamesimamishwa kupisha uchunguzi huo.

 

Aidha, alisema tangu mwanzoni mwa mwaka huu serikali ilikuwa ikifanyia kazi tuhuma zinazohusu mabehewa mabovu ya mizigo yaliyoagizwa kutoka India na TRL, baada ya kukamilika kwa uchunguzi wa tuhuma hizo na kamati iliyoundwa na Mwakyembe, aliagiza bodi ya wakurugenzi ya TRL ipitie taarifa hiyo na maelezo ya suala zima la mabehewa hayo.

 

Alisema katika uchunguzi huo ilibainika kuwa mabehewa mengi kati ya yaliyoagizwa yana kasoro, pia kulikuwa na uzembe katika uagizaji na ufuatiliaji kiwandani yalipokuwa yanatengenezwa na kulikuwa na uzembe katika kuendelea kuyapokea mabehewa hayo pamoja na ubovu wake kujulikana.

 

Alisema amemteua Elias Mshana kukaimu nafasi ya Mkurugenzi Mtendaji hadi hapo uchunguzi utakapokamilika. Pia ameagiza bodi ya wakurugenzi ya TRL ikutane kuteua watumishi wenye sifa kukaimu nafasi wanaozishikilia waliosimamishwa kazi.

 

Kipande wa TPA  Akizungumza suala la Kipande, Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Bandari aliyekuwa amesimamishwa kazi tangu Februari 16, mwaka huu ili kupisha uchunguzi wa tuhuma mbalimbali dhidi yake, Sitta alisema Tume aliyoichagua ilikamilisha kazi yake Machi 20, na kumkabidhi taarifa ya uchunguzi wao Machi 24 kwa hatua zaidi.

 

“Baada ya kuisoma taarifa ya tume na hatimaye kushauriana na taasisi mbalimbali zinazohusika na masuala haya, tumeridhika pasipo mashaka yoyote kwamba isingefaa Madeni Kipande kuendelea na kazi ya kuongoza Mamlaka ya Bandari.

 

“Hii ni kutokana na kuridhika na utawala mbovu aliouendesha uliosababisha manung’uniko mengi miongoni mwa wateja na wadau wa bandari na mgawanyiko mkubwa wa wafanyakazi,” alisema Sitta. 

 

Alisema kutokana na hali hiyo, serikali imeamua kumrejesha Kipande Idara Kuu ya Utumishi ili aweze kupangiwa majukumu mengine.

 

“Kipande ameonekana hafai kuongoza bandari ana maamuzi ya pupa, yasiyofuata taratibu pia yenye karaha. Tulichunguza uwezo wake wa kuendesha mamlaka ya bandari sasa kishapwaya inabidi arudishwe utumishi.

 

Hapa hatujachunguza masuala ya jinai, bali uwezo wa kutenda kazi,” alisema Sitta.
 
Tangu kusimamishwa kwa Kipande ambaye alikuwa anakaimu nafasi ya Mkurugenzi Mkuu, Ephraim Mgawe aliyekuwa ameondolewa kutokana na tuhuma mbalimbali, nafasi hiyo sasa inashikiliwa na Awadhi Massawe aliyepata baraka za Waziri Sitta na kuendelea kuwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu TPA.

 

POSTED BY; RASHID HAMZA

MAGARI YETU YATATUPONESHA KWELI

Ajali ya Daladala yaua watu 19 Leo jijini Mbeya



Ajali ya Daladala imeua watu 19 eneo maarufu kama Uwanja wa ndege, Kiwila, Mkoani Mbeya baada ya daladala hiyo kutumbukia kwenye Mto.
 
Habari  toka  eneo la tukio zinaarifu kuwa watu wawili tu ndio wamepona akiwemo kondakta. 
 
Ajali hii imetokea baada  ya Coaster zinazofanya safari zake kati ya Mbeya na Kyela kugoma hivyo baadhi ya daladala za mjini kuamua kubeba abiria.












Alhamisi, 16 Aprili 2015

MVUA NA RADI HIZI ZITATUPONESHA

MKUU WA MKOA WA KIGOMA AONGOZA WANANCHI KUAGA MIILI YA MWALIMU NA WANAFUNZI WALIOPIGWA NA RADI.


]

 

POSTED BY: BORA MBANGAHA TOGETHER WE CANE 

SEREKALI SIKIVU INAYO ANGALIA ELIMU BORA WATAMKA

Wasiojua kusoma,kuandika kutoenda darasa la tatu.

Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Elimu), Kassim Majaliwa
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Elimu), Kassim Majaliwa
KATIKA kuhakikisha inaondoa kabisa tatizo la watu wasiojua kusoma na kuandika nchini, Serikali imefanya mabadiliko ambapo kuanzia sasa mtoto wa darasa la pili hawezi kuruhusiwa kuingia darasa la tatu kama hajui kusoma, kuandika na kuhesabu ili kuondoa tatizo la watoto wanaomaliza shule ya msingi wakiwa hawajui kusoma.
Pia imepunguza wingi wa masomo katika ngazi za chini kwa darasa la kwanza na la pili ambapo sasa watoto hao watasoma masomo matatu tu badala ya saba, huku ikifuta utaratibu wa walimu na watumishi wengine kulazimika kukubali vyeo kabla ya kuwarekebishia mishahara.
Kauli hiyo ilitolewa juzi na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) anayeshughulikia Elimu, Kassim Majaliwa wakati wa ufunguzi wa mafunzo kabilashi ya mtaala mpya kwa walimu wa darasa la kwanza na pili yanayofanyika katika ukumbi wa Chimwaga, Chuo Kikuu cha Dodoma.
Alisema serikali imeamua kuwapunguzia mzigo wa masomo wanafunzi ili waweze kumudu masomo yao. Pia kwenye sera mpya ya elimu mtoto wa darasa la pili hawezi kwenda la tatu kama hajui kusoma, kuandika na kuhesabu na atalazimika kurudia darasa mpaka afahamu.
Awali, mbali ya masomo hayo matatu, walikuwa wanasoma pia Kiingereza, Sayansi, Haiba na Michezo na Stadi za Kazi. "Sera mpya ya elimu ni bora lakini unashangaa leo mtu anasimama na kuikosoa.
Mtu wa aina hiyo ni wa kusamehewa tu. "Tumeamua kuwapunguzia mzigo wa masomo wanafunzi wa darasa la kwanza na la pili ambapo sasa watasoma masomo matatu ili kuimarisha uelewa wao na kuzingatia masomo na kama kuna kitu kitakachoongezwa bali ni elimu ya afya tu," alisema.
Alifafanua kwamba programu ya stadi za kusoma, kuandika na kuhesabu inalenga katika kuboresha elimu kwa watoto wote wenye umri kati ya miaka mitano hadi 13 nchini katika ngazi za elimu ya awali na msingi, elimu nje ya mfumo rasmi kwa watoto walio katika mazingira hatarishi na elimu ya malezi (Chekechea) kupitia vyuo vya maendeleo ya wananchi.
Naibu Waziri alisema programu hiyo imelenga katika maeneo matano ikiwemo kuwawezesha watoto wa shule za awali na msingi kusoma, kuandika na kuhesabu.
Pia kuwawezesha watoto ambao hawapo katika mfumo rasmi wa elimu katika masomo ya awali na msingi kuweza kusoma, kuandika na kuhesabu, kuongeza uelewa wa watoto wadogo ili kuwawezesha kuingia madarasa ya awali mapema.
Alisema malengo mengine ni kuimarisha mfumo wa elimu na watendaji wake katika maeneo ya mipango, uratibu na uongozi kwa lengo la kuwezesha utoaji wa elimu bora pamoja na kuongeza ushiriki wa jamii katika kuwezesha ujifunzaji wa watoto na ufundishaji wa stadi za kusoma, kuandika na kuhesabu.
Walimu wazamia semina Wakati huohuo, takribani walimu 1,000 wanaodaiwa kuzamia semina ya mtaala mpya inayoendelea mjini hapa, wametakiwa kuondoka kwa kuwa hawana mialiko maalumu. Naibu Waziri Majaliwa akizungumza na walimu hao juzi wakati wa kufungua mafunzo hayo, alisema kama kuna mwalimu anajijua amefika kwenye semina hiyo bila kufuata utaratibu ni bora ajiondoe mwenyewe, si kusubiri mpaka aondolewe.
Alisema idadi ya walimu walioalikwa kwenye semina hiyo, imezidi na hiyo inafanya washindwe kupatiwa mahitaji muhimu kama malazi na chakula.
"Nasikia kuna walimu wamekuja kuwakilisha walimu wengine, waliona tabu kupeleka barua kwenye shule husika na kuamua kuteua watu wao kuja hapa," alisema na kuongeza, "Hapa tulihitaji walimu ambao wanafundisha darasa la kwanza na la pili tu, lakini kama umekuja ukiwa hufundishi masomo hayo ukitoka kwenye mafunzo haya lazima ukafundishe masomo hayo," alisema.
Pia, alisema inawezekana kuna walimu wakuu wamekuja kwenye mafunzo hayo na kuacha wahusika ambao ni walengwa wakubwa wa mpango huo. Kaimu Katibu Mkuu Tamisemi, Mohamed Pawaga alisema mafunzo hayo yalilenga washiriki 4,430, lakini washiriki waliofika zaidi ya 5,000.
Alisema hali hiyo imeleta mkanganyiko mkubwa katika kuwahudumia, lakini kinachofanyika ni kuhakiki taarifa zao ili wale wanaostahili wabaki na wale wasiostahili kushiriki mafunzo hayo, warudi kwenye vituo vyao vya kazi.

Walimu wanaoshiriki mafunzo hayo ya awamu ya kwanza wanatoka mikoa ya Arusha, Dar es Salaam, Tanga, Singida, Rukwa, Ruvuma, Morogoro na Pwani . Jumla ya walimu 18,000 wanatarajiwa kupatiwa mafunzo hayo, yatakayotolewa kwa awamu. CHANZO: HABARI LEO (Muro)

 

POSTED BY: RASHID HAMZA