Jumatano, 1 Aprili 2015

BELLA MKALI AU

Iliponifikia hii Video mpya ya Christian Bella, nimekuwekea na wewe uicheki hapa- ‘Nashindwa’

bellaMuziki wa Christian Bella ni burudani ambayo inamfikia kila mtu, message ya wimbo wa ‘Nani Kama Mama‘ inamgusa kila mtu kwa nafasi yake.

Tulimuona mkali huyu kwenye stage ya Serengeti FIESTA 2014 akipiga bonge la show, na kuna wakati stage alikuwa anaisimamia pekeyake na bado watu wanaikubali kazi yake.

Amekuja na hii mpya mtu wangu, wimbo unaitwa ‘Nashindwa’, tayari VIDEO imetoka na mimi nakusogezea hapa mtu wa Christian Bella uenjoy hii yani.

 

POST BY HASSAIN MTUNDA

j. Aaron kufanya fashion? Diamond na wimbo wake wa mduara.. Darasa na nyimbo mitandaoni #255 @CloudsFM

unnamed
Baada ya mtangazaji Adam Mchomvu kutangaza kwenda China kwa ajili ya kujifunza mambo ya ubunifu, Dj. Aaron wa Clouds FM amesema ameamua kuingia rasmi kwenye mambo ya fashion na kwa sasa anadesign vitu mbalimbali kama nguo zenye asili ya Tanzania za ‘Aarons Wear’ ambazo anategemea kuja kufanya uzinduzi rasmi muda mfupi.
COCO 2Weekend iliyopita Diamond Platnumz aliachia video ya wimbo wake mpya wa ‘Nasema Nawe’ aliomshirikisha Khadija Kopa, akizungumza kwenye 255 Diamond amesema ameamua kuimba mduara kwa sababu ana uwezo wa kufanya muziki wa aina yoyote na ukawa mzuri wimbo aliourekodi mwaka 2012.
Diamond amesema ameamua kufanya video na director Hanscana baada ya kupenda kazi alizozifanya na kuamini atafanya kitu kizuri na kweli ikawa hivyo video ambayo inafanya vizuri kwenye mitandao kwa kuangaliwa na watu wengi.
970948_509952679083997_929953988_n_fullMsanii Darasa amesema suala la wasanii kuuza nyimbo zao online halina faida kwa wasanii badala yake watu wanaouza ndio wanafaidika kwa sababu watu wanaingia kwenye Website kuangalia na kusikiliza nyimbo za wasanii na wengine wanadownload, lakini mwisho wa siku wasanii hawafaidiki chochote kama ambavyo wanapata wamiliki wa Website.

POSTED BY HASSAIN MTUNDA

VYUO VYETU

Majibu ya Pastor Myamba kuhusu malalamiko ya wanafunzi wa chuo cha Filamu…#U Heard

MyambaKwenye U Heard ya jana ilisikika story ya vijana waliokuwa wanasoma Chuo cha Filamu cha TFTC Ubungo, kinachomilikiwa na muigizaji Pastor Myamba kulalamikia suala la chuo hicho kutowakabidhi vyeti baada ya kumaliza masomo.
Wanafunzia hao wamesema walisoma katika Chuo hicho kozi ya miezi sita mwaka 2013, lakini mpaka leo hawajapewa vyeti wala kucheza filamu kama walivyoahidiwa na waliopewa vyeti walipoenda kutafuta kazi waliambiwa kuwa ni feki.
Leo Soudy Brown amemtafuta Pastor Myamba na kumuelezea malalamiko hayo ambae amesema ni tetesi za muda mrefu, lakini kuhusu mitihani wanafunzi ambao walifanya mtihani walipata vyeti ila wale ambao walikataa hawakupewa vyeti, kuhusu ishu ya tamthilia amesema ni project wanayofanya wanafunzi wenyewe lakini wakati wa kushoot walikuwa hawaonekani.
Kuhusu vyeti kukataliwa wanapoenda kuomba kazi, amesema vyeti hivyo ni halali na vilitolewa na BASATA lakini baadae aligundua kuna mapungufu ambayo yaliwataka wawe wanafanya mitihani tofauti na awali, alipowaambia wafanye mitihani hawakuwa tayari na wao wanataka vyeti hawataki mitihani.

POSTEDY BY; RASHID HAMZA 

THANKS MILLARD AYO

VITUKO

Mbwa huyu alipewa kazi ya kumlinda mtoto, kilichofuatia ni story mtu wangu…(Video)

pppMara nyingi mbwa hutumika katika nyumba kama walinzi na kwa nchi za wenzatu wamekuwa zaidi ya walinzi kwani wamekuwa wakipewa nafasi kubwa na kuwa sehemu ya familia kama rafiki wa karibu sana.
Hapa nimekuwekea video ya mbwa huyu ambaye alikuwa akimlinda mtoto lakini akajikuta na yeye akizidiwa na usingizi na kuamua kulala juu ya mtoto huyo ili kuendelea kumlinda.
Cheki video yake nimekuwekea hapa.

POSTED BY; RASHID HAMZA

THANKS; MILLARD AYO BLOG

IGP Mangu Afanya Mabadiliko Kwa Baadhi ya Makamanda wa Polisi wa Mikoa.


Inspekta Jenerali wa Polisi IGP Ernest Mangu amefanya mabadiliko kwa baadhi ya makamanda wa polisi wa mikoa.

