Majibu ya Pastor Myamba kuhusu malalamiko ya wanafunzi wa chuo cha Filamu…#U Heard
Kwenye U Heard ya jana ilisikika story ya vijana waliokuwa wanasoma Chuo cha Filamu cha TFTC Ubungo, kinachomilikiwa na muigizaji Pastor Myamba kulalamikia suala la chuo hicho kutowakabidhi vyeti baada ya kumaliza masomo.
Wanafunzia hao wamesema walisoma katika
Chuo hicho kozi ya miezi sita mwaka 2013, lakini mpaka leo hawajapewa
vyeti wala kucheza filamu kama walivyoahidiwa na waliopewa vyeti
walipoenda kutafuta kazi waliambiwa kuwa ni feki.
Leo Soudy Brown amemtafuta Pastor Myamba na
kumuelezea malalamiko hayo ambae amesema ni tetesi za muda mrefu,
lakini kuhusu mitihani wanafunzi ambao walifanya mtihani walipata vyeti
ila wale ambao walikataa hawakupewa vyeti, kuhusu ishu ya tamthilia
amesema ni project wanayofanya wanafunzi wenyewe lakini wakati wa
kushoot walikuwa hawaonekani.
Kuhusu vyeti kukataliwa wanapoenda kuomba kazi, amesema vyeti hivyo ni halali na vilitolewa na BASATA
lakini baadae aligundua kuna mapungufu ambayo yaliwataka wawe wanafanya
mitihani tofauti na awali, alipowaambia wafanye mitihani hawakuwa
tayari na wao wanataka vyeti hawataki mitihani.
POSTEDY BY; RASHID HAMZA
THANKS MILLARD AYO
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni