WATANZANIA TUUNGANE KUENDELEZA NA KUPATA HABARI KUTOKA KWA WANANCHI WETU WA KIGOMA PAMOJA TUTASHINDA BLOGER BY; RASHID HAMZA 0672965856 MAARUFU KAMA RASHID ZAGA AU DOGO 'R'
Jumatano, 1 Aprili 2015
MAGAZETI YA LEO
Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Alhamisi ya Tarehe 2 March 2015
CHANZO MPEKUZI BLOG
POSTED BY; RASHID HAMZA
KUELEKEA SIKUUU BEI ZAPANDA
Bei Za Vyakula ZZAPANDA Kuelekea Pasaka
Bei
za mazao katika kipindi hiki cha kuelekea sikukuu za Pasaka katika
soko la Kariakoo zimeongezeka kutokana na imani iliyojengeka kwa wafanya
biashara kuwa uwezo wa manunuzi unakuwa juu.
Meneja
Mkuu wa Shirika la Masoko ya Kariakoo, jijini Dar es Salaam, Florens
Seiya alisema jana katika taarifa yake aliyoitoa kwa vyombo vya habari.
Seiya
alisema kila inapofikia kipindi cha sikukuu kubwa za kidini, imekuwepo
desturi kwa wafanyabiashara nchini kupandisha bei za vitu sio kwenye
bidhaa tu hata nguo ama usafiri.
Alitaja
bidhaa zinazopanda bei katika kipindi hiki kuwa ni nyanya maji,
vitunguu maji, pilipili hoho, vitunguu swaumu, tangawizi, karoti,
njegere, matunda mbalimbali na mchele. Alisema wastani wa ongezeko za
bei hizo ni Sh 5,000 hadi 100,000 kutokana na aina ya mazao.
Alitolea
mfano nyanya kwa kawaida hivi sasa boksi ni Sh 35,000 lakini kipindi
hiki imekuwa Sh 40,000. Mchele gunia ni Sh 150,000 kipindi cha sikukuu
ni Sh 200,000. Tangawizi awali gunia liliuzwa Sh 200,000 hivi sasa ni Sh
300,000.
CHANZO Mpekuzi blog
POST BY; RASHID HAMZA
WAZIRI MKUU AZUNGUMZI JUU KURA YA KATIBA
Waziri Mkuu Asema NEC Ndiyo Itakayoamua Iwapo Kura ya Maoni Ifanyike April 30 au La.......Awataka Wafanyabiashara Wasitshe Mgomo, Atoa Neo kuhusu Mahakama ya Kadhi
POSTED BY ANNASTAZIA RH
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda ametoa ufafanuzi kuhusu suala la uandikishaji katika daftari la kudumu la wapigakura na siku maalum ya kupiga kura.
Amebainisha
kuwa kutokana na hali ilivyo, Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) ndio
itakayotoa ratiba kamili kuhusu hatma ya upigaji kura ya maoni.
Aidha,
katika mgogoro na mgomo wa wafanyabiashara unaoendelea, amewataka
wafungue maduka yao kwa kuwa tayari Serikali imeanza kushughulikia na
kuyafanyia kazi malalamiko yao.
Akizungumza
bungeni jana wakati wa kuhitimisha shughuli za mkutano wa 19 wa Bunge,
alisema Serikali inatambua kuwa muda uliobaki kufikia siku ya kupiga
kura ni mfupi, lakini Tume ndiyo yenye mamlaka kwa sasa ya kutoa ratiba
kamili kuhusu tukio hilo.
“Tunatarajia
Tume itatoa taarifa ya Ratiba itakayotumika kutuwezesha kukamilisha
zoezi la uandikishaji pamoja na kutoa taarifa siku za hivi karibuni
kuhusu upigaji wa Kura ya Maoni. Ni dhahiri muda uliobaki kuanzia sasa
ni mfupi lakini Tume ndiyo itakayotujulisha ratiba kamili,” alisisitiza.
Alisema
Serikali kwa upande wake, imehakikisha fedha yote kwa ajili ya ununuzi
wa BVR 8,000 zimelipwa kwa NEC na matarajio ni kwamba kazi ya
kuandikisha katika mikoa mingine itaanza na kuendelea kwa kasi.
Pia,
alisema wakati tume inajitahidi kufikia malengo hayo, Serikali
inaendelea na mipango ya kuelimisha wananchi kupitia redio,
televisheni, magazeti mbalimbali kuhusu umuhimu wa Katiba
inayopendekezwa ili kila mwananchi aielewe vizuri na kuweza kuipigia
kura kwa matakwa yake mwenyewe bila kurubuniwa muda utakapofika.
Alisema
tume hiyo imelenga kuandikisha wapiga kura milioni 21 na inakadiriwa
kutakuwa na vituo 36,164, kila kituo kitaandikisha kwa siku saba hadi 11
kutokana na idadi ya watu na vituo vitafunguliwa kuanzia saa mbili hadi
saa 12 jioni.
Akizungumzia
suala la mgogoro wa wafanyabiashara Pinda, alisema katika kushughulikia
suala hilo, Serikali ilikutana na wafanyabiashara hao na kukubaliana
kuwa kwa sababu Serikali imeonesha nia ya kushughulikia malalamiko na
changamoto zinazowakabili wafanyabiashara nchini ni vizuri mgomo huo
ukasitishwa.
“Serikali
inathamini sana mchango wa wafanyabiashara katika kukuza Uchumi na
kuchangia mapato ya Serikali. Napenda kuwahakikishia wafanyabiashara na
wananchi wote kwamba, Serikali ipo tayari kukaa pamoja na
wafanyabiashara kuzungumzia changamoto zinazowakabili na kuzipatia
ufumbuzi wa haraka,” alisisitiza.
Akizungumzia
suala la mauaji ya watu wenye ulemavu (albino), alisema itaendelea
kuchukua hatua mbalimbali za kiuchunguzi na kiupelelezi na kuwakamata
wote wanaohusika na mauaji hayo yaliyojirudia tena nchini na
kuwachukulia hatua za kisheria.
Alisema
kwa sasa jumla ya watuhumiwa 181, wakiwemo Wanaume 171 na Wanawake 10
walikamatwa na kuhojiwa, kati yao watuhumiwa 133 walifikishwa mahakamani
na kufunguliwa kesi za mauaji na 46 kwa makosa ya kujeruhi.
“Chanzo
kikubwa cha mauaji hayo ni imani za kishirikina. Aidha, Matukio 41 kati
ya 43 yametokea katika Ukanda wa Ziwa na Magharibi, kwani hadi sasa
yametokea matukio 13 ya Mauaji Mwanza, Kagera matukio sita (6), Tabora
matukio matano (5), Mara matukio manne (4), Geita matukio manne (4),
Kigoma matukio Manne (4) Simiyu matukio matatu (3) na Shinyanga matukio
mawili (2)” alisisitiza.
Kuhusu
Mahakama ya Kadhi, alisema katika Mkutano wa 18 wa Bunge Serikali
ilikusudia kuwasilisha bungeni Muswada wa Marekebisho ya Sheria
Mbalimbali na sehemu ya tano ya muswada huo, ilikusudia kurekebisha
Sheria ya Tamko la Sheria za Kiislamu.
Alisema muswada huo ni miongoni mwa Miswada minne ambayo haikupata nafasi ya kujadiliwa na Bunge.
“Serikali itatumia fursa kuendelea kushirikisha wadau mbalimbali kwa
lengo la kupanua uelewa juu ya maudhui na madhumuni ya Muswada huu”.
Pia,
Waziri Mkuu alitoa pole kwa ajali zilizotokea na maafa yaliyotokana na
mvua katika mikoa ya Dar es Salaam, Mtwara na Kahama mkoani Shinyanga.
Spika
wa Bunge, Anne Makinda, alilazimika kuvunja kikao cha asubuhi cha Bunge
majira saa nne, baada ya wabunge wa vyama vya siasa vya upinzani kugoma
mijadala mingine isiendelee hadi Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, atakapotoa
kauli juu ya mustakabali wa uandikishwaji wapiga kura na hatima ya kura
ya maoni.
Wabunge
hao, pamoja na kujibiwa na Spika kuwa suala hilo, litatolewa maamuzi
wakati Waziri Mkuu akihitimisha hoja ya kuahirisha Bunge, waligoma kukaa
na wote wakasimama bungeni, na kuanza kuimba wakiwa wamewasha vipaza
sauti huku wakigonga meza wakitaka hoja yao ijibiwe kwanza.
Chanzo
cha vurugu kilianza pale, Mbunge wa Kisarawe Selemani Jafo (CCM),
alipoomba mwongozo wa Spika, akitaka Bunge hilo lisitishe shughuli
zilizopangwa na kujadili suala la kura ya maoni na namna ya kutengeneza
Katiba ya mpito kwa ajili ya uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba mwaka
huu.
Katika
hoja yake hiyo, Jafo alisema kutokana na hali ilivyo ya uandikishaji
katika daftari la kudumu la wapiga kura, ni wazi kura ya maoni haiwezi
kufanyika Aprili 30, kama ilivypangwa.
Alisema
ni wakati sasa Bunge hilo, lianze kujadili vipengele kama vile mgombea
binafsi, kupinga matokeo ya urais mahakamani, kuwepo kwa tume huru ya
uchaguzi na umri wa wabunge na Bunge ili viingizwe na kupitishwa kwenye
kikao cha 20 cha Bunge ili Katiba ya Mpito ipitishwe.
Wakati
Jafo akitoa maelezo yake kuhusu mwongozo huo, baadhi ya wabunge wa
upinzani walikuwa wamesha vipaza sauti wakimpinga kwa madai kuwa, suala
analotaka siyo la dharura.
Baada
ya maelezo hayo ya Jafo, mbunge wa Ubungo, John Mnyika (Chadema) naye
aliomba mwongozo kwa kanuni ya 47 (1) inayohusu kusimamisha shughuli za
Bunge zilizopangwa kwa siku hiyo ili jambo la dharura lijadiliwe.
“Mheshimiwa
Spika uandikishaji wapiga kura nchi nzima, haujakamilika hata katika
mkoa wa Njombe, Watanzania wapo katika sintofahamu ni lini
wataandikishwa kwenye daftari la kudumu la wapiga kura,” alisema.
Alisema
suala hilo ni la dharura na lilishaombewa miongozo zaidi ya mara moja
bila majibu, hivyo si vyema Bunge hilo likaahirishwa bila kupatiwa
majibu juu ya hatma ya uandikishaji huo wa wapiga kura na kura ya maoni.
“Tusitishe
shughuli zote tuhakikishe tunajali, majibu yapatikane leo katika
mkutano huu wa Bunge, nimeomba miongozo juu ya jambo hili mara mbili na
mara zote Serikali haitoi majibu, sasa hakieleweki hapa hadi tupatiwe
majibu,” alisema Mnyika.
Alisema “Waziri Mkuu yupo hapa anaweza kutoa majibu hapa na tukajadili jambo hili hapa,” alisema Mnyika.
Baada
ya Mnyika kumaliza kuomba Mwongozo, Spika Makinda alibainisha kuwa hoja
hiyo ya Mnyika haina tofauti na Jafo, na zote zipatiwa majibu na Waziri
Mkuu wakati akitoa hoja ya kuahirisha Bunge.
Hata
hivyo, jibu hilo la Spika halikukubaliwa na wabunge hao wa upinzani na
ndipo mbunge wa Kasulu Mjini, Moses Machali, alipowasha kipaza sauti
bila ruhusa ya Spika na kusema “Hoja hii haifanani na hoja ya
kwanza, ile ya kwanza inataka majibu mkutano wa 20 na hoja hii ya pili
inataka majibu mkutano huu.”
Wabunge
wote wa upinzani wa vyama vya Chadema, NCCR-Mageuzi na CUF, walisimama
na kuwasha vipaza sauti huku wakiongea kwa nguvu kuwa hoja hizo
hazifanani na ni lazima hoja yao ipatiwe majibu kabla ya shughuli
nyingine za Bunge kuendelea.
Machali alidakia tena na kusema, “Tunataka majibu, tumechoka kuburuzwa.”
Spika Makinda aliwajibu kwa kusema “Anawaburuza
nani, nimewaambia kwamba swali lile litajibiwa leo (jana),au njooni
basi nyie muendeshe hiki kikao, kama hamtaki kukubali majibu yangu
tokeni nje.”
Huku
wabunge hao wakiwa bado wamesimama na kuimba kuwa wanataka majibu,
Spika alimwita Msemaji Kambi ya Upinzani kwenye Wizara ya Mawasiliano,
Sayansi na Teknolojia, ili asome maoni ya kambi hiyo juu ya Mswada wa
Sheria ya Miamala ya Kielektroniki ya mwaka 2014 na ule wa Makosa ya
Kimtandao wa mwaka 2015, lakini hakutoka.
Aidha
Spika aliendelea na kumtaka Katibu ataje shughuli inayofuata, ambaye
aliisoma kwa mara ya kwanza Miswada ya Shera ya Kupata Habari wa mwaka
2015, wa Sheria Vyombo vya Habari wa mwaka 2015, wa Sheria ya
Marekebisho ya Sheia ya Ushindani wa mwaka 2015 na wa Sheria ya Tume ya
Walimu wa mwaka 2015.
Wakati akisema hivyo, baadhi ya wabunge wa upinzani waliendelea kusema kuwa alichofanya siyo utaratibu.
Baada
ya hapo aliwafafanulia wabunge kuwa kwa mujibu wa kifungu cha 47
kinasema, iwapo Spika ataridhika kwamba jambo hilo ni la dharura na lina
maslahi kwa umma basi ataruhusu hoja litolewe kwa muda dakika tano, na
mjadala wa hoja utawezekana kama Spika ataridhika.
Pamoja na maelezo hayo, vurugu hizo za wabunge ziliendelea hadi alipoamua kuahirisha kikao hicho hadi jioni.
