Ijumaa, 3 Aprili 2015

KATIBU MKUU ASONGA MBELE

ZIARA YA KINANA JIMBO LA MWANGA‏


 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipokelewa na kikundi cha ngoma wakati akiwasili kwenye kata ya Kileo,wilaya ya Mwanga ,anayeongozana na Katibu Mkuu ni Mbunge wa Jimbo la Mwanga na Waziri wa Maji Profesa Jumanne Maghembe.
 Kikundi cha utamaduni kikitumbuiza wakati wa mapokezi ya Katibu Mkuu wa CCM Ndugu abdulrahman Kinana alipotembelea kwenye kijiji cha Kileo,kata ya Kileo ambapo alijionea ujenzi wa nyumba za kisasa za walimu
              Nyumba ya kisasa ya  Waalimu wa shule ya sekondari Kileo
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwasalimu wakazi wa kata ya Kileo ambapo alijionea ujenzi wa nyumba bora za walimu.
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akipita juu ya mfereji wa maji katika Skimu ya umwagiliaji Kivulini
Mbunge wa Jimbo la Mwanga ,Waziri wa Maji Profesa Jumanne Maghembe (katikati) akimpa maelezo ya mradi Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana (kushoto) wakati alipotembelea skimu ya umagiliaji Kivulini ,mwingine pichani ni Katibu wa CCM Tawi la Kivulini Ndugu Nuru Juma Mwanga.
Skimu hii ya Umwagiliaji Kivulini hulimwa mpunga, mahindi,maharagwe na mboga mboga za majani.

Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki ujenzi wa mtaro wa maji katika skimu ya umwagiliaji Kivulini, kushoto ni Profesa Jumanne Maghembe Mbunge wa Jimbo la Mwanga na Waziri wa Maji .
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa Kivulini wilaya ya Mwanga na kuwaambia wajitahidi kutafuta masoko nje zaidi ya mkaa maalumu unaotengenezwa pumba ya mchele pamoja na majani ya makuruwila.
Mkaa huo unatengenezwa na kikundi cha Mkombozi Kivulini

Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na Katibu wa Itikadi na Uenezi Nape Nnauye mara baada ya kuzungumza na wananchi wa kata ya Kivulini, Kileo.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinanaakizungumza na Mbunge wa Jimbo la Mwanga na Waziri wa Maji Profesa Jumanne wakati wa kukagua mashine za kuvunia mpunga
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akiendesha gari maalumu la kuvunia mpunga
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na wananchi wa kata ya Lembeni kijiji cha Mangara ambapo alihimiza waendelee kushikama na kuwa na umoja.
Mbunge wa Jimbo la Mwanga akizungumza na wananchi wa kijiji chaMangara ,kata ya Lembeni .
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM kutoka wilaya ya Mwanga Ndugu Joseph Tadayo akiwasalimia wananchi wa kijiji cha Mangara
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiweka jiwe la msingi la ofisi ya CCM tawi la Mangara kata ya Lembeni
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipanda mti kama ishara ya kutunza mazingira nje ya jengo la ofisi ya CCM tawi la Mangara, Lembeni wilaya ya Mwanga.
Mbunge wa Jimbo la Mwanga ambaye pia ni Waziri wa Maji Profesa Jumanne Maghembe akicheza ngoma ya asili mbele ya Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana kabla ya kuingia kwenyekikao cha Halmashauri Kuu ya wilaya.
Wajumbe wa kikao cha Halmashauri Kuu ya Wilaya ya Mwanga wakimsikiliza kwa makini Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana .
Katibu Mkuu yupo kwenye ziara ya kuimarisha na kukijenga chama mkoa wa Kilimanjaro

 
 Mbunge wa Jimbo la Mwanga Profesa Jumanne Maghembe akisalimiana na Ndugu Wildad Msuya mara baada ya kuwali kwenye kijiji cha Kifula.
  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiingia kwenye uwanja wa mikutano Vuchama akiongozana na kikundi cha ngoma ya asili ya mjungu
Mjumbe wa NEC ,Ndugu Joseph Tadayo akiwasalimu wananchi wa Vuchama wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika uwanjani Vuchama wilaya ya Mwanga.
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia wakazi wa kijiji cha Vuchama kata ya Mwaniko ambapo aliwaambia wapinzani wameshapoteza dira.
Mzee akifuatilia kwa makini hotuba za viongozi wa chama.
Wazee wa Vuchama wakisikiliza hotuba.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wananchi wa kijiji cha Mwaniko kata ya Vuchama na kuwataka washkamane katika kusimamia haki na shughuli zao za kila siku za kuletea maendeleo.

 PAMOJA TUTASHINDA


chanzo blog kilimanjaro yetu


posted by rashid hamza


 

Nape Amtaka Zitto Ajenge Upinzani wa Kweli.....Asema Akitaka Heshima Aachane na Siasa za CHADEMA Zenye Mlengo wa Kuruga Amani


Siku chache baada ya aliyekuwa Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe, kutangaza kujiunga na  chama cha ACT-Tanzania, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Nape Nnauye, amemtaka kujenga upinzani wa kweli kwa ajili ya kujenga  nchi na si kubomoa.

Akizungumza katika mkutano wa hadhara wa kuhitimisha ziara ya Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, katika mikoa ya Dodoma, Arusha na Kilimanjaro, Nape alisema anamkaribisha mwanasiasa huyo upya katika ulingo wa siasa.

Alisema kinachotakiwa ni upinzani wenye lengo la kujenga na Zitto akitaka heshima aachane na siasa za Chadema zenye lengo la kuvuruga.

Hata hivyo, alisema hawawezi kuwa na mfumo wa vyama vingi vyenye lengo la kubomoa, hivyo ajenge upinzani wa kweli wa kuijenga nchi.

CHANZO Mpekuzi blog 

 

POSTED BY; RASHID HAMZA

WANAFUNZI WA VYUO VIKUU MWANZA WANENA

Wanafunzi Wa Vyuo Vikuu Jijini Mwanza Wamtaka Lowassa Agombee Urais......Wasema Hawapo Tayari Kuzibwa Midomo, Wapo Tayari Kufa Ili Lowassa Awe Lowassa Awe Rais


Shinikizo la kumshawishi Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa, kuchukua fomu ya kugombea urais katika Uchaguzi Mkuu Oktoba, mwaka huu, limeendelea na safari hii wanafunzi wa vyuo vikuu vitatu vya jijini Mwanza, wametoa tamko la kumtaka kuingia kwenye kinyang’anyiro hicho.

Wakizungumza na waandishi wa habari jana jijini hapa, viongozi wa vyuo vya Chuo Kikuu cha Mtakatifu Agostino (SAUT), Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) na Chuo Kikuu Katoliki cha Sayansi  na Tiba za Afya (CUHAS), walimtaka Lowassa kuchukua fomu ya kuwania urais wakati ukifika.

Viongozi hao waliyazungumza hayo wakati wakikabidhi misaada mbalimbali kwenye kituo cha kulelea watoto yatima cha Upendo Daima, jijini Mwanza.

Rais wa Serikali ya Wanafunzi wa CUHAS, Godfrey Kisigo, alisema wameamua kumuunga mkono Lowassa kwa sababu anapendwa na kila Mtanzania.

 Alisema wanamuomba muda ukifika awe mtu wa kwanza kujitokeza kuchukua fomu ili kugombea nafasi ya urais.

“Tamko hili ni la vyuo  vikuu vyote vya Mwanza, sauti zetu ni za busara kwa sababu zinataka kuikomboa nchi yetu kwa miaka 10 ijayo, tunayo imani kubwa na Lowassa katika hatma ya nchi hususan elimu kwa watu wote,” alisema na kuongeza:

“Hatma ya nchi hii ipo mikononi mwako na sisi wanavyuo hatuwezi kusubiri kuona tunakosa kiongozi atakayelisaidia Taifa kwa kuzibwa midomo, tupo tayari kufa ili uwe rais uokoe watakaobaki na Tanzania.”

Waziri Mkuu wa Serikali ya wanafunzi SAUT, Christopher Mkodo, alisema Chama Cha Mapinduzi (CCM) kisijaribu kukata jina la Lowassa kwani Tanzania bila kiongozi huyo Watanzania watakuwa wamenyimwa fursa ya kupata maendeleo ndani ya miaka 10.

Waliitaka CCM kusikiliza maoni ya wanachama wake  vinginevyo chama kitaharibika.

Mwakilishi wa CBE, Paul Dotto, alisema Lowassa ni chaguo la wanafunzi wa vyuo vikuu na wana imani ataifikisha Tanzania katika uchumi wa kati kabla ya malengo yaliyowekwa na Serikali.
chanzo mpekuzi blog
 

posted ; hassain mtunda

BLOGGERS WANENA

Wanaharakati, Bloggers, Wamtaka JK kutotia saini Miswada ya dharura iliyojadiliwa Bungeni

Mkurugenzi mtendaji wa Kampuni ya Jamii Media, Maxence Melo, akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam wakati wa kutoa tamko lililotolewa na Wanaharakati wa kutetea haki za binadamu

Mkurugenzi mtendaji wa Kampuni ya Jamii Media, Maxence Melo, (wamiliki wa mitandao maarufu ya mijadala kwa jamii kupitia mitandao ya jamii, JamiiForums na FikraPevu hapa nchini) akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam (hawako pichani) wakati wa kutoa tamko la pamoja lililotolewa na Wanaharakati wa kutetea haki za binadamu
KUFUATIA kitendo cha Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitisha miswada miwili ukiwemo Muswada wa Sheria ya Takwimu ya Mwaka 2015 na pamoja na Sheria ya Makosa ya Mtandaoni bila kurekebisha au kuviondoa vifungu vinavyokwenda kinyume na Katiba ya Jamhuri ya Muungano ya Muungano ya mwaka 1977, wanaharakati wa kutetea haki za binadamu kwa pamoja wamelaani vikali kupitishwa kwa miswada hiyo bungeni mjini Dodoma.
Tamko la baadhi ya Wanachama wake wakiwemo Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu (THRDC), SIKIKA, Mtandao wa Jinsia-TGNP, Kampuni ya Jamii Media ambao ni wamiliki wa mitandao maarufu nchini inayoendesha mijadala kwa jamii (JamiiForums na FikraPevu) pamoja na Mtandao wa Watoa Huduma za Msaada wa Kisheria (TANLAP) wameeleza kushtushwa kwa hatua hiyo na kwamba muswada wa takiwmu umetoa madaraka makubwa kwa Ofisi ya Taifa ya Takwimu kama Kitovu cha utoaji wa Takwimu nchini.(P.T)
Taarifa iliyotolewa leo Aprili 2, 2015 na Mratibu wa Kitaifa wa Mtandao huo, Onesmo Olengurumwa (FikraPevu imepata nakala), imesema muswada wa Sheria ya Makosa ya Mtandaoni unaainisha makosa yanayohusiana na matumizi ya mfumo wa kompyuta na Teknolojia ya Habari na Mawasiliano na kwamba inawabana sana watumiaji na hivyo kama Rais atasaini muswada huo wananchi wengi wataumia kuliko inavyofikiriwa na watu wengi.
"Sheria hii ya Mitandao itaminya kwa kiasi kikubwa uhuru wa wananchi kuwasilina na kupashana habari kama itasainiwa bila marekebisho. Ni dhahiri sheria hii imelenga kufuta kabisa matumizi ya mitandao ya kijamii kama vile Facebook, WhatsApp,JamiiForums, twitter, blogu n.k. Kupitishwa kwa sheria hii bila kufanyiwa marekebisho kutasabisha watanzania wengi kuwekwa hatiani bila sababu, lakini pia kutaondoa kabisa uhuru wa habari nchini"ilieleza sehemu ya tamko hilo.
Mbali na hayo taarifa hiyo imebainisha kuwa wanaharakati hao wameona kuwa sheria hiyo imetungwa kwa uharaka kwa malengo yaliyofichika hasa kipindi hichi cha vuguvugu la uchaguzi bila kuzingatia madhara yake kwa jamii ambayo hivi sasa inatumia kwa wingi mitandao ya kijamii kuwasiliana na kujadili mambo muhimu na kwamba mamlaka waliyopewa wakuu wa Vituo vya Polisi na Waziri mwenye dhamana yatawaumiza watanzania walio wengi hivyo ni vyema suala hilo likaangaliwa kwa jicho la pili ili mhimili wa Mahakama uweze kupata heshima yake.
Hata hivyo, wanaharakati hao wamewataka Watanzania wote na watumiaji wa mitandao ya kijamii kumtaka Rais Jakaya Kikwete, kusitisha kupitisha muswada huo, bali atoe muda kwa Watanzania kutoa maoni na mapungufu ya sheria hizi kwa ajili ya marekebisho mbalimbali.
Wakizungumzia kuhusu Muswada wa Takwimu uliopitishwa na Bunge wamesema muswada huo unataka taasisi zote za Serikali, Mashirika Binafsi, Taasisi za Elimu ya Juu, Vyuo vikuu na Taasisi za Utafiti kutokuwa na uhuru wa kutoa matokeo ya tafiti wanazozifanya bila ya kibali au ridhaa ya Ofisi ya Takwimu hali ambayo itakuwa inawanyima haki wananchi kujua mambo yanayoendelea kwenye taifa lao.
"Rais Jakaya Kikwete, amekuwa akijahidi kuanzisha progamu mbalimbali za uwazi na ukweli kama vile Open Government Partnership na mengineyo. Hivyo tunamsihi sana asikubali kutia sahihi sheria hii ya Takwimu kwa kuwa inakwenda kinyume na Misingi ya Utawala Bora pamoja na vifungu vya kikatiba. Asitishe kutia saini kwenye sheria hii hadi itakapofanyiwa marekebisho ya vifungu vinavyolalamikiwa"
Wakati Taifa likihubiri kuzingatia uhuru wa vyombo vya habari na haki ya kupata habari, wamesema wanashangazwa kuona serikali inazidi kuongeza sheria kandamizi dhidi ya uhuru wa habari kutokana na sheria kulenga kuua uhuru wa habari kwa kuweka adhabu ya faini isiyopungua milioni 10 na kuifungo cha miaka miwili kwa kuchapisha taarifa au takwimu za uongo au za upotoshaji.
Wamewataka wadau wote wa masuala ya utafiti nchini, vyombo vya habari, wananchi wote, wadau wa maendeleo na Wabunge, kutumia vyombo vyao vizuri kwa muda huu ili kuonyesha ubaya wa sheria katika kazi za utafiti chini na hata katika uhuru wa habari nchini.
Mtandao wa Mabloggers walalamika
Mtandao wa Waandishi wa habari kupitia mitandao nchini, Tanzania Bloggers Network (TBN) wamemtaka Rais Kikwete, kutopitisha muswada wa Sheria ya Makosa ya Mtandao, 2015 unaokandamiza uhuru wa mawasiliano mitandaoni na kwamba umoja huo ulishtushwa na kitendo cha bunge kukubali kuupitisha, kitendo ambacho hakikutarajiwa kutokana na kuwa mitandao bado ni kitu kipya nchini hivyo walihitaji maridhiano na wadau na elimu kati ya raia na Serikali ili wengi watambue yapi ni makosa kwa kutumia mitandao na yapi yanakubalika.
"Kimsingi TBN haipingi Tanzania kuwa na Sheria ya Makosa ya Mtandao bali inaiomba Serikali kuwashirikisha wananchi na hasa wadau wa habari na wanamitandao ya jamii ili kuridhiana kwa vipengele ambavyo vinaonekana kukandamiza uhuru wa vyombo vya habari. Na hatimaye kutokana na sheria isiyo na viashiria kandamizi juu ya uhuru wa kupata na pokea taarifa...tumeshuhudia watetezi wa haki za binadamu pamoja na wawakilishi wa watumiaji wa Mtandao wa intaneti nchini wakitoa sababu zenye uzito" ilieleza sehemu ya taarifa hiyo.
Taarifa hiyo imesema pia kuwa wao kama waandishi wengine ulimwenguni wanafuata maadili ya kazi zao ikiwa ni pamoja na kutunza usiri wa chanzo cha habari pale inapotakiwa lakini wanashangazwa na katika sheria hiyo wao kama bloggers, sheria hiyo inakiuka kipendele hicho kwa kuwalazimisha kutaja vyanzo vya habari.
"Tunakukumbusha kuwa mwananchi wa kawaida anayetumia mtandao wa intaneti kuwa hayuko salama kwani sheria hii inamlazimisha mtoa huduma wa mtandao kutoa taarifa za wateja wake jambo ambalo linahatarisha uhuru wa kutoa na kupokea habari"

Tangu kutolewa taarifa ya kuwepo kwa miswada hiyo katika Bunge la 10 na mkutano wa 19 wananchi mbalimbali katika mitandao ya kijamii ukiwemo mtandao wa JamiiForums wamesema sheria hiyo inaonekana imeletwa kwa malengo ya kupunguza matumizi mabaya ya mitandao kutokana na kutokuwepo na busara ya serikali kushishirika umma wa Watanzania kabla ya kuupitisha.

Chanzo:http://www.fikrapevu.com/

POSTED BY;ANNASTAZIA RH & HASSAIN MTUNDA

MAGAZETI YETU LEO


Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Ijumaa ya Tarehe 3 March 2015























POSTED BY; RASHID HAMZA

Alhamisi, 2 Aprili 2015

Thursday, April 2, 2015

Athari 12 Za Sheria Mpya Ya Masuala ya Mitandao ( Tanzania Cybercrimes Act, 2015 ) Iliyopitishwa Jana Bungeni......Athari Hizi Zimechambuliwa Na Mbunge David Kafulila

Sheria hii ni muhimu duniani kote na ndio maana hata Tanzania ilikuwa inangojea kupata sheria ya kuongoza masuala ya mitandao yaani Cyber Law kutokana na uhalifu wa aina mbalimbali wa masuala ya mitandao.


Sifa kuu ya sheria ya kuongoza masuala ya mitandao ni kuweka bayana makosa ya mitandaoni na pia kuyatolea adhabu. Sheria hii inayopitishwa kwa dharura madhara yake ni:

Moja, Kifungu 7 (2b): Mpokeaji wa ujumbe (receiver) anaweza kushtakiwa kwa kosa la kupokea ujumbe ambao sheria imeufanya kuwa wa jinai. (Mfano: Mtu akikuforwadia ujumbe, ukiupokea na wewe umefanya kosa la jinai).

Pili, Kifungu 21(1): Mtumia mtandao wa Intaneti yeyote hayuko salama kwani mtoa huduma wake analazimika kutoa habari zake kwa serikali pale zitakapohitajika (kwa lazima).

Tatu, Kifungu 8: Itakuwa ni kosa la jinai kama mtu ataweka wazi nyaraka za siri za serikali hata kama ni nyaraka ya kusaidia nchi kwa ujumla (Mfano: Matumizi mabaya ya mali ya umma).

Nne, Kifungu 14: Picha yoyote yenye mwelekeo unaoweza kuonekana kama ‘mchafu kingono’ inaweza kupelekea mtu kufungwa hadi miaka 10 au kulipa milioni 30; Sasa kama mtu kaweka picha yake Instagram ambayo sio ya ponografia lakini ‘ikatafsiriwa’ hivyo. Sheria haijatafsiri ponografia!

Tano, Kifungu 23: Je, ulijua kuwa ‘kusababisha maudhi ya hisia’ kwa mtu mwingine ni unyanyasaji na unaweza kufungwa kifungo kisichopungua mwaka mmoja?

Sita, Rejea adhabu ya ibara mbalimbali: Sheria hii kila kosa linaweza fanya mtu afungwe kifungo hadi cha maisha na kulipa pesa hadi zisizohesabika kwani hakijawekwa kikomo cha juu cha adhabu bali kikomo cha chini tu kwa Kiingereza “not less than”

Saba, Sheria haijaeleza vizuri suala la kutumia jina lisilo lako kwenye mtandao na hivyo mtu anaweza kushitakiwa kama kuna mtu mwingine mwenye jina kama hilo katika maisha halisi.

Nane, Serikali kupitia waziri husika ndio ina mamlaka ya kusema jambo lililowekwa kwenye mtandao ni la kweli, uongo au la kupotosha. Kumbuka hata ESCROW, EPA walisema ni uwongo; ni wangapi katika mtandao wangeshtakiwa kiuonevu kwa hili?

Tisa, Kifungu 22: Ukiweka ujumbe katika mtandao na ukaufuta au kuuboresha, kama ukishtakiwa kwa kuweka ujumbe huo unaweza kuhukumiwa pia kwa adhabu ya kuuboresha au kuufuta. Ni mara ngapi unafuta ‘status’ zako za WhatsApp? Unaweza shtakiwa kwa kuchelewesha ushahidi kisa tu ulifuta na hamna mtu anayeweza kujua ulifuta kwa kusudi au la.

Kumi, Mkuu wa kituo cha Polisi chochote kile nchini anaweza kuagiza wewe umpatie simu/laptop yako au taarifa zako zote (kwenye email, chats) au hata vifaa vyako au ofisi yako kwa ajili ya upelelezi bila oda ya Mahakama.

Kumi na moja, Kifungu 31 (3a): “As soon as practicable” the law states. Askari Polisi wakichukua vitu vyako wanaweza kukupatia listi ya vitu walivyovipokea muda watakaoona kwao inawezekana kufanya hivyo. Jiulize, inaweza chukua muda gani?

Kumi na mbili, Kifungu 31-35 & 39-45: Kama wewe ni Blogger au mtoa huduma ya mtandao, pale unapobaini kosa ukalitoa na uko katika mikakati ya kuitaarifu mamlaka husika (Kama sheria inavyosema), askari naye anaweza kwa wakati huohuo akaja kukagua na kuchukua vitu vya kazi zako, hivyo sheria inakinzana yenyewe kwa yenyewe. Blogger yuko sawa kisheria na askari yuko sawa kisheria.

Je, sheria hii ikisainiwa na Rais Jakaya Kikwete tutapona?

DAVID Kafulila
Mbunge wa Kigoma Kusini (NCCR-Mageuzi) 
 
POSTED HASSAIN MTUNDA

Thursday, April 2, 2015

Breaking News:Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Yaahirisha Kura ya Maoni Ya Katiba Mpya.....Zoezi La Uandikishaji Kuendelea Hadi Mwezi Wa 7


Tume ya Taifa ya uchaguzi (NEC) imesema kuwa kura ya maoni ya katiba inayopendekezwa, haitaweza kufanyika tena tarehe 30 April hadi hapo itakapotangazwa tarehe nyingine tena.
 
Akizungumza na waandishi wa habari  leo  mchana, mwenyekiti wa tume ya uchaguzi , Jaji Mstaafu Damian Lubavu amesema sababu ya kuhairisha kura hiyo April 30 ni kutokana na kutokamilika kwa zoezi la uboreshaji daftari la kudumu la wapiga kura  kutokana na changamoto za mashine za BVR.

Jaji  Lubavu  amesema zoezi la uandikishaji mkoa wa Njombe litakamilika April 18 na baada ya hapo itafuatia mikoa ya Ruvuma, Iringa, Mtwara na Lindi ‪. Vifaa vya kuandikishia (BVR kits) nyingine 248 zitawasili ndani ya wiki ijayo na vingine 1600 vitafuata baada ya muda mfupi. 
 
Pia,  amesema kama vifaa vya kuandikishia vitafika vyote zoezi la uandikishaji litakamilka ifikapo mwezi julai mwaka huu.
 
Jaji  Lubavu  ameainisha  kuwa Gharama za vifaa vyote vilivyoagizwa kwaajili ya vifaa vya kuandikishia (BVR kits) ni dola za Kimarekani milioni 72 ambazo ni sawa na Tsh bilioni 13,338,520,536
 
POSTED BY ; RASHID HAMZA