Miongoni mwa makamanda wa mikoa waliofanyiwa mabadiliko ni pamoja na aliyekuwa kamanda wa Mkoa wa Simiyu, Naibu Kamishna wa Polisi (DCP) Charles Mkumbo anakwenda kuwa kamanda wa Polisi mkoa wa Mwanza na nafasi yake kuchukuliwa na aliyekuwa afisa mnadhimu mkoa wa Manyara Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Gemini Mushi.
 
Aliyekuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza Naibu Kamishna wa Polisi (DCP) Valentino Mlowola anakwenda kuwa Kaimu Kamishna wa Intelijensia makao makuu. 
 
Aliyekuwa kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala Naibu Kamishna wa Polisi (DCP) Maria Nzuki amehamishwa makao makuu kuwa mkuu wa polisi jamii na nafasi yake kuchukuliwa na aliyekuwa kamanda wa kikosi cha ufundi Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Lucas Mkondya.

Wengine ni aliyekuwa Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Godfrey Kamwela amehamishiwa Polisi Makao Makuu na nafasi yake kuchukuliwa na aliyekuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Njombe Kamishna Msaidi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Fulgence Ngonjani.
 
Aliyekuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Ulrich Matei amehamishiwa Kanda Maalum ya Dar es Salaam kuwa mkuu wa utawala na nafasi yake kuchukuliwa na aliyekuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kigoma Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Jafary Mohamed.
 
Aidha, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Ferdinand Mtui aliyekuwa mkuu wa operesheni maalum polisi makao makuu ameenda kuwa Kamanda wa Polisi mkoa wa Kigoma.

Zaidi ya hao wengine waliyohamishwa ni pamoja na aliyekuwa Kamanda wa Polisi mkoa wa Tanga Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Frasser Kashai amehamishiwa Polisi makao makuu na nafasi yake kuchukuliwa na aliyekuwa mkuu wa upelelezi mkoa wa Iringa Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Zuberi Mwombeji.
 
Aliyekuwa Kamanda wa Polisi mkoa wa Temeke Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Kihenya Kihenya amehamishiwa polisi makao makuu na nafasi yake kuchukuliwa na aliyekuwa mkuu wa polisi wa wilaya ya kati Ilala, Dar es Salaam Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Andrew Satta.

Kwa mujibu wa kanuni, taratibu na miongozo ya Jeshi la Polisi, mabadiliko hayo ni ya kawaida katika kuhakikisha kwamba usalama wa raia na mali zao unaendelea kuimarika.

Imetolewa na:
Advera Bulimba-SSP
Msemaji wa Jeshi la Polisi.
 POSTED BY ; R D PRODUCTION

THANKS MPEKUZI BLOG

MAGAZETI YETU LEO

POSTED BY; R D PRODUCTION

Wednesday, April 1, 2015

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumatano ya Tarehe 1 March 2015

Mpekuzi blog






















THANKS MPEKUZI BLOGY

WAPINZANI WAANZA

Breaking News: Vurugu Zaibuka Bungeni.......Wapinzani Wamtuhumu Spika Kuilinda Serikali, Bunge Laahirishwa hadi Mchana. Video Ya Tukio Hilo Iko Hapa.


Kikao cha  Bunge kimevunjika muda mfupi uliopita baada ya kutokea vurugu za maneno kufuatia wapinzani kutaka Waziri Mkuu atoe taarifa juu ya mwenendo wa kura ya maoni ya katiba mpya april 30,2015.

Kutokana na vurugu hizo za dakika kama 10 hivi Spika Anna Makinda amesitisha gafla shughuli za bunge hadi mchana.

Hali likuwa hivi:

Mnyika: Nimesimama kupata idhini kwa mujibu wa kanuni ili shughuli za bunge zisitishwe badala yake tujadili zoezi la uandikishaji nchi nzima.

Mpaka sasa zoezi halijakamilika hata kwa mkoa mmoja tu wa Njombe, jambo hili ni la dharura na lilishatolewa na ukaagiza kamati ishughulikie.Tunaomba majibu tupate kikao hiki na leo tunafunga mkutano.

Spika Makinda: Hoja hii inafanana na ile ya kwanza(  Hoja  ya  mbunge wa Kisarawe Seleman Jafo ambaye  alipendekeza kura ya maoni ya katiba  inayopendekezwa isogezwe mbele  na  badala  yake  kuwe  na  katiba  ya  mpito  kuelekea  uchaguzi  mkuu)

Baada  ya  kauli  hiyo, Mnyika  na  wabunge  wa  upinzani  walianza  kupiga  kelele  bungeni  wakidai  kuonewa  huku  wakimtuhumu  Spika  makinda  kuibeba  serikali.

Hata hivyo, Spika  hakuonesha  kutishwa  na  kelele  hizo  na  badala  yake  alimtaka  katibu  wa  Bunge  atoe  mwongozo  wa  kile  kinachofuata.

Katibu  alisimama  na  kuanza  kusoma  miswada  ya  habari ambapo  wapinzani  nao  walisimama  na  kuzidisha  kelele  huku  wakisema: "Tunataka majibu..Tunataka majibu. Tumechoka kuburuzwa..Makinda kwanini unailinda Serikali.??!!!

Hali  hiyo  ikamlazima  Spika  Makinda  Kuliahirisha  Bunge  hadi  mchana.

Tazama  Video  hapo  chini.



POSTEDY BY; RASHID  HAMZA