j. Aaron kufanya fashion? Diamond na wimbo wake wa mduara.. Darasa na nyimbo mitandaoni #255 @CloudsFM
Baada ya mtangazaji Adam Mchomvu kutangaza kwenda China kwa ajili ya kujifunza mambo ya ubunifu, Dj. Aaron wa Clouds FM amesema
ameamua kuingia rasmi kwenye mambo ya fashion na kwa sasa anadesign
vitu mbalimbali kama nguo zenye asili ya Tanzania za ‘Aarons Wear’ ambazo anategemea kuja kufanya uzinduzi rasmi muda mfupi.
Weekend iliyopita Diamond Platnumz aliachia video ya wimbo wake mpya wa ‘Nasema Nawe’ aliomshirikisha Khadija Kopa, akizungumza kwenye 255 Diamond
amesema ameamua kuimba mduara kwa sababu ana uwezo wa kufanya muziki wa
aina yoyote na ukawa mzuri wimbo aliourekodi mwaka 2012.
Diamond amesema ameamua kufanya video na director Hanscana
baada ya kupenda kazi alizozifanya na kuamini atafanya kitu kizuri na
kweli ikawa hivyo video ambayo inafanya vizuri kwenye mitandao kwa
kuangaliwa na watu wengi.
Msanii Darasa
amesema suala la wasanii kuuza nyimbo zao online halina faida kwa
wasanii badala yake watu wanaouza ndio wanafaidika kwa sababu watu
wanaingia kwenye Website kuangalia na kusikiliza nyimbo za wasanii na
wengine wanadownload, lakini mwisho wa siku wasanii hawafaidiki chochote
kama ambavyo wanapata wamiliki wa Website.
POSTED BY HASSAIN MTUNDA
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni