WATANZANIA TUUNGANE KUENDELEZA NA KUPATA HABARI KUTOKA KWA WANANCHI WETU WA KIGOMA PAMOJA TUTASHINDA BLOGER BY; RASHID HAMZA 0672965856 MAARUFU KAMA RASHID ZAGA AU DOGO 'R'
Alhamisi, 30 Aprili 2015
PESA ZETU
Sarafu ya Sh 500 YAHUJUMIWA....... Yanunuliwa kwa Sh. 2500 hadi 5000 ili Kutengeneza Mikufu, Benki Kuu Ya Tanzania (BoT) Yatoa Tamko
SARAFU mpya ya shilingi 500 inadaiwa kuhujumiwa na baadhi ya watu ambao huinunua kwa Sh 2,500 na baadaye kuiyeyusha kwa ajili ya kutengenezea mikufu ya fedha (silver).
Taarifa ambazo tumezipata kutoka vyanzo mbalimbali zinaeleza
tangu sarafu hizo zilipotolewa kwa mara ya kwanza Oktoba mwaka jana,
baadhi ya watu wamekuwa wakizikusanya na kuzifanya kuadimika mtaani.
Imeelezwa kuwa tangu kutolewa kwa sarafu hiyo imekuwa adimu mitaani
jambo ambalo si kawaida kwa fedha mpya zinazoingizwa kwenye mzunguko
kuadimika kwa kiwango hicho.
“Nimekutana na watu watatu wakitafuta sarafu ya Sh 500 kwa Sh 2,500 hadi
5,000, mwanzoni nilipuuza lakini baada ya kutulia na kufanya utafiti
nimegundua kwamba kwanza hii sarafu imekuwa adimu na inatafutwa kwa udi
na uvumba,” kilisema chanzo chetu cha habari jijini Dar es Salaam.
Alipoulizwa kupitia simu yake ya kiganjani kuhusu hujuma hizo, Meneja
Sarafu wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Jovent Rushaka, alisema taarifa
hizo wanazo na wanazifanyia kazi.
“Taarifa hizo tumezipata juzi na tunalifanyia kazi suala hilo, kwa sasa
tunafanya uchunguzi zinakofanyiwa kazi, zinakouzwa ili tuweze kwenda
katika maduka hayo na kufanya uchunguzi,” alisema Rushaka.
Katika hatua hiyo, meneja huyo aliwataka Watanzania kwa yeyote atakayebaini sehemu zinakotengenezwa na kuuzwa atoe taarifa.
Alipoulizwa kuhusu aina ya madini iliyotengenezewa sarafu hiyo ya Sh
500, alisema imetengenezwa kwa madini ya chuma kwa asilimia 94.
“Asilimia sita iliyobaki imetengenezwa kwa madini aina ya nickel plated
silver ambayo kidogo unaweza kutengenezea mikufu ya ‘silver’. Sasa ni
mtu gani anayenunua madini ya chuma ni vigumu kuwezekana sasa, maswali
ya kujiuliza ni je, imetengenezwa na hiyo nickel plated silver?” alihoji
Rushaka.
Alipoulizwa sababu za sarafu hiyo kuadimika imetokana na nini, alisema BoT ilitoa sarafu hiyo tangu Oktoba mwaka jana na kwamba bado wanazo nyingi.
Alipoulizwa sababu za sarafu hiyo kuadimika imetokana na nini, alisema BoT ilitoa sarafu hiyo tangu Oktoba mwaka jana na kwamba bado wanazo nyingi.
“Tangu Oktoba mwaka jana tumezitoa nyingi kupitia Commercial Bank (benki
za biashara) na kama kuna mtu anahitaji aende kwenye benki hizo halafu
atapewa kwa sababu sisi tunasambaza kupitia benki hizo,” alisema
Rushaka.
Hata hivyo taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari na BoT jana ilisema
asilimia 94 ya madini katika sarafu ya Sh 500 ni chuma na asilimia 6 ni
Nickel.
Taarifa hiyo iliyotolewa na Mkurugenzi wa Huduma za Kibenki BoT, Marcian
Kobello ilieleza kuwa hadi sasa sarafu za Sh 500 zenye thamani ya zaidi
ya Sh bilioni moja zimesambazwa kote nchini.
Pia aliongeza kuwa Nickel sio miongoni mwa madini maarufu kwa ajili ya kutengeneza vidani vya thamani.
“Hakuna kabisa madini ya fedha katika sarafu ya shilingi 500,” alisema
Kobello na kuongeza kuwa haitegemewi kwamba mfanyabiashara yeyote
anaweza kununua sarafu hiyo kwa bei ya juu kuliko thamani yake halisi.
“Kwa hiyo, tunapenda kuwafahamisha wananchi kwamba kuna kiasi cha
kutosha cha sarafu za shilingi 500 nchini na kwamba kununua sarafu hiyo
kwa bei ya juu kuliko thamani yake ni kujiingizia hasara,” alisema
mkurugenzi huyo.
posted by rashid hamza
Vurugu Burundi: Mitandao ya Kijamii Ikiwemo Facebook,Twitter,Whatsapp Yafungwa
MAMLAKA nchini Burundi zimekata mawasiliano ya mitandao ya kijamii kupitia simu za mkononi, ambayo yamekuwa yakitumika kupanga maandamano ya kumpinga Rais Pierre Nkurunziza.
Mamia ya waandamanaji wako barabarani kwenye mji mkuu wa Burundi,
Bujumbura kwa siku ya nne jana wakipinga uamuzi wa Nkurunziza kuwania
urais kwa muhula wa tatu.
Mawasiliano hayo ni kupitia mitandao ikiwamo ya Facebook, Whatsapp,
Twitter na Tango huku kituo kikuu binafsi cha redio kikiwa kimefungwa
katika harakati za Serikali kuzuia kuenea kwa ujumbe unaohamasisha
maandamano.
Mitandao ya jamii imekuwa ikitumika kuratibu maandamano hayo ambayo ni
makubwa zaidi nchini Burundi tangu kumalizika kwa vita vya wenyewe kwa
wenyewe mwaka 2005.
African Public Rasio, maarufu kama ‘Sauti ya Wasio na Sauti’, ni moja ya
vituo vitatu vya redio ambavyo matangazo yake ya moja kwa moja
yamesitishwa, kwa kile Serikali ilichodai kuwa vinavuruga amani.
Nkurunziza, kiongozi wa zamani wa waasi ameonya kuwa yeyote anayetaka
kusababisha matatizo kwa chama tawala atajiweka mwenyewe matatani.
Watu watatu wameuawa tangu Jumapili wakati polisi walipoutawanya umati
kwa risasi za moto huku makumi kwa maelfu wakiikimbia nchi.
Chini ya Katiba ya Burundi, marais wanaweza kuchaguliwa kwa mihula
miwili , lakini washirika wa Nkurunziza wanasema muhula wake wa kwanza
hauhesabiki kwa vile aliteuliwa na Bunge.
Nkurunziza yu madarakani tangu mwaka 2005, wakati vita vya wenyewe kwa wenyewe vya miaka 12 vilipomalizika rasmi.
Watu zaidi ya 300,000 waliuawa katika mgogoro huo baina ya jeshi
lililodhibitiwa na Watutsi walio wachache na makundi ya waasi wa Kihutu
kama vile CNDD-FDD la Nkurunziza.
chanzo Mpekuzi blog
posted by;rashid hamza
IRAQ: Wapiganaji 91 wa Kundi la Dola la Kiislamu (IS) Wauawa
WAPIGANAJI 91 wa kundi la Dola la Kiislamu (IS) wameuawa na jeshi la Iraq lililokuwa likisaidiana na wapiganaji wa kujitolea katika sehemu mbalimbali huko nchini Iraq.
Wapiganaji hao waliuawa katika matukio mawili tofauti wakati vikosi vya jeshi la Iraq vilipokuwa vikipambana na wapiganaji hao.
Vyombo vya habari nchini Iraq vimetangaza kuwa Wizara ya Ulinzi ya Iraq imetoa taarifa kuwa vikosi vya Iraq vimewaua wapiganaji 61 wa kundi la IS na kuteketeza maficho manne ya wapiganaji hao.
Taarifa hiyo imesema kuwa magari manne ya kijeshi ya wapiganaji wa kundi la IS yajulikanayo kama Humvee ambayo yalikuwa yamesheheni silaha za milipuko pamoja na malori sita yaliyokuwa na silaha yameteketezwa.
Jeshi la Iraq na vikosi vya kujitolea vilifanya operesheni hiyo dhidi ya kundi hilo katika mji wa al Karmah umbali wa kilomita 16, kaskazini mashariki mwa Fallujah.
Mkoa wa Fallujah ni miongoni mwa mikoa ambayo imekumbwa na machafuko wa al-Anbar.
Katika tukio jingine tafauti vikosi vya Iraq vimewaua magaidi 30 wa kundi hilo na kutegua bomu moja lililokuwa limetegwa katika lori wakati vikosi vya Iraq vilipokuwa vikipambana na magaidi hao katika mji wa Ramadi.
Mji wa Ramad upo umbali wa kilomita 110 magharibi mwa Baghdad mji mkuu wa Iraq
chanzo mpekuzi blog
posted by rashid hamza
Jumatano, 29 Aprili 2015
CLOUDS
CLOUDS FM YASHINDA TENA TUZO YA UBORA YA SUPERBRAND KWA MARA YA TATU AFRIKA MASHARIKI.
Picha ya pamoja ya baadhi ya makapuni binafsi waliopewa tuzo bora za
viwango,kutoka shoto ni Bi.Dorothy Mashamsham kutoka kampuni ya Mafuta
ya PetrolFuel,Mkurugenzi Mtendaji wa ITV/Radio One Bi Joyce
Mhaville,Mkurugenzi wa Uzalishaji na Vipindi Clouds Media Group Bwa.Ruge
Mutahaba,Meneja Masoko Bwa. Elisa Ernest kutoka kampuni ya bima ya
Alliance Insurance.
viwango,kutoka shoto ni Bi.Dorothy Mashamsham kutoka kampuni ya Mafuta
ya PetrolFuel,Mkurugenzi Mtendaji wa ITV/Radio One Bi Joyce
Mhaville,Mkurugenzi wa Uzalishaji na Vipindi Clouds Media Group Bwa.Ruge
Mutahaba,Meneja Masoko Bwa. Elisa Ernest kutoka kampuni ya bima ya
Alliance Insurance.
Mkuu wa Kitengo cha Idara ya Uchambuzi wa viwango Afrika Mashariki,Bwana
Jawad Jaffer akiwa na baadhi ya viongozi wa juu wa kampuni ya Clouds
Media Group,kutoka kulia ni Mkuu vipindi wa Clouds FM Sebastian
Maganga,wa tatu ni Mkurugenzi wa vipindi na Uzalishaji Ruge Mutahaba na
Mkuu wa kitengo cha huduma,Promosheni na Tamasha Clouds Media Group.Bi
Fauzia Kullane.
Jawad Jaffer akiwa na baadhi ya viongozi wa juu wa kampuni ya Clouds
Media Group,kutoka kulia ni Mkuu vipindi wa Clouds FM Sebastian
Maganga,wa tatu ni Mkurugenzi wa vipindi na Uzalishaji Ruge Mutahaba na
Mkuu wa kitengo cha huduma,Promosheni na Tamasha Clouds Media Group.Bi
Fauzia Kullane.
Mkuu wa Kitengo cha Idara ya Uchambuzi wa viwango Afrika Mashariki,Bwana
Jawad Jaffer akimkabidhi tuzo bora ya viwango Mkurugenzi wa Uzalishaji
na vipindi wa Clouds Media Group,Bwa. Ruge Mutahaba,kwenye hafla fupi ya
utoaji tuzo bora za viwango hizo iliyofanyika ndani ya hotel ya Hyatt Regency jijini Dar.
Jawad Jaffer akimkabidhi tuzo bora ya viwango Mkurugenzi wa Uzalishaji
na vipindi wa Clouds Media Group,Bwa. Ruge Mutahaba,kwenye hafla fupi ya
utoaji tuzo bora za viwango hizo iliyofanyika ndani ya hotel ya Hyatt Regency jijini Dar.
Mkurugenzi wa Uzalishaji na Vipindi Clouds Media Group,Ruge Mutahaba akizungumza jambo na Mkuu
wa Kitengo cha Idara ya Uchambuzi wa viwango Afrika Mashariki,Bwana Jawad Jaffer.
wa Kitengo cha Idara ya Uchambuzi wa viwango Afrika Mashariki,Bwana Jawad Jaffer.
