Jumatano, 1 Aprili 2015

MAGAZETI YA LEO

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Alhamisi ya Tarehe 2 March 2015






















CHANZO MPEKUZI BLOG


POSTED BY; RASHID HAMZA

KUELEKEA SIKUUU BEI ZAPANDA

Bei Za Vyakula ZZAPANDA  Kuelekea Pasaka


Bei za mazao katika kipindi hiki cha kuelekea sikukuu  za Pasaka katika soko la Kariakoo zimeongezeka kutokana na imani iliyojengeka kwa wafanya biashara kuwa uwezo wa manunuzi unakuwa juu.

Meneja Mkuu wa Shirika la Masoko ya Kariakoo, jijini Dar es Salaam, Florens Seiya alisema jana katika taarifa yake aliyoitoa kwa vyombo vya habari.
 
Seiya alisema kila inapofikia kipindi cha sikukuu kubwa za kidini, imekuwepo desturi kwa wafanyabiashara nchini kupandisha bei za vitu sio kwenye bidhaa tu hata nguo ama usafiri.
 
Alitaja bidhaa zinazopanda bei katika kipindi hiki kuwa ni nyanya maji, vitunguu maji, pilipili hoho, vitunguu swaumu, tangawizi, karoti, njegere, matunda mbalimbali na mchele. Alisema wastani wa ongezeko za bei hizo ni Sh 5,000 hadi 100,000 kutokana na aina ya  mazao.
 
Alitolea mfano nyanya kwa kawaida hivi sasa boksi ni Sh 35,000 lakini kipindi hiki imekuwa Sh 40,000. Mchele gunia ni Sh 150,000 kipindi cha sikukuu ni Sh 200,000. Tangawizi awali gunia liliuzwa Sh 200,000 hivi sasa ni Sh 300,000.
 
CHANZO Mpekuzi blog 
 
POST BY; RASHID HAMZA

WAZIRI MKUU AZUNGUMZI JUU KURA YA KATIBA

Waziri Mkuu Asema NEC Ndiyo Itakayoamua Iwapo Kura ya Maoni Ifanyike April 30 au La.......Awataka Wafanyabiashara Wasitshe Mgomo, Atoa Neo kuhusu Mahakama ya Kadhi

POSTED BY ANNASTAZIA RH

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda ametoa ufafanuzi kuhusu suala la uandikishaji katika daftari la kudumu la wapigakura na siku maalum ya kupiga kura.

Amebainisha kuwa kutokana na hali ilivyo, Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) ndio itakayotoa ratiba kamili kuhusu hatma ya upigaji kura ya maoni.
 
Aidha, katika mgogoro na mgomo wa wafanyabiashara unaoendelea, amewataka wafungue maduka yao kwa kuwa tayari Serikali imeanza kushughulikia na kuyafanyia kazi malalamiko yao.
 
Akizungumza bungeni jana wakati wa kuhitimisha shughuli za mkutano wa 19 wa Bunge, alisema Serikali inatambua kuwa muda uliobaki kufikia siku ya kupiga kura ni mfupi, lakini Tume ndiyo yenye mamlaka kwa sasa ya kutoa ratiba kamili kuhusu tukio hilo.
 
“Tunatarajia Tume itatoa taarifa ya Ratiba itakayotumika kutuwezesha kukamilisha zoezi la uandikishaji pamoja na kutoa taarifa siku za hivi karibuni kuhusu upigaji wa Kura ya Maoni.  Ni dhahiri muda uliobaki kuanzia sasa ni mfupi lakini Tume ndiyo itakayotujulisha ratiba kamili,” alisisitiza.
 
Alisema Serikali kwa upande wake, imehakikisha fedha yote kwa ajili ya ununuzi wa BVR 8,000 zimelipwa kwa NEC  na matarajio ni kwamba kazi ya kuandikisha katika mikoa mingine itaanza na kuendelea kwa kasi.
 
Pia, alisema wakati  tume inajitahidi kufikia malengo hayo, Serikali inaendelea na mipango ya kuelimisha wananchi kupitia  redio, televisheni, magazeti mbalimbali kuhusu umuhimu wa Katiba inayopendekezwa ili kila mwananchi aielewe vizuri na kuweza kuipigia kura kwa matakwa yake mwenyewe bila kurubuniwa muda utakapofika.
 
Alisema tume hiyo imelenga kuandikisha wapiga kura milioni 21 na inakadiriwa kutakuwa na vituo 36,164, kila kituo kitaandikisha kwa siku saba hadi 11 kutokana na idadi ya watu na vituo vitafunguliwa kuanzia saa mbili hadi saa 12 jioni.
 
Akizungumzia suala la mgogoro wa wafanyabiashara Pinda, alisema katika kushughulikia suala hilo, Serikali ilikutana na wafanyabiashara hao na kukubaliana kuwa kwa sababu Serikali imeonesha nia ya kushughulikia malalamiko na changamoto zinazowakabili wafanyabiashara nchini ni  vizuri mgomo huo ukasitishwa.
 
“Serikali inathamini sana mchango wa wafanyabiashara katika kukuza Uchumi na kuchangia mapato ya Serikali. Napenda kuwahakikishia wafanyabiashara na wananchi wote kwamba, Serikali ipo tayari kukaa pamoja na wafanyabiashara kuzungumzia changamoto zinazowakabili na kuzipatia ufumbuzi wa haraka,” alisisitiza.
 
Akizungumzia suala la mauaji ya watu wenye ulemavu (albino), alisema itaendelea kuchukua hatua mbalimbali za kiuchunguzi na kiupelelezi na kuwakamata wote wanaohusika na mauaji hayo yaliyojirudia tena nchini na kuwachukulia hatua za kisheria.
 
Alisema kwa sasa jumla ya watuhumiwa 181, wakiwemo Wanaume 171 na Wanawake 10 walikamatwa na kuhojiwa, kati yao watuhumiwa 133 walifikishwa mahakamani na kufunguliwa kesi za mauaji  na 46 kwa makosa ya kujeruhi.
 
 “Chanzo kikubwa cha mauaji hayo ni imani za kishirikina. Aidha, Matukio 41 kati ya 43 yametokea katika Ukanda wa Ziwa na Magharibi, kwani hadi sasa yametokea matukio 13 ya Mauaji Mwanza, Kagera matukio sita (6), Tabora matukio matano (5), Mara matukio manne (4), Geita matukio manne (4), Kigoma matukio Manne (4) Simiyu matukio matatu (3) na Shinyanga matukio mawili (2)” alisisitiza.
 
Kuhusu Mahakama ya Kadhi, alisema katika Mkutano wa 18 wa Bunge Serikali ilikusudia kuwasilisha bungeni Muswada wa Marekebisho ya Sheria Mbalimbali na sehemu ya tano ya muswada huo, ilikusudia kurekebisha Sheria ya Tamko la Sheria za Kiislamu.
 
Alisema muswada huo ni miongoni mwa Miswada minne ambayo haikupata nafasi ya kujadiliwa na Bunge. “Serikali itatumia fursa kuendelea kushirikisha wadau mbalimbali kwa lengo la kupanua uelewa juu ya maudhui na madhumuni ya Muswada huu”.
 
Pia, Waziri Mkuu alitoa pole kwa ajali zilizotokea na maafa yaliyotokana na mvua katika mikoa ya Dar es Salaam, Mtwara na Kahama mkoani Shinyanga.
 
Spika wa Bunge, Anne Makinda, alilazimika kuvunja kikao cha asubuhi cha Bunge majira saa nne, baada ya wabunge wa vyama vya siasa vya upinzani kugoma mijadala mingine isiendelee hadi Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, atakapotoa kauli juu ya mustakabali wa uandikishwaji wapiga kura na hatima ya kura ya maoni.
 
Wabunge hao, pamoja na kujibiwa na Spika kuwa suala hilo, litatolewa maamuzi wakati Waziri Mkuu akihitimisha hoja ya kuahirisha Bunge, waligoma kukaa na wote wakasimama bungeni, na kuanza kuimba wakiwa wamewasha vipaza sauti huku wakigonga meza wakitaka hoja yao ijibiwe kwanza.
 
Chanzo cha vurugu kilianza pale, Mbunge wa Kisarawe Selemani Jafo (CCM), alipoomba mwongozo wa Spika, akitaka Bunge hilo lisitishe shughuli zilizopangwa na kujadili suala la kura ya maoni na namna ya kutengeneza Katiba ya mpito kwa ajili ya uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba mwaka huu.
 
Katika hoja yake hiyo, Jafo alisema kutokana na hali ilivyo ya uandikishaji katika daftari la kudumu la wapiga kura, ni wazi kura ya maoni haiwezi kufanyika Aprili 30, kama ilivypangwa.
Alisema ni wakati sasa Bunge hilo, lianze kujadili vipengele kama vile mgombea binafsi, kupinga matokeo ya urais mahakamani, kuwepo kwa tume huru ya uchaguzi na umri wa wabunge na Bunge ili viingizwe na kupitishwa kwenye kikao cha 20 cha Bunge ili Katiba ya Mpito ipitishwe.
 
Wakati Jafo akitoa maelezo yake kuhusu mwongozo huo, baadhi ya wabunge wa upinzani walikuwa wamesha vipaza sauti wakimpinga kwa madai kuwa, suala analotaka siyo la dharura.
 
Baada ya maelezo hayo ya Jafo, mbunge wa Ubungo, John Mnyika (Chadema) naye aliomba mwongozo kwa kanuni ya 47 (1) inayohusu kusimamisha shughuli za Bunge zilizopangwa kwa siku hiyo ili jambo la dharura lijadiliwe.
 
“Mheshimiwa Spika uandikishaji wapiga kura nchi nzima, haujakamilika hata katika mkoa wa Njombe, Watanzania wapo katika sintofahamu ni lini wataandikishwa kwenye daftari la kudumu la wapiga kura,” alisema.
 
Alisema suala hilo ni la dharura na lilishaombewa miongozo zaidi ya mara moja bila majibu, hivyo si vyema Bunge hilo likaahirishwa bila kupatiwa majibu juu ya hatma ya uandikishaji huo wa wapiga kura na kura ya maoni.
 
“Tusitishe shughuli zote tuhakikishe tunajali, majibu yapatikane leo katika mkutano huu wa Bunge, nimeomba miongozo juu ya jambo hili mara mbili na mara zote Serikali haitoi majibu, sasa hakieleweki hapa hadi tupatiwe majibu,” alisema Mnyika.
 
Alisema “Waziri Mkuu yupo hapa anaweza kutoa majibu hapa na tukajadili jambo hili hapa,” alisema Mnyika.
 
Baada ya Mnyika kumaliza kuomba Mwongozo, Spika Makinda alibainisha kuwa hoja hiyo ya Mnyika haina tofauti na Jafo, na zote zipatiwa majibu na Waziri Mkuu wakati akitoa hoja ya kuahirisha Bunge.
 
Hata hivyo, jibu hilo la Spika halikukubaliwa na wabunge hao wa upinzani na ndipo mbunge wa Kasulu Mjini, Moses Machali, alipowasha kipaza sauti bila ruhusa ya Spika na kusema “Hoja hii  haifanani na hoja ya kwanza, ile ya kwanza inataka majibu mkutano wa 20 na hoja hii ya pili inataka majibu mkutano huu.”
 
Wabunge wote wa upinzani wa vyama vya Chadema, NCCR-Mageuzi na CUF, walisimama na kuwasha vipaza sauti huku wakiongea kwa nguvu kuwa hoja hizo hazifanani na ni lazima hoja yao ipatiwe majibu kabla ya shughuli nyingine za Bunge kuendelea.
 
Machali alidakia tena na kusema, “Tunataka majibu, tumechoka kuburuzwa.”
 
Spika Makinda aliwajibu kwa kusema “Anawaburuza nani, nimewaambia kwamba swali lile litajibiwa leo (jana),au njooni basi nyie muendeshe hiki kikao, kama hamtaki kukubali majibu yangu tokeni nje.”
 
Huku wabunge hao wakiwa bado wamesimama na kuimba kuwa wanataka majibu, Spika alimwita Msemaji Kambi ya Upinzani kwenye Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, ili asome maoni ya kambi hiyo juu ya Mswada wa Sheria ya Miamala ya Kielektroniki ya mwaka 2014 na ule wa Makosa ya Kimtandao wa mwaka 2015, lakini hakutoka.
 
Aidha Spika aliendelea na kumtaka Katibu ataje shughuli inayofuata, ambaye aliisoma kwa mara ya kwanza Miswada ya Shera ya Kupata Habari wa mwaka 2015, wa Sheria Vyombo vya Habari wa mwaka 2015, wa Sheria ya Marekebisho ya Sheia ya Ushindani wa mwaka 2015 na wa Sheria ya Tume ya Walimu wa mwaka 2015.
 
Wakati akisema hivyo, baadhi ya wabunge wa upinzani waliendelea kusema kuwa alichofanya siyo utaratibu.
 
Baada ya hapo aliwafafanulia wabunge kuwa kwa mujibu wa kifungu cha 47 kinasema, iwapo Spika ataridhika kwamba jambo hilo ni la dharura na lina maslahi kwa umma basi ataruhusu hoja litolewe kwa muda  dakika tano, na mjadala wa hoja utawezekana kama Spika ataridhika.
 
Pamoja na maelezo hayo, vurugu hizo za wabunge ziliendelea hadi alipoamua kuahirisha kikao hicho hadi jioni.
 
CHANZO MPEKUZI BLOG
 
 

GWAJIMA AMSHAURI MBASHA

Mbasha: "Gwajima Mungu Amenilipa, Njoo Uniombe Msamaha Tumalize Ugomvi"


Licha ya Mchungaji wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima kukanusha mara zote kwamba, hahusiki na kusambaratika kwa ndoa ya Mwimba Injili Flora Mbasha na mumewe, Emmanuel Mbasha, lakini mume huyo ambaye amekuwa akimshutumu Gwajima ameibuka na jipya.


Jipya aliloibuka nalo Mbasha ni kudai kuwa, msala uliompata Mchungaji Gwajima wa kumtolea maneno yenye kuudhi Askofu wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Mwadhama Polycap Kadinali Pendo na kisha kuhojiwa polisi na kupata mshtuko, kuzimia hadi kulazwa hospitali ni malipo ya Mungu kwake kutokana na kilio chake.

Akizungumza na Amani kwa njia ya simu kwa dakika 15 juzi, Mbasha alisema: “Ile hali (kupoteza fahamu) ya Gwajima ni malipo. Mimi nilishasema jamani, mtu akikutendea ubaya malipo ni hapahapa duniani, hakuna kwingine.
 
“Mimi ndoa yangu haipo,  mke wangu anajua yeye anavyoishi. Kwa hivyo mimi nimekuwa nikiishi kwa manung’uniko kila siku, unadhani nini kitatokea kwake?”

Mbasha alikwenda mbele zaidi kwa kutoa tamko na agizo kwa mchungaji huyo kwa kusema:
 
“Tena namwomba Mungu ampe afya Gwajima, akitoka hospitali alikolazwa (TMJ, Dar) anitafute kuniomba msamaha.
 
“Ni vyema na itakuwa vyema zaidi akinitafuta na kuniomba msamaha ili kila mmoja aishi kwa amani. Mimi nisiwe na kinyongo na yeye na wala yeye asiwe na kinyongo na mimi.”
 
Mbasha hakumalizia hapo, alipoulizwa kama kauli ya Gwajima iliyosababisha mtafaruku ilikuwa sawasawa au la! Mbasha alisema:
 
“Hilo atajua yeye mwenyewe na Mungu wake, mimi sijui. Ila ninachojua mimi ni kitu kimoja tu, kwamba Mungu amenilipia basi, sasa aniombe msamaha.”
 
Naye mchungaji mmoja wa kanisa la Gwajima alipopatikana kwa simu na kuulizwa kuhusu madai ya Mbasha, alisema: 
 
“Yule hajui maandiko sawasawa. Hakuna uhusiano wowote kati ya kilichompata mchungaji wangu na hisia zake kuhusu mkewe Flora.
 
“Gwajima na Flora hawana uhusiano wowote usiofaa. Sasa yeye anaposema kalipiwa, kalipiwa kitu gani? Mungu anaweza kulipa jambo la hisia?”

Wiki mbili zilizopita, kwenye Viwanja vya Tanganyika Perkers ambako kuna kanisa,  Gwajima alitoa mahubiri yaliyolenga kumshutumu Kadinali Pengo kwa kitendo chake cha kwenda kinyume na maazimio ya Baraza la Maaskofu Tanzania kuhusu msimamo wao wa Mahakama ya Kadhi nchini.
 
Hali hiyo ilimfanya Gwajima kuitwa Polisi Kituo cha Kati, Dar na kuhojiwa. Akiwa katika mahojiano, ghafla alisikia kizunguzungu, akaanguka na kupoteza fahamu. alikimbizwa katika Hospitali ya Polisi Baracks kisha Hospitali ya TMJ, Dar kwa matibabu zaidi.
 
Juzi, Gwajima aliruhusiwa kutoka hospitalini hapo lakini akachukuliwa hadi Kituo cha Polisi Oysterbay kwa mahojiano zaidi na kuachiwa kwa dhamana.


Chanzo mpekuzi blog


post by;RASHID HAMZA

MAZISHI YA ABDU BONGE MENEJA TIPTOP


Kwenye safari ya mwisho ya Marehemu Abdul Bonge, alivyozikwa Morogoro.


IMG_1363Tip Top Connection ni kundi ambalo limeishi muda mrefu kwenye muziki wa Bongo Fleva, safari hiyo imekuwa ya mafanikio makubwa kutokana na usimamizi wa Marehemu Abdul Bonge.

Kundi hilo limepata pengo kumpoteza kiongozi huyo muhimu, safari yake ya mwisho duniani ilikuwa ni leo, wasanii, ndugu, jamaa na marafiki na watu wengine wameshirikiana kwenye mazishi ya Abdul Bonge ambayo yamefanyika leo Morogoro.

IMG_1006
IMG_1008
IMG_1010
IMG_1013
IMG_1014
IMG_1018
IMG_1020
IMG_1024  IMG_1026
REST IN PEACE
IMG_1036
IMG_1064
IMG_1068
IMG_1076 _ IMG_1106
IMG_1248
IMG_1295
IMG_1363
IMG_1364
IMG_1425
IMG_1437
IMG_1446





IMG_1456

BELLA MKALI AU

Iliponifikia hii Video mpya ya Christian Bella, nimekuwekea na wewe uicheki hapa- ‘Nashindwa’

bellaMuziki wa Christian Bella ni burudani ambayo inamfikia kila mtu, message ya wimbo wa ‘Nani Kama Mama‘ inamgusa kila mtu kwa nafasi yake.

Tulimuona mkali huyu kwenye stage ya Serengeti FIESTA 2014 akipiga bonge la show, na kuna wakati stage alikuwa anaisimamia pekeyake na bado watu wanaikubali kazi yake.

Amekuja na hii mpya mtu wangu, wimbo unaitwa ‘Nashindwa’, tayari VIDEO imetoka na mimi nakusogezea hapa mtu wa Christian Bella uenjoy hii yani.

 

POST BY HASSAIN MTUNDA

j. Aaron kufanya fashion? Diamond na wimbo wake wa mduara.. Darasa na nyimbo mitandaoni #255 @CloudsFM

unnamed
Baada ya mtangazaji Adam Mchomvu kutangaza kwenda China kwa ajili ya kujifunza mambo ya ubunifu, Dj. Aaron wa Clouds FM amesema ameamua kuingia rasmi kwenye mambo ya fashion na kwa sasa anadesign vitu mbalimbali kama nguo zenye asili ya Tanzania za ‘Aarons Wear’ ambazo anategemea kuja kufanya uzinduzi rasmi muda mfupi.
COCO 2Weekend iliyopita Diamond Platnumz aliachia video ya wimbo wake mpya wa ‘Nasema Nawe’ aliomshirikisha Khadija Kopa, akizungumza kwenye 255 Diamond amesema ameamua kuimba mduara kwa sababu ana uwezo wa kufanya muziki wa aina yoyote na ukawa mzuri wimbo aliourekodi mwaka 2012.
Diamond amesema ameamua kufanya video na director Hanscana baada ya kupenda kazi alizozifanya na kuamini atafanya kitu kizuri na kweli ikawa hivyo video ambayo inafanya vizuri kwenye mitandao kwa kuangaliwa na watu wengi.
970948_509952679083997_929953988_n_fullMsanii Darasa amesema suala la wasanii kuuza nyimbo zao online halina faida kwa wasanii badala yake watu wanaouza ndio wanafaidika kwa sababu watu wanaingia kwenye Website kuangalia na kusikiliza nyimbo za wasanii na wengine wanadownload, lakini mwisho wa siku wasanii hawafaidiki chochote kama ambavyo wanapata wamiliki wa Website.

POSTED BY HASSAIN MTUNDA