Jumatano, 29 Aprili 2015

CLOUDS

CLOUDS FM YASHINDA TENA TUZO YA UBORA YA SUPERBRAND KWA MARA YA TATU AFRIKA MASHARIKI.

 Picha ya pamoja ya baadhi ya makapuni binafsi waliopewa tuzo bora za
viwango,kutoka shoto ni Bi.Dorothy Mashamsham kutoka kampuni ya Mafuta
ya PetrolFuel,Mkurugenzi Mtendaji wa ITV/Radio One Bi Joyce
Mhaville,Mkurugenzi wa Uzalishaji na Vipindi Clouds Media Group Bwa.Ruge
Mutahaba,Meneja Masoko Bwa. Elisa Ernest kutoka kampuni ya bima ya
Alliance Insurance.
 Mkuu wa Kitengo cha Idara ya Uchambuzi wa viwango Afrika Mashariki,Bwana
Jawad Jaffer akiwa na baadhi ya viongozi wa juu wa kampuni ya Clouds
Media Group,kutoka kulia ni Mkuu vipindi wa Clouds FM Sebastian
Maganga,wa tatu ni Mkurugenzi wa vipindi na Uzalishaji Ruge Mutahaba na
Mkuu wa kitengo cha huduma,Promosheni na Tamasha Clouds Media Group.Bi
Fauzia Kullane.
 Mkuu wa Kitengo cha Idara ya Uchambuzi wa viwango Afrika Mashariki,Bwana
Jawad Jaffer akimkabidhi tuzo bora ya viwango Mkurugenzi wa Uzalishaji
na vipindi wa Clouds Media Group,Bwa. Ruge Mutahaba,kwenye hafla fupi ya
utoaji tuzo bora za viwango hizo iliyofanyika ndani ya hotel ya Hyatt Regency jijini Dar.
 Mkurugenzi wa Uzalishaji na Vipindi Clouds Media Group,Ruge Mutahaba akizungumza jambo  na Mkuu
wa Kitengo cha Idara ya Uchambuzi wa viwango Afrika Mashariki,Bwana Jawad Jaffer.
 Mkurugenzi wa Uzalishaji na vipindi wa Clouds Media Group,Bwa. Ruge Mutahaba akiishukuru taasisi
ya SUPERBRAND East Africa mbele ya wageni waalikwa na waaandishi wa
habari kwa kutambua ubora wa kituo cha redio hiyo na kuipa tuzo bora za
viwango katika Afrika Mashariki kwenye hafla fupi ya utoaji tuzo hizo
iliyofanyika ndani ya hotel ya Hyatt Regency jijini Dar.
 Baadhi ya Wageni waalikwa na wanahabari wakifuatilia jambo kabla ya utoaji
tuzo bora za viwanga a.k.a SUPERBRAND kwa makampuni binafis nchini
Tanzania.
Mkurugenzi wa Uzalishaji na Vipindi kutoka Clouds Media Group,Ruge Mutahaba akiwa amepozi na Mtangazaji wa ITV Bwa.Godwin Gondwe
 
…………………………………………………………………………….
KAMPUNI ya Clouds Media Group imeendelea kuwa kinara kwa ubora wa SuperBrand kwa mara ya tatu katika nchi za Afrika Mashariki.
 
 Mkuu wa Kitengo cha Idara ya Uchambuzi wa Viwango Afrika Mashariki,Jawad
Jaffer amesema kuwa matokeo ya utafiti huo ulizingatia maoni ya watalaam
wazoefu wa masoko na walengwa wa huduma za bidhaa ambao wanahaki ya
kuamua aina ya haki ya viwango bora vya superbrands na kupongeza
makampuni ambayo yamefanikiwa kuingia 20 bora.
 
Utafiti
huo umefanywa na idara ya uchambuzi wa viwango  makao makuu nchini
Uingereza kutokana na kuzingatia ushauri wa wataalam wa masoko  na maoni
ya watumiaji bidhaa zaidi ya 600 wa huduma hizo.
Amesema kampuni nyingi zilizoingia katika ubora wa superbrands ni 1000
zikapambanishwa na kufanya kampuni 20 ziingie katika ubora superbrands
na kufanya kampuni Clouds Media Group kuendelea kushikiria nafasi ya
jsu  kwa mwaka wa 2015 -2016.
 

POSTED BY; RASHID  HAMZA

RAISI KIKWETE

Rais Kikwete Azindua Meli Mbili Za KIVITA Kwa Kishindo Jijini Dar


RAIS Jakaya Kikwete, jana amezindua na kuzitunukia Kamisheni meli mbili za kivita za Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania Kamandi ya Wanamaji ambazo zitatumika kufanya doria na kulinda mipaka ya majini katika Bahari ya Hindi.


Meli hizo zimepewa majina ya P77 Mwitongo na P78 Msoga zenye urefu wa mita 60 na zina uwezo wa kufanya doria katika kina kirefu cha maji.


Rais Kikwete alisema, kupatikana kwa meli hizo kumeifanya Tanzania kuandika ukurasa mpya wa uhusiano kati yake na China ambao uliasisiwa na waasisi wa mataifa hayo hayati Mwalimu Nyerere na Mao Tse Tung.


Alisema meli hizo zimekuja nchini kwa msaada wa Serikali ya Watu wa China zikiwa na uwezo wa kubeba silaha nzito kila moja ikiwa na mizinga miwili mikubwa na midogo sita.


"Jeshi letu la Wanamaji wakati linaanzishwa 1971, lilisaidiwa na Serikali ya China meli 13, rada na wataalamu wetu kupatiwa nafasi mbalimbali za mafunzo...meli hizi zitatuongezea ulinzi katika mipaka yetu majini.


"Kilio kikubwa cha jeshi letu kilikuwa uwezo mdogo wa meli zetu, tumekuwa na kazi ya kutafuta meli hizo na sasa tuna mpango wa kuchukua meli nyingine kubwa zaidi zenye uwezo, kilichobaki ni taratibu za kifedha tu," alisema Rais Kikwete.


Aliongeza kuwa, lazima Tanzania ijenge uwezo wa kulinda mali zetu, mipaka, samaki na mitambo ya gesi ambayo imesimikwa baharini hivi karibuni.


Kwa upande wake, Waziri wa Ulinzi, Dkt. Hussen Mwinyi, alisema Serikali ya China imekuwa msaada mkubwa kwa Tanzania.


Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Davis Mwamunyange, alisema jeshi hilo limepiga hatua katika ununuzi wa dhana za kivita na kuendeleza mafunzo ya kijeshi.

Amiri Jeshi Mkuu Rais Jakaya Mrisho Kikwete akikagua mara baada ya kuzindua rasmi meli vita mbili za doria bahari kuu TNS Msoga na TNS Mwitongo kwenye sherehe zilizofanyika Kamandi ya Jeshi la Maji Kigamboni jijini Dar es salaam jana April 28, 2015

Amiri Jeshi Mkuu Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipata picha ya kumbukumbu na makamanda wa meli vita mbili za doria bahari kuu TNS Msoga na TNS Mwitongo kwenye sherehe zilizofanyika Kamandi ya Jeshi la Maji Kigamboni jijini Dar es salaam jana April 28, 2015

Amiri Jeshi Mkuu Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Chifu Edward Wanzagi wa kabila la Wazanaki (kati) pamoja na Mbunge wa Afrika Mashariki Mhe Makongoro Nyerere baada ya kuzindua rasmi meli vita mbili za doria bahari kuu TNS Msoga na TNS Mwitongo kwenye sherehe zilizofanyika Kamandi ya Jeshi la Maji Kigamboni jijini Dar es salaam jana April 28, 2015.

 

(PICHA NA IKULU)

 

POSTED BY;RASHID HAMZA

KIGOMA YETU

Majambazi Matatu (3) Yauawa na Jeshi la Polisi Mkoani Kigoma


JESHI  la Polisi Mkoani Kigoma limefanikiwa kuuwa majambazi watatu baada ya kurushiana risasi na kukamata silaha mbalimbali za kivita.

Akizungumzia tukio hilo ofisini kwake Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kigoma,Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Frednand Mtui alisema kuwa majira ya saa nane usiku katika eneo la  mto kahabwe mpakani mwa Wilaya ya Kakonko na Kibondo, askari Polisi wakiwa doria walirushiana risasi na majambazi ambao idadi yao haijajuikana na kufanikiwa kuwauwa majambazi watatu.

Alisema wamefanikiwa kukamata silaha moja aina ya AK.47 yenye namba 10363 ikiwa na risasi 11 ndani ya magazine na risasi 22 za SMG ndani ya mfuko wa rambo pamoja na mabomu 2 ya kutupa kwa mkono .

Kamanda Mtui alisema kuwa aina ya mabomu waliyokutwa nayo majambazi hao ni offensive handgrenade namba Y.3PM-2 na jingine ni aina  ya deffensive handgrenade ambalo namba zake hazisomeki.

''Leo ilikuwa ni siku ya mnada hivyo inaonekana majambazi hao walijipanga kwenda kupora mali na pesa katika mnada wa leo,tunawashukuru raia wema kwa kutoa taarifa mapema na kufanikiwa kuwanasa majambazi hao na kuwauwa''alisema Kamanda Mtui

Alisema maiti za majambazi wote watatu ambao majina yao hayajafahamika ila wote wana umri kati ya miaka 25-35 zimehifadhiwa katika Wilaya ya Kibondo na upelelezi wa tukio hilo unaendelea.

POSTED BY; RASHID HAMZA

Ijumaa, 17 Aprili 2015

KIGOMA KUMEKUCHA

VIONGOZI WA SHIRIKISHO MKOA KIGOMA WAKIWA KWENYE VIKAO MBALIMBALI

 KATIBU WA SHIRIKISHO MKOA WA KIGOMA BWA HASSAN BUSORO AKIZUNGUMZA JAMBO
 MUHESHIMIWA KATIBU AKIENDELEA KUSOMA TAARIFA
 KATIBU AKIENDELEA KUSOMA TAARIFA HIYO


 MEZA KUU WAKIMSIKILIZA KATIBU KWA MAKINI SANA


 HAWA NI BAADHI YA WANACHUO WALIOHUDHURIA MKUTANO HUO

 WAJUMBE AKIENDELEA KUMSIKILIZA

 WANACHUO WAKISIKILIZA KWA MAKINI


 WANACHUO WAKIWA MAKINI MNO KUMSIKILIZA KATIBU SHIRIKISHO MKOA WA KIGOMA

 WAKISIKILIZA KWA MAKINI

 HAPA BAADHI YA WANACHUO WAKIANDIKA DONDOO



 HAPA BAADHI YA WANACHUO WAKIMSIKILIZA



 HAPA BAADHI YA WANACHUO WAKIMSIKILIZA
 HAPA BAADHI YA WANACHUO WAKIMSIKILIZA


  HAPA BAADHI YA WANACHUO WAKIMSIKILIZA
  HAPA BAADHI YA WANACHUO WAKIMSIKILIZA
  HAPA BAADHI YA WAGENI RASMI WAKIMSIKILIZA


 MUHESHIMIWA KATIBU WA MKOA AKIENDELEA KUHUTUBIA

 HAPA AKIKABIDHI TAARIFA KWA MGENI RASMI KATIBU WA MKOA WA CCM  KIGOMA
 HAPO AKISALIMIANA VIONGOZI WA MEZA KUU


 KATIBU WA CCM KIGOMA MJINI AKIHUTUBIA


 KATIBU WA UWT MKOA NA KATIBU WA VIJANA KIGOMA MJINI WAKISIKILIZA
 MGENI RASMI NA MNEC MHESHIMIWA MAYONGA KAHENA WAKISIKILIZA
 KATIBU WA SHIRIKISHO  UCHUMI NA FEDHA MKOA  BI; HADIJA  RUGETE AKISIKILIZA KWA MAKINI
VIONGOZI WA MATAWI (CHUO)

 M/KITI WA TAWI CHUO CHA KIHINGA F.DC  BWANA HUSSEIN H.  BUSORO

 HAPA VIONGOZI NA WANACHUO WAKIWA WANAIMBA MWIMBO KWA FURAHA NA RAHA TELE
 MGENI RASMI KATIBU WA CCM MKOA WA KIGOMA AZUNGUMZA JAMBO (AKIHUTUBIA)
 MUHESHIMIWA KATIBU WA CCM MKOA AKIENDELEA KUTOA UJUMBE KWA WANACHUO
 KATIBU WA UHAMASISHAJI SHIRIKISHO BWANA RUWAZA SHABANI AKIIMBA WIMBO KWA FURAHA






  KATIBU WA UVCCM KIGOMA MJINI NA VIJIJINI PAMOJA NA KATIBU WA MKOA UWT



 WANACHUO WAKIENDELEA KUSIKILIZA



 


POSTED TODAY BY;RASHID HAMZA

Waziri Sitta Awatimua Vigogo wa Kampuni ya Reli nchini (TRL)..... Madeni Kipande Wa TPA Kafukuzwa Kazi Rasmi


SERIKALI imewasimamisha kazi karibu viongozi wote wakuu wa Kampuni ya Reli nchini (TRL), kwa kile kilichoelezwa kuwa hujuma ya mabilioni ya shilingi yaliyotumika kununua mabehewa chakavu.


Waliosimamishwa ni pamoja na Mkurugenzi Mtendaji, Kipallo Kisamfu, Mhandisi Mkuu wa Mitambo, Ngosomwile Ngosomiles, Mhasibu Mkuu, Mbaraka Mchopa, Mkaguzi Mkuu wa Ndani, Jasper Kisiraga na Meneja Mkuu wa Manunuzi wa kampuni hiyo, Ferdinand Soka.

 

Wakati hayo yakiwakuta hao, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari (TPA), Madeni Kipande aliyekuwa amesimamishwa kazi kutokana na tuhuma mbalimbali, sasa amefukuzwa rasmi.

 

Hayo yaliwekwa hadharani jana na Waziri wa Uchukuzi, Samuel Sitta alipokutana na waandishi wa habari na kutoa taarifa ya uchunguzi kuhusu ununuzi wa mabehewa machavu katika Kampuni ya Reli nchini.

 

Sitta, mmoja wa wanasiasa wakongwe aliyeshika nyadhifa mbalimbali serikalini ikiwa ni pamoja na uwaziri tangu enzi za utawala wa Awamu ya Kwanza chini ya Mwalimu Julius K. Nyerere, alisema mbali ya madudu yaliyoonekana katika kamati iliyoundwa na mtangulizi wake katika wizara hiyo, Dk Harrison Mwakyembe, waligundua mambo mengi Jumatatu wiki hii.

 

Yaliyogunduliwa ni pamoja na ukiukwaji mkubwa wa masharti ya mkataba wa ununuzi wa mabehewa hayo, kwani mzabuni alilipwa fedha zote, tofauti na taarifa za awali iliyoonesha malipo yangefanyika kwa awamu.

 

“Hivyo wizara ina maoni kwamba mazingira ya utekelezaji wa mkataba huu yana dalili za hujuma kwa TRL na kwa nchi yetu na siyo uzembe,” alisema Sitta. 

 

Akifafanua hilo alisema TRL iliagiza mabehewa ya mizigo 274 ambapo zabuni ilikwenda kwa Kampuni ya Hindustan & Industrial Engineering Limited ya India, ambapo katika uagizwaji wa mabehewa hayo kulikuwa na uzembe katika ufuatiliaji kiwandani, pamoja na uzembe katika kuyapokea yakiwa mabovu.

 

Alisema mabehewa hayo yalipofikia 150 aliyazuiwa, hivyo 124 yakawa bado hayajafika nchini. Sitta alisema kwa mujibu wa taarifa alizonazo ilibidi mpaka sasa asilimia 50 ya gharama ya mabehewa hayo iwe imeshalipwa, lakini kinyume chake nyaraka zinaonyesha mpaka sasa pamoja na kuzuiwa kwa mabehewa 124 mzabuni huyo ameshalipwa asilimia 100.

 

“Huu ni uzembe, ni hujuma kama kiongozi sitamstahi yeyote atakayekuwa sehemu ya hujuma,” alisema Sitta.

 

Alisema kutokana na hali hiyo ameagiza kwamba uchunguzi wa kubaini uwezekano wa hujuma ufanyike, hivyo amemwelekeza Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Dk Shaaban Mwinjaka asimamie kuundwa kwa kamati ya uchunguzi.

 

Alisema kamati hiyo itaongozwa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kwa kushirikiana na Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (TAKUKURU), Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi katika Sekta ya Umma (PPRA), na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

 

Sitta ametoa wiki tatu kuanzia Jumatatu ijayo Aprili 20, mwaka huu kuchunguza na kukamilisha kazi. Katika kipindi hicho, viongozi wakuu wa kampuni hiyo ya reli wanaowajibika na mkondo wa kashfa hiyo ya uagizaji na malipo ya ununuzi wa mabehewa hayo wote wamesimamishwa kupisha uchunguzi huo.

 

Aidha, alisema tangu mwanzoni mwa mwaka huu serikali ilikuwa ikifanyia kazi tuhuma zinazohusu mabehewa mabovu ya mizigo yaliyoagizwa kutoka India na TRL, baada ya kukamilika kwa uchunguzi wa tuhuma hizo na kamati iliyoundwa na Mwakyembe, aliagiza bodi ya wakurugenzi ya TRL ipitie taarifa hiyo na maelezo ya suala zima la mabehewa hayo.

 

Alisema katika uchunguzi huo ilibainika kuwa mabehewa mengi kati ya yaliyoagizwa yana kasoro, pia kulikuwa na uzembe katika uagizaji na ufuatiliaji kiwandani yalipokuwa yanatengenezwa na kulikuwa na uzembe katika kuendelea kuyapokea mabehewa hayo pamoja na ubovu wake kujulikana.

 

Alisema amemteua Elias Mshana kukaimu nafasi ya Mkurugenzi Mtendaji hadi hapo uchunguzi utakapokamilika. Pia ameagiza bodi ya wakurugenzi ya TRL ikutane kuteua watumishi wenye sifa kukaimu nafasi wanaozishikilia waliosimamishwa kazi.

 

Kipande wa TPA  Akizungumza suala la Kipande, Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Bandari aliyekuwa amesimamishwa kazi tangu Februari 16, mwaka huu ili kupisha uchunguzi wa tuhuma mbalimbali dhidi yake, Sitta alisema Tume aliyoichagua ilikamilisha kazi yake Machi 20, na kumkabidhi taarifa ya uchunguzi wao Machi 24 kwa hatua zaidi.

 

“Baada ya kuisoma taarifa ya tume na hatimaye kushauriana na taasisi mbalimbali zinazohusika na masuala haya, tumeridhika pasipo mashaka yoyote kwamba isingefaa Madeni Kipande kuendelea na kazi ya kuongoza Mamlaka ya Bandari.

 

“Hii ni kutokana na kuridhika na utawala mbovu aliouendesha uliosababisha manung’uniko mengi miongoni mwa wateja na wadau wa bandari na mgawanyiko mkubwa wa wafanyakazi,” alisema Sitta. 

 

Alisema kutokana na hali hiyo, serikali imeamua kumrejesha Kipande Idara Kuu ya Utumishi ili aweze kupangiwa majukumu mengine.

 

“Kipande ameonekana hafai kuongoza bandari ana maamuzi ya pupa, yasiyofuata taratibu pia yenye karaha. Tulichunguza uwezo wake wa kuendesha mamlaka ya bandari sasa kishapwaya inabidi arudishwe utumishi.

 

Hapa hatujachunguza masuala ya jinai, bali uwezo wa kutenda kazi,” alisema Sitta.
 
Tangu kusimamishwa kwa Kipande ambaye alikuwa anakaimu nafasi ya Mkurugenzi Mkuu, Ephraim Mgawe aliyekuwa ameondolewa kutokana na tuhuma mbalimbali, nafasi hiyo sasa inashikiliwa na Awadhi Massawe aliyepata baraka za Waziri Sitta na kuendelea kuwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu TPA.

 

POSTED BY; RASHID HAMZA

MAGARI YETU YATATUPONESHA KWELI

Ajali ya Daladala yaua watu 19 Leo jijini Mbeya



Ajali ya Daladala imeua watu 19 eneo maarufu kama Uwanja wa ndege, Kiwila, Mkoani Mbeya baada ya daladala hiyo kutumbukia kwenye Mto.
 
Habari  toka  eneo la tukio zinaarifu kuwa watu wawili tu ndio wamepona akiwemo kondakta. 
 
Ajali hii imetokea baada  ya Coaster zinazofanya safari zake kati ya Mbeya na Kyela kugoma hivyo baadhi ya daladala za mjini kuamua kubeba abiria.