Mkurugenzi wa Uzalishaji na vipindi wa Clouds Media Group,Bwa. Ruge Mutahaba akiishukuru taasisi
ya SUPERBRAND East Africa mbele ya wageni waalikwa na waaandishi wa
habari kwa kutambua ubora wa kituo cha redio hiyo na kuipa tuzo bora za
viwango katika Afrika Mashariki kwenye hafla fupi ya utoaji tuzo hizo
iliyofanyika ndani ya hotel ya Hyatt Regency jijini Dar.
ya SUPERBRAND East Africa mbele ya wageni waalikwa na waaandishi wa
habari kwa kutambua ubora wa kituo cha redio hiyo na kuipa tuzo bora za
viwango katika Afrika Mashariki kwenye hafla fupi ya utoaji tuzo hizo
iliyofanyika ndani ya hotel ya Hyatt Regency jijini Dar.
Baadhi ya Wageni waalikwa na wanahabari wakifuatilia jambo kabla ya utoaji
tuzo bora za viwanga a.k.a SUPERBRAND kwa makampuni binafis nchini
Tanzania.
tuzo bora za viwanga a.k.a SUPERBRAND kwa makampuni binafis nchini
Tanzania.
Mkurugenzi wa Uzalishaji na Vipindi kutoka Clouds Media Group,Ruge Mutahaba akiwa amepozi na Mtangazaji wa ITV Bwa.Godwin Gondwe
…………………………………………………………………………….
KAMPUNI ya Clouds Media Group imeendelea kuwa kinara kwa ubora wa SuperBrand kwa mara ya tatu katika nchi za Afrika Mashariki.
Mkuu wa Kitengo cha Idara ya Uchambuzi wa Viwango Afrika Mashariki,Jawad
Jaffer amesema kuwa matokeo ya utafiti huo ulizingatia maoni ya watalaam
wazoefu wa masoko na walengwa wa huduma za bidhaa ambao wanahaki ya
kuamua aina ya haki ya viwango bora vya superbrands na kupongeza
makampuni ambayo yamefanikiwa kuingia 20 bora.
Jaffer amesema kuwa matokeo ya utafiti huo ulizingatia maoni ya watalaam
wazoefu wa masoko na walengwa wa huduma za bidhaa ambao wanahaki ya
kuamua aina ya haki ya viwango bora vya superbrands na kupongeza
makampuni ambayo yamefanikiwa kuingia 20 bora.
Utafiti
huo umefanywa na idara ya uchambuzi wa viwango makao makuu nchini
Uingereza kutokana na kuzingatia ushauri wa wataalam wa masoko na maoni
ya watumiaji bidhaa zaidi ya 600 wa huduma hizo.
huo umefanywa na idara ya uchambuzi wa viwango makao makuu nchini
Uingereza kutokana na kuzingatia ushauri wa wataalam wa masoko na maoni
ya watumiaji bidhaa zaidi ya 600 wa huduma hizo.
Amesema kampuni nyingi zilizoingia katika ubora wa superbrands ni 1000
zikapambanishwa na kufanya kampuni 20 ziingie katika ubora superbrands
na kufanya kampuni Clouds Media Group kuendelea kushikiria nafasi ya
jsu kwa mwaka wa 2015 -2016.
zikapambanishwa na kufanya kampuni 20 ziingie katika ubora superbrands
na kufanya kampuni Clouds Media Group kuendelea kushikiria nafasi ya
jsu kwa mwaka wa 2015 -2016.
POSTED BY; RASHID HAMZA
RAISI KIKWETE
Rais Kikwete Azindua Meli Mbili Za KIVITA Kwa Kishindo Jijini Dar
RAIS
Jakaya Kikwete, jana amezindua na kuzitunukia Kamisheni meli mbili za
kivita za Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania Kamandi ya Wanamaji
ambazo zitatumika kufanya doria na kulinda mipaka ya majini katika
Bahari ya Hindi.
Meli hizo zimepewa majina ya P77 Mwitongo na P78 Msoga zenye urefu wa mita 60 na zina uwezo wa kufanya doria katika kina kirefu cha maji.
Rais Kikwete alisema, kupatikana kwa meli hizo kumeifanya Tanzania kuandika ukurasa mpya wa uhusiano kati yake na China ambao uliasisiwa na waasisi wa mataifa hayo hayati Mwalimu Nyerere na Mao Tse Tung.
Alisema meli hizo zimekuja nchini kwa msaada wa Serikali ya Watu wa China zikiwa na uwezo wa kubeba silaha nzito kila moja ikiwa na mizinga miwili mikubwa na midogo sita.
"Jeshi letu la Wanamaji wakati linaanzishwa 1971, lilisaidiwa na Serikali ya China meli 13, rada na wataalamu wetu kupatiwa nafasi mbalimbali za mafunzo...meli hizi zitatuongezea ulinzi katika mipaka yetu majini.
"Kilio kikubwa cha jeshi letu kilikuwa uwezo mdogo wa meli zetu, tumekuwa na kazi ya kutafuta meli hizo na sasa tuna mpango wa kuchukua meli nyingine kubwa zaidi zenye uwezo, kilichobaki ni taratibu za kifedha tu," alisema Rais Kikwete.
Aliongeza kuwa, lazima Tanzania ijenge uwezo wa kulinda mali zetu, mipaka, samaki na mitambo ya gesi ambayo imesimikwa baharini hivi karibuni.
Kwa upande wake, Waziri wa Ulinzi, Dkt. Hussen Mwinyi, alisema Serikali ya China imekuwa msaada mkubwa kwa Tanzania.
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Davis Mwamunyange, alisema jeshi hilo limepiga hatua katika ununuzi wa dhana za kivita na kuendeleza mafunzo ya kijeshi.
Amiri Jeshi Mkuu Rais Jakaya Mrisho Kikwete akikagua mara baada ya kuzindua rasmi meli vita mbili za doria bahari kuu TNS Msoga na TNS Mwitongo kwenye sherehe zilizofanyika Kamandi ya Jeshi la Maji Kigamboni jijini Dar es salaam jana April 28, 2015
Amiri Jeshi Mkuu Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipata picha ya kumbukumbu na makamanda wa meli vita mbili za doria bahari kuu TNS Msoga na TNS Mwitongo kwenye sherehe zilizofanyika Kamandi ya Jeshi la Maji Kigamboni jijini Dar es salaam jana April 28, 2015
Amiri Jeshi Mkuu Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Chifu Edward Wanzagi wa kabila la Wazanaki (kati) pamoja na Mbunge wa Afrika Mashariki Mhe Makongoro Nyerere baada ya kuzindua rasmi meli vita mbili za doria bahari kuu TNS Msoga na TNS Mwitongo kwenye sherehe zilizofanyika Kamandi ya Jeshi la Maji Kigamboni jijini Dar es salaam jana April 28, 2015.
(PICHA NA IKULU)
POSTED BY;RASHID HAMZA
KIGOMA YETU
Majambazi Matatu (3) Yauawa na Jeshi la Polisi Mkoani Kigoma
JESHI la Polisi Mkoani Kigoma limefanikiwa kuuwa majambazi watatu baada ya kurushiana risasi na kukamata silaha mbalimbali za kivita.
Akizungumzia
tukio hilo ofisini kwake Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kigoma,Kamishna
Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Frednand Mtui alisema kuwa majira
ya saa nane usiku katika eneo la mto kahabwe mpakani mwa Wilaya ya
Kakonko na Kibondo, askari Polisi wakiwa doria walirushiana risasi na
majambazi ambao idadi yao haijajuikana na kufanikiwa kuwauwa majambazi
watatu.
Alisema
wamefanikiwa kukamata silaha moja aina ya AK.47 yenye namba 10363 ikiwa
na risasi 11 ndani ya magazine na risasi 22 za SMG ndani ya mfuko wa
rambo pamoja na mabomu 2 ya kutupa kwa mkono .
Kamanda
Mtui alisema kuwa aina ya mabomu waliyokutwa nayo majambazi hao ni
offensive handgrenade namba Y.3PM-2 na jingine ni aina ya deffensive
handgrenade ambalo namba zake hazisomeki.
''Leo
ilikuwa ni siku ya mnada hivyo inaonekana majambazi hao walijipanga
kwenda kupora mali na pesa katika mnada wa leo,tunawashukuru raia wema
kwa kutoa taarifa mapema na kufanikiwa kuwanasa majambazi hao na
kuwauwa''alisema Kamanda Mtui
Alisema
maiti za majambazi wote watatu ambao majina yao hayajafahamika ila wote
wana umri kati ya miaka 25-35 zimehifadhiwa katika Wilaya ya Kibondo na
upelelezi wa tukio hilo unaendelea.
POSTED BY; RASHID HAMZA
Jisajili kwenye:
Machapisho (Atom)