CHANZO MPEKUZI BLOG
GWAJIMA AMSHAURI MBASHA
Mbasha: "Gwajima Mungu Amenilipa, Njoo Uniombe Msamaha Tumalize Ugomvi"
Licha ya Mchungaji wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima kukanusha mara zote kwamba, hahusiki na kusambaratika kwa ndoa ya Mwimba Injili Flora Mbasha na mumewe, Emmanuel Mbasha, lakini mume huyo ambaye amekuwa akimshutumu Gwajima ameibuka na jipya.
Jipya aliloibuka nalo Mbasha ni kudai kuwa, msala uliompata Mchungaji
Gwajima wa kumtolea maneno yenye kuudhi Askofu wa Kanisa Katoliki Jimbo
Kuu la Dar es Salaam, Mwadhama Polycap Kadinali Pendo na kisha kuhojiwa
polisi na kupata mshtuko, kuzimia hadi kulazwa hospitali ni malipo ya
Mungu kwake kutokana na kilio chake.
Akizungumza na Amani kwa njia ya simu kwa dakika 15 juzi, Mbasha
alisema: “Ile hali (kupoteza fahamu) ya Gwajima ni malipo. Mimi
nilishasema jamani, mtu akikutendea ubaya malipo ni hapahapa duniani,
hakuna kwingine.
“Mimi ndoa yangu haipo, mke wangu anajua yeye anavyoishi. Kwa hivyo
mimi nimekuwa nikiishi kwa manung’uniko kila siku, unadhani nini
kitatokea kwake?”
Mbasha alikwenda mbele zaidi kwa kutoa tamko na agizo kwa mchungaji huyo kwa kusema:
“Tena namwomba Mungu ampe afya Gwajima, akitoka hospitali alikolazwa (TMJ, Dar) anitafute kuniomba msamaha.
“Ni vyema na itakuwa vyema zaidi akinitafuta na kuniomba msamaha ili
kila mmoja aishi kwa amani. Mimi nisiwe na kinyongo na yeye na wala yeye
asiwe na kinyongo na mimi.”
Mbasha hakumalizia hapo, alipoulizwa kama kauli ya Gwajima iliyosababisha mtafaruku ilikuwa sawasawa au la! Mbasha alisema:
“Hilo atajua yeye mwenyewe na Mungu wake, mimi sijui. Ila ninachojua
mimi ni kitu kimoja tu, kwamba Mungu amenilipia basi, sasa aniombe
msamaha.”
Naye mchungaji mmoja wa kanisa la Gwajima alipopatikana kwa simu na
kuulizwa kuhusu madai ya Mbasha, alisema:
“Yule hajui maandiko sawasawa. Hakuna uhusiano wowote kati ya kilichompata mchungaji wangu na hisia zake kuhusu mkewe Flora.
“Yule hajui maandiko sawasawa. Hakuna uhusiano wowote kati ya kilichompata mchungaji wangu na hisia zake kuhusu mkewe Flora.
“Gwajima na Flora hawana uhusiano wowote usiofaa. Sasa yeye anaposema
kalipiwa, kalipiwa kitu gani? Mungu anaweza kulipa jambo la hisia?”
Wiki mbili zilizopita, kwenye Viwanja vya Tanganyika Perkers ambako
kuna kanisa, Gwajima alitoa mahubiri yaliyolenga kumshutumu Kadinali
Pengo kwa kitendo chake cha kwenda kinyume na maazimio ya Baraza la
Maaskofu Tanzania kuhusu msimamo wao wa Mahakama ya Kadhi nchini.
Hali hiyo ilimfanya Gwajima kuitwa Polisi Kituo cha Kati, Dar na
kuhojiwa. Akiwa katika mahojiano, ghafla alisikia kizunguzungu,
akaanguka na kupoteza fahamu. alikimbizwa katika Hospitali ya Polisi
Baracks kisha Hospitali ya TMJ, Dar kwa matibabu zaidi.
Chanzo mpekuzi blog
post by;RASHID HAMZA
MAZISHI YA ABDU BONGE MENEJA TIPTOP
Kwenye safari ya mwisho ya Marehemu Abdul Bonge, alivyozikwa Morogoro.
Tip Top Connection ni kundi ambalo limeishi muda mrefu kwenye muziki wa Bongo Fleva, safari hiyo imekuwa ya mafanikio makubwa kutokana na usimamizi wa Marehemu Abdul Bonge.
Kundi hilo limepata pengo kumpoteza kiongozi huyo muhimu, safari yake ya mwisho duniani ilikuwa ni leo, wasanii, ndugu, jamaa na marafiki na watu wengine wameshirikiana kwenye mazishi ya Abdul Bonge ambayo yamefanyika leo Morogoro.
REST IN PEACE
_
Jisajili kwenye:
Machapisho (Atom)