Bei Za Vyakula ZZAPANDA Kuelekea Pasaka
Bei
za mazao katika kipindi hiki cha kuelekea sikukuu za Pasaka katika
soko la Kariakoo zimeongezeka kutokana na imani iliyojengeka kwa wafanya
biashara kuwa uwezo wa manunuzi unakuwa juu.
Meneja
Mkuu wa Shirika la Masoko ya Kariakoo, jijini Dar es Salaam, Florens
Seiya alisema jana katika taarifa yake aliyoitoa kwa vyombo vya habari.
Seiya
alisema kila inapofikia kipindi cha sikukuu kubwa za kidini, imekuwepo
desturi kwa wafanyabiashara nchini kupandisha bei za vitu sio kwenye
bidhaa tu hata nguo ama usafiri.
Alitaja
bidhaa zinazopanda bei katika kipindi hiki kuwa ni nyanya maji,
vitunguu maji, pilipili hoho, vitunguu swaumu, tangawizi, karoti,
njegere, matunda mbalimbali na mchele. Alisema wastani wa ongezeko za
bei hizo ni Sh 5,000 hadi 100,000 kutokana na aina ya mazao.
Alitolea
mfano nyanya kwa kawaida hivi sasa boksi ni Sh 35,000 lakini kipindi
hiki imekuwa Sh 40,000. Mchele gunia ni Sh 150,000 kipindi cha sikukuu
ni Sh 200,000. Tangawizi awali gunia liliuzwa Sh 200,000 hivi sasa ni Sh
300,000.
CHANZO Mpekuzi blog
POST BY; RASHID HAMZA
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni