Jumatano, 1 Aprili 2015

CCM BADO INAKUBALIKA MIKOANI

KINANA AHITIMISHA ZIARA YAKE Ya MIKOA MITATU


Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wananchi wa Moshi mjini kwenye mkutano wa hadhara Bomambuzi viwanja vya shule ya msingi Mandela na kuwaambia kuwa wamekuwa na ushabiki kwa miaka 20 imefika wakati sasa kuamua kuchagua maendeleo kwa manufaa ya maisha yao.


Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana akiwa ameambatana na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye wamekamilisha ziara yao ya mikoa mitatu ikiwemo Dodoma,Arusha na Kilimanjaro,Ziara hiyo ililenga Kuimarisha,kutekeleza na kuhimiza Ilani ya Uchaguzi ya mwaka 2010 ya CCM,ikiwemo pia kusikiliza matatizo ya Wananchi na kuyapatia ufumbuzi.


wananchi wa Moshi mjini wakiwa wamekusanyika kwenye mkutano wa hadhara Bomambuzi viwanja vya shule ya msingi Mandela,wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana alipokuwa akiwahutubia,ambapo aliwaeleza kuwa wamekuwa na ushabiki kwa miaka 20 imefika wakati sasa kuamua kuchagua maendeleo kwa manufaa ya maisha yao.


wananchi wa Moshi mjini wakiwa wamekusanyika kwenye mkutano wa hadhara Bomambuzi viwanja vya shule ya msingi Mandela,wakimsikiliza Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye huku wameweka mikono kichwani kuashiria kuwa miaka 20 kwa upinzani jimbo la Moshi mjini imetosha.


Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia wakazi wa Moshi mjini mkutano wa hadhara Bomambuzi viwanja vya shule ya msingi Mandela na kuwaambie wastuke sasa wasiendelee kukandamizwa na viongozi wasiojali maendeleo yao.


Wakazi wa Moshi mjini wakiwa wamekusanyika kwenye mkutano wa hadhara Bomambuzi viwanja vya shule ya msingi Mandela,wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana alipokuwa akiwahutubia,ambapo aliwaeleza kuwa wamekuwa na ushabiki kwa miaka 20 imefika wakati sasa kuamua kuchagua maendeleo kwa manufaa ya maisha yao.


Msafara wa Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana ukiwasili Moshi Mjini kutokea Wilaya ya Rombo kwa Ziara ya siku kumi ndani ya mkoa wa Kilimanjaro. 

 PAMOJA TUTASHINDA 

 

POSTED BY; RASHID HAMZA $ HASSAIN MTUNDA